The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Nikiwa nafanya manunuzi madukani, niliingia duka moja nikaulizia bidhaa niliyoitaka nikaambiwa ipo. Kijana niliyemkuta nje ana rangi kama yangu, akanitajia bei na akanitolea bidhaa niliyohitaji. Ilipofika muda wa malipo akanielekeza dirishani nikalipie.
Kufika hapo dirishani nikakuta mvulana wa miaka saba, ndiye anapokea pesa. Ni mtoto mwenye asili ya Asia. Wazazi hawapo dukani ila wamemuacha yeye na huyo kijana ndiyo wanauza.
Nikafikiria watoto wetu tumewapeleka "twisheni". Tangu likizo imeanza watoto wanafukuzwa kwenda "twisheni". Tuna miradi na shughuli mbali mbali za familia ila watoto wetu hawashiriki kabisa.
Hii ni miongoni mwa sababu miradi na biashara za wenzetu zinadumu na wanarithishana vizazi na vizazi. Za kwetu huwa zinakufa na mwenye nazo. Hakuna anayeandaliwa kuendeleza miradi hii. Na hata inapotokea wanarithishwa hawawezi kuziendesha sababu hawana uzoefu. Hajui hata huwa zinafanyikaje.
Watoto wanakatazwa kufanya kazi ili wasichafuke, wasiumie, wasifeli, kumbe ndiyo tunawaandaa kushindwa maisha. Na ndiyo maana watoto wengi wanalaumu wazazi na walezi wao, maana wana mchango mkubwa kwenye maisha yao.
Tunapaswa kubadilika na kuachana na ule msemo wa "urithi wa watoto ni elimu". Tumeona watoto wanarithishwa mali, wanarithishwa miradi, na hata nafasi za uongozi.
TAFAKARI, CHUKUA HATUA!
Mwl. Doris Mboma.