Pre GE2025 Likizo inaisha lini?

Pre GE2025 Likizo inaisha lini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Tanganyika huru. Nilikuwa mapumziko ya likizo ndefu nimerejea tena jukwaani na hii ndio mada yangu ya kwanza.

Kwa sheria na kanuni za Kazi duniani kote kila mfanyakazi anastahili mapumziko ya likizo ya mwezi mmoja katika miezi 12 ya mwaka.

Hili ni takwa la kisheria ndio maana hata marais hustahili hii likizo na uma hutaarifiwa rasmi kuhusu mapumziko ya rais. Kuna baadhi ya watumishi hasa wanaopenda sana kutumia mitandao ya kijamii, hupenda kutoa taarifa kwa kila wafanyacho ikiwepo mapumzikoni likizoni.

Pia soma: Tetesi: - Mtoto pendwa kapatwa na nini? Yuko hoi kwa Madiba, inadaiwa ni sumu

Kama kipindi Hicho cha likizo hawajasafiri kwenda popote, kijijini ama nje ya nchi kulingana na ukwasi ni ngumu kuona mitupio na selfie za kutosha.

Lakini kama wametoka nje mbali na eneo la Kazi kuselfika na kutupia mapichapicha ni jambo lisilo epukika na kwakuwa siku hizi camera tunatembea nazo lazima ushawishike. Kuna kipindi wakati wa mapumziko ya likizo Hayati mwendazake alitupia mapichapicha akiwa kapumzika kwenye miamba na majabali.. Nadhani alikuwa anayapenda sana mawe ndio maana hata akajiita jiwe!

Pia soma: Kumbe RC Makonda yuko Likizo, Uzushi kwamba anaumwa upuuzwe

Likizo ni wakati wa kupumzisha mwili na akili lakini pia ni wakata wa ku 'refresh mind' kwa bata za hapa na pale.. Ni katika kipindi hiki lazima tu utashawishika kutupia matukio mitandaoni..! Hasa kwa wale addicted.

Ukiwa mapumziko ya likizo na ukajikataa kabisa kutoonekana popote hasa kama wewe ni mpenda sifa ni uthubutu wa hali ya juu mno na lazima jamii inayokujua vena ikushangae sana na kutengeneza mijadala mingi

Anaway likizo ya kisheria ni wiki nne! Zikiisha hizi hujarudi kibaruani ni aidha kati ya haya mawili

1. Kuzidisha tetesi
2. Breaking news

Bado tunahesabu siku.. Tuupe muda wakati.

Good morning Tanganyika.❤
 
Wala hakuna aliyekua anajua kama ulikua likizo au hukua likizo zaidi ya hao chawa wako tu wanakuabudu,acha kujipa umuhimu usiokua nao,huna impact yeyote hapa zaidi ya kujaza server za JF kwa mada za kishirikina tu.

Umerudia kwenye zile zile mada zako za kufikirika,huna jipya.
 
Karibu Tena ndugu mshana karibu kwenye kilinge cha waganga wa Simba SC club inabidi mfanye sana ulozi mwaka huu msiwe wa tatu kwenye ligi adios amigos @Cc ephen_
20240727_215048.jpg
 
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Tanganyika huru.. Nilikuwa napumzika ya likizo ndefu nimerejea tena jukwaani na hii ndio mada yangu ya kwanza
Kwa sheria na kanuni za Kazi duniani kote kila mfanyakazi anastahili napumzika ya likizo ya mwezi mmoja katika miezi 12 ya mwaka
Hili ni takwa la kisheria ndio maana hata marais hustahili hii likizo na uma hutaarifiwa rasmi kuhusu mapumziko ya rais
Kuna baadhi ya watumishi hasa wanaopenda sana kutumia mitandao ya kijamii, hupenda kutoa taarifa kwa kila wafanyacho ikiwepo mapumzikoni likizoni

Kama kipindi Hicho cha likizo hawajasafiri kwenda popote, kijijini ama nje ya nchi kulingana na ukwasi ni ngumu kuona mitupio na selfie za kutosha
Lakini kama wametoka nje mbali na eneo la Kazi kuselfika na kutupia mapichapicha ni jambo lisilo epukika na kwakuwa siku hizi camera tunatembea nazo lazima ushawishike
Kuna kipindi wakati wa napumzika ya likizo Hayati mwendazake alitupia mapichapicha akiwa kapumzika kwenye miamba na majabali.. Nadhani alikuwa anayapenda sana mawe ndio maana hata akajiita jiwe!

Likizo ni wakati wa kupumzisha mwili na akili lakini pia ni wakata wa ku 'refresh mind' kwa bata za hapa na pale.. Ni katika kipindi hiki lazima tu utashawishika kutupia matukio mitandaoni..! Hasa kwa wale addicted...
Ukiwa napumzika ya likizo na ukajikataa kabisa kutoonekana popote hasa kama wewe ni mpenda sifa ni uthubutu wa hali ya juu mno na lazima jamii inayokujua vena ikushangae sana na kutengeneza mijadala mingi

Anaway likizo ya kisheria ni wiki nne! Zikiisha hizi hujarudi kibaruani ni aidha kati ya haya mawili
1. Kuzidisha tetesi
2. Breaking news
Bado tunahesabu siku.. Tuupe muda wakati..!

Good morning Tanganyika.❤
Sema tena jezi za Yanga zina laana
 
Kwa kuwasaidia kufungua code, Mshana ameanza kuuliza swali "Likizo itaisha lini?". Ina maana siyo yeye aliye likizoni. Katikati ya maelezo yake, ameelezea mambo kadha wa kadha hususan mambo ya kupenda camera. Lkn mwishoni amemalizia kwa kusema mambo mawili ambayo hutokea kama hujatoka likizoni, na baadae akasema tujipe muda.
 
Back
Top Bottom