'Likes na comments' kwenye mitandao ya kijamii imekuwa ni chanzo cha furaha au mfadhaiko kwa vijana wengi. Je, unalizungumziaje hili?

'Likes na comments' kwenye mitandao ya kijamii imekuwa ni chanzo cha furaha au mfadhaiko kwa vijana wengi. Je, unalizungumziaje hili?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mitandao ya kijamii kwa sasa imekuwa sehemu ya maisha ya watu. Baadhi yao watumiaji hao wamepata uraibu wa hali ya juu kiasi ambacho bora akose chakula lakini awe na bando la kuingia kwenye mitandao ya kijamii (hawa ndio wazee wa stress sasa).

Mitandao ya kijamii watu wamekuwa wakitumia kwa malengo tofauti tofauti. Kuna wanaotumia kibiashara wengi kujifurahisha na wengine kupata habari mbalimbali.

Nikija kwenye hoja, suala la likes na comments limekuwa ni kitovu cha msingi cha raha na ladha ya mitandao ya kijamii. Watu wanafanya ubunifu wa hali ya juu ikiwamo kutuma picha zao bora kabisa ili wapate likes na comment za kutosha. Katika hili watu wanalazimika kuchagua picha wakiwa maeneo mazuri au wakiwa katika hali nzuri ili tu kuvuta hadhira watoe likes ikibidi wacomment. Ndio njia pekee unaweza kufikia hitimisho la kujua post yako gani nzuri au iliyopendwa kwa kuangalia likes na comments za wadau.

Like na comment ni alama ya kukubalika au kupongezwa (Appriciation) kwa kile kitu ulichokipost. Ikitokea kama mtu katumia ubunifu wake wote ili kupata attention aliyoitarajia halafu ikawa tofauti lazima roho iume. Mfano, umepiga picha ukiwa ukiwa sehemu nzuri picha ambayo kwa mtazamo wako ukaiona ndio bora na ya kuvutia kwa wakati huo na ukaamua kuipoist kwenye mtandao halafu itokee baada ya siku tano hakuna mtu aliyelike wala kucomment chochote hapo (Hope kuna kahisia ambako kabaya kuhusu hiyo picha utakapata)

Binafsi pia nikipost picha yangu halafu ikakaa miezi kadhaa haina likes wala reaction yoyote huwa sijisikii vizuri. Kwahiyo hapo inakuja jambo binafsi ni namna gani mtu aliyepost atalichukulia hili jambo. Mwingine atapata hisia za kutengwa, mwingine ataona kama amepost kitu kisicho na maana mwingine ataona amedharauliwa. Hapo ndipo depression inapoanza.

Kutokana na na hali hii kuna jaribio linafanyika la kutaka kuondoa sehemu inayoonesha like na comment ili kuondoa ile hali ya baadhi ya vijana kupata msongo wa mawazo kwa kuhisi hawakubaliki katika jamii zao kwa kuwa kila wakipost vitu vyao mitandaoni wanaona havipokelewi vyema. Hii imepelekea baadhi ya vijana kukata tamaa na kuona wametengwa na jamii.

Kwa upande wangu naona ni sahihi wakificha likes kwa sababu inaondoa matabaka fulani na kuwafanya watu wawe comfortable na kutumia mtandao.
Je wewe mdau wa JamiiForums unalionaje swala hili.
 
Feeling of importance...one of fucking hot ego of every human..but where you want to be appreciated,it's matter of your choice ..
 
These generation X kids need to know that, ten years from today 'likes' wont pay the bills!
 
Ikiwa wewe ni mwanaume basi Kuna tatizo mahali si bure. Yaani usijisikie vizuri kisa hakuna like wala comment kwa post yako, narudia tena kuna tatizo mahali sio bure ,huo wako si uraibu bali ni ulevi wa kupindukia.
 
My personal account huwa naangalia tu watu wangapi nawajua na wananijua wame-like post yangu (comments disabled) huwa sifatilii zipo likes ngapi, wanaonijua ndio huwa walengwa wangu kupata updates kuhusu mimi, waki-like basi najua wana taarifa kuhusu mimi.

Post ikiwa na likes chache haimaanishi kutengwa, nadhani mawasiliano ndio kitu muhimu ktk jamii na ukikosa mawasiliano na watu basi ndio inaumiza zaidi ila hizi likes hazina umuhimu na wala sio kipimo cha kupendwa.
 
Back
Top Bottom