Likizo na Pasi Zasitishwa JWTZ. Waliokuwa likizo waitwa warudi kambini

Likizo na Pasi Zasitishwa JWTZ. Waliokuwa likizo waitwa warudi kambini

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesitisha wapiganaji wake kwenda likizo na kuwaita waliokuwa likizo kurudi makambini. Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani kabisa vya kiinteligensia vijulikanavyo kama ‘KAINZI' uamuzi huo umeenda sambamba na kuweka hali ya utayari wa kijeshi (military readiness) kufikia asilimia 50; katika hali ya utulivu na amani nchini hali ya utayari wa kijeshi inakuwa kwenye asilimia 25 hivi.​

Kwa mujibu wa chanzo changu hicho ambacho kimekuwa kikifuatilia mwitikio wa vyombo vyetu vya usalama kufuatia kuongezeka kwa hali ya utete katika eneo la maziwa mazuri vikosi vya jeshi nchini kufikia jana vilikuwa vimesomewa taarifa hiyo ya kusitisha likizo na hata pasi za kutoka makambani huku maafisa wake ambao walikuwa nje ya vituo vyao vya kazi wakitakiwa kurudi makambini. Uamuzi huu hata hivyo haijawa wazi kama unahusu wapiganaji wote nchini au wa Brigedia za Tabora au Brigedia za vikosi maalum.

Baadhi ya vikosi vilisomewa taarifa hiyo jana.

Kwa mujibu wa chanzo hicho cha kuaminika Brigedia za Tembo na Kifaru (Tabora) tayari zimepewa maagizo ya kuwa katika hali ya utayari endapo watahitajika kufanya ‘movement' yoyote ya kijeshi. "Unajua tangu sakata la Rwanda vyombo vyetu vya usalama na inteligensia vimeona kuwa kuna sababu ya msingi ya kujiweka katika hali ya utayari wa kijeshi" kilisema chanzo hicho. Akizidi kufafanua mtoa habari huyo amemdokeza mwandishi kuwa japo jambo hili limetokea wakati huu wa utete hata hivyo ni kawaida pia kwa jeshi kujiweka katika hali ya mazoezi wakiigiza hali ya kivita (war simulation) na hivyo watu wasije wakasoma mengi katika hili.

Nilipojaribu kufuatilia zaidi na kwa kina habari hizi inaonekana kuwa kuna taarifa za kiusalama ambazo pia zinasababisha uamuzi huu kuchukuliwa. Pamoja na uamuzi huu habari hizi zinadokeza pia kuwa JWTZ linaweza kuwaita baadhi ya reserve ili kuliongezea nguvu. Kwa kawaida kama ilivyokuwa kabla ya Vita ya Kagera baadhi ya maafisa wanaoweza kuongeza nguvu jeshini ni pamoja na wale kutoka vyombo vingine vya usalama kama Polisi, Mgambo, Magereza, n.k ambavyo vinaweza kutakiwa kutoa idadi fulani ya watu kujiunga na JWTZ.

Wakati wa Vita ya Kagera kuongeza nguvu jeshi kulilipatia jeshi nguvu ya kufikia watu 100,000 ndani ya wiki chache tu na hivyo kulifanya kuwa miongoni mwa majeshi makubwa ya wakati huo katika Afrika. Pamoja na kujipatia watu kutoka vyombo vingine JWTZ pia linaweza kufungua milango yake kwa watu wanaojitolea kujiunga (volunteers).

Pamoja na maamuzi hiyo vyanzo vyetu vinataarifu kuwa hata wapiganaji wa JWTZ ambao walikuwa wanaandaliwa kwenye shughuli mbalimbali za kulinda amani nao wamesitishwa sasa hivi na wanapelekwa kwenye moja ya mikoa iliyoko mpakani kwa sababu ambazo mtoa habari wetu hakutaka kuziweka wazi mara moja. Hata hivyo hadi hivi sasa hakuna uhamishaji wa vifaa na zana za kijeshi kuelekea maeneo yenye migogoro. Tutaendelea kuwaletea taarifa mpya kwa kadiri tukavyozipata.


Na. M. M. Mwanakijiji
 
wiki iliyopita hapa Arusha wamepita kwenye mashule kutoa tahadhali kuwa watoto wakiona kitu cha mviringo wasikiokote au wakipewa na kupewa maelekezo ya kukirusha kwa wenzao wasikubali..
hii inaonyesha kumesha pambazuka
 
Kama taarifa hii ni ya kweli, ninaamini kuwa serikali yetu itakuwa na sababu ya kutosha kufanya hivyo kwa maslahi na ulinzi wa nchi yetu. Rwanda wametumia watu wa asili ya rwanda walioko tz na wanaojifanya raia wa tz kuchukua siri nyingi za jeshi kwa muda mrefu, sijui kagame alikuwa na nia gani kufanya vile. kuna mambo mengi sana yamejificha ambayo wana usalama wa tz wanajua kuhusiana na rwanda, ndio maana ugomvi wetu na rwanda haujaanzia tu pale kwenye kauli ya rais, kuna mengi yamejificha ambayo rwanda wamekuwa wakitufanyia kitu mbaya sana kisirisiri, wananchi wa kawaida hawawezi kujua ila wana usalama wanajua hili. tumwache rais wetu afanye chochote kila, ninaamini atakuwa amepima mapana na marefu. tuache siasa za vyama vingi katika hili, utaifa kwanza.
 
Mungu ibariki Tanzania na watu wake mungu bariki JWTZ ikiwezekana waseme hata kesho twende volunteers hawa manyang'au wasichezee hii ardhi yetu

msiwe wepesi wa kwenda mtwara kubaka dada zetu nendeni mkabake wanyarwanda..
 
ni muhimu sana kwa jeshi letu kuwa tayari muda wowote kwa batalian za Tabora, kigoma, bukoba etc, ili rwanda wakianza kuchakazwa upande wa drc na makomandoo wa tz, makomandoo wengine wa tz waanze kuwaingilia kinyume upande huu wa bukoba kigoma tuwaminye katikati ya kigali. sijui kagame atakimbilia wapi, idi amini alikimbilia libya, jwtz walikuta ikulu iko empty, kagame kila mtu anamchukia sijui atakimbilia wapi. na kule drc nina uhakika fdlr wataunga mkono jeshi linalopiga kutokea kule. kama kweli tutaamua kumchapa, tunatakiwa kuchapa hadi ikulu, hata akisema haya basi nanyoosha mikono kuwe na cease fire, sisi tuendelee kupiga hakuna cha msamaha hadi arudi msituni.
 
Umesomeka vyema mzee, usikawie kutu update kila upatapo chochote toka mdomoni mwa ka INZI.


Historia haiishiwi wino.
 
Haki ya nani hawa jwtz wanavyotamani kumpiga mtu;
patakuwa hapatoshi, Mungu apitishe tu mbali.

@mzee mwanakijiji,
salimia wote wabeba mabox wenzio huko;
mkiweza rudini tujenge nchi yetu; copy: chama
 
Tanzania hatuna usiri wa vitu nyeti kama hivi?.
usiri gani wakati kuna kamanda yule wa jeshi aliyetorokea rwanda, alikuwa na siri zote alikuwa anampa kagame kuhusu jeshi letu. kagame amekuwa akispy jeshi na nchi zinazozunguka ili atuweke nchi zinazomzunguka mfukoni/kiganjani kama alivyowaweka wanyarwanda. kuna viongozi wengi tu wa jeshi na serikali ni wanyarwanda na hawana royalty kabisa na tz. ni muhimu nchi yetu ianze screening katika kila sector, wanajulikana hawajajificha.
 
Haki ya nani hawa jwtz wanavyotamani kumpiga mtu;
patakuwa hapatoshi, Mungu apitishe tu mbali.

@mzee mwanakijiji,
salimia wote wabeba mabox wenzio huko;
mkiweza rudini tujenge nchi yetu; copy: chama

kwa mchezo waliokuwa wanaufanya kule mtwara usikute wanatamani kwenda kubaka vimwana wa kwa KAGAME..
 
msiwe wepesi wa kwenda mtwara kubaka dada zetu nendeni mkabake wanyarwanda..

Mkuu Crashwise naona unataka kuwaponza, kule hakuna "nchale" ni makombora na kichapo kwa kwenda mbele.

Nawaonea huruma rafiki zangu walioamua kuwa wafunga buti.
 
Last edited by a moderator:
Duh Safari ya Kigali imewadia, but there will be great price to pay economically.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom