Likizo ya Corona kwa wanafunzi: Wasichana 100 wapata ujauzito mkoani Mtwara

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Picha

MIKOA minne imetajwa kuwa kinara wa ndoa za utotoni kipindi hiki ambapo wanafunzi wapo majumbani, kutokana cha mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Serikali ilitangaza kuzifunga shule zote za msingi, sekondari na vyuo Machi 17, mwaka huu kutokana na mlipuko wa janga hilo. Mikoa hiyo ni Ruvuma, Mara, Arusha na Mtwara.
Kwa Mtwara wanafunzi 100 wameripotiwa kupata mimba katika kipindi hiki cha corona.

Akizungumza katika mkutano wa majadiliano, uliofanyika kwa njia ya mtandao wenye kauli mbiu ‘Usawa wa Kijinsia’ ulioandaliwa na UN Women na Plan International, ukishirikisha na wadau mbalimbali, Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebecca Gyumi alisema miaka 25 ya kimkakati ya Beijing, bado wanawake wana changamoto kubwa katika kusaka usawa wa jinsia

Alisema kipindi cha ‘lockdown’ wanawake na wasichana, wameendelea kupitia vipindi vigumu kwa kuyumba kiuchumi ikiwa ni pamoja na kufanyiwa ukatili wa kijinsia.

“Wasichana wanalazimishwa kuolewa wakiwa katika umri mdogo wakati ambao wamepumzishwa nyumbani kutokana na ugonjwa wa Covid-19, ukatili pia umeongezeka, na mimba za utotoni,” alisema Gyumi.

Alisema pia kipindi hiki cha corona, wanawake wengi wasio katika sekta rasmi wakiwemo mama ntilie, wafanyabiashara sokoni, wanawake wanaofanya kwenye hoteli na sekta nyingine za utalii, wameathirika zaidi kutokana na mlipuko wa janga hilo.

Mkuu wa Idara ya Ushirikiano kutoka Ubalozi wa Finland, Riikka Roatikainen alisema ukatili wa majumbani, umeongezeka katika kipindi hiki cha mlipuko wa Covid 19. Kwamba uwazi unahitajika kwa kutoa takwimu sahihi na utoaji wa habari sahihi na kuwapa nguvu wanawake katika ngazi za maamuzi.

“Kwa kipindi hiki cha janga la Covid- 19, upatikanaji wa taarifa sahihi ni haki kwa kila mwananchi. Hivyo ni muhimu mbinu zinazotumika ziangalie mahitaji ya taarifa kwa makundi mbalimbali ya kijamii na vyombo na muda sahihi wa kupeleka taarifa kwa makundi hayo hasa vijijini,” alisema.

Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Lihundi alisema ugonjwa wa Covid-19 umeleta changamoto kubwa kwa wanawake na kuitaka serikali iweke kipaumbele na nguvu zaidi katika huduma za jamii, ikiwemo sekta ya elimu, maji na afya.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Ajira Duniani (ILO) mwaka 2006, zaidi ya asilimia 80 ya wanawake wapo katika ajira zisizo rasmi, kama vile sokoni kwenye mikusanyiko mikubwa, jambo linalowaweka katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Alisema pia kwa miaka mingi kundi hilo limekuwa lipo chini kielimu. Taarifa ya UNESCO ya 2019, inaonesha kuwa kiwango cha elimu kwa watu wazima ni asilimia 77.89, ambapo wanaume ni asilimia 83 na wanawake ni asilimia 73.09

“Takwimu hizi ni ushahidi wa wazi kuwa wanawake wameachwa nyuma katika masuala mbalimbali. Tofauti hiyo ya wanawake kuwa nyuma utaiona pia katika nyanja ya ufikiwaji wa taaarifa sahihi kwa wakati mfano magazeti, redio, televisheni na mitandao ya kijamii,” alisema.
Alisema hali hiyo kwa kiasi kikubwa inatokana na mifumo ya jamii ya kutokuwa na mgawanyo sawa wa majukumu.

Wanawake kwa kiasi kikubwa wameelemewa na majukumu ya kulea familia na kazi za kutoa huduma, ambazo zinasababisha kukosa muda wa majukumu ya kiuchumi, kisiasa, na hata kupata taarifa sahihi na kwa wakati.

Alisema janga hili la virusi vya corona, limeibua changamoto mpya katika familia na jamii, hususani kwa watoto wa kike na wa kiume, ambao shule zimefungwa na wapo majumbani Liundi alisema takwimu zinaonesha kuwa takribani asilimia 60 ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, hutokea majumbani na wanaofanya vitendo hivyo ni ndugu wa karibu au majirani.

“Kwa ujumla, ukatili wa kijinsia huongezeka sana wakati wa majanga kama haya, si tu kwa watoto bali pia kwa wanawake,”alisema.

Liundi alisema wanawake wengi wapo katika sekta isiyo rasmi, wakijishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile mama lishe, biashara sokoni, shughuli za viwandani na wafanyakazi wa majumbani.

Kazi hizo zinahusisha kutoka mazingira ya nyumbani na kukutana na watu mara nyingi katika mazingira yenye misongamano. Hali hii inawaweka katika mazingira hatarishi ya kupata virusi hivi vya corona.
 
Zito atakuja kuwatetea hapa
 
Alafu wanalalamika kwamba kusini wanabaguliwa kimaendeleo.
 
Na mbingu tutaiona tu na kuume kwa baba tutaketi na kuimba nyimbo za kumsifu yeye alie juu..😂

Wanaume wote tupige kelele..
 
Hilo tumbo pichani ni la miezi miwili Tu baada ya shule Kufungwa au kuna siasa hapo Maana Tanzania kila kitu Ni siasa
 
Mimba bwana ikiwa kwa mwanafunzi ni jinai ila kwenye ndoa ni kitu kinatafutwa hasa kwa gharama kubwa
 
Hakuna sehemu salama kwa watoto tena...wanabeba mimba wakiwa majumbani mwao mbele za baba zao, mama, shangaz, na wajomba zao. Anyway kubeba mimba ni kiherehere chao walee mimba salama wazazi mwiko shuleni.
 
Picha

MIKOA minne imetajwa kuwa kinara wa ndoa za utotoni kipindi hiki ambapo wanafunzi wapo majumbani, kutokana cha mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Serikali ilitangaza kuzifunga shule zote za msingi, sekondari na vyuo Machi 17, mwaka huu kutokana na mlipuko wa janga hilo. Mikoa hiyo ni Ruvuma, Mara, Arusha na Mtwara.
Kwa Mtwara wanafunzi 100 wameripotiwa kupata mimba katika kipindi hiki cha corona.

Akizungumza katika mkutano wa majadiliano, uliofanyika kwa njia ya mtandao wenye kauli mbiu ‘Usawa wa Kijinsia’ ulioandaliwa na UN Women na Plan International, ukishirikisha na wadau mbalimbali, Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebecca Gyumi alisema miaka 25 ya kimkakati ya Beijing, bado wanawake wana changamoto kubwa katika kusaka usawa wa jinsia

Alisema kipindi cha ‘lockdown’ wanawake na wasichana, wameendelea kupitia vipindi vigumu kwa kuyumba kiuchumi ikiwa ni pamoja na kufanyiwa ukatili wa kijinsia.

“Wasichana wanalazimishwa kuolewa wakiwa katika umri mdogo wakati ambao wamepumzishwa nyumbani kutokana na ugonjwa wa Covid-19, ukatili pia umeongezeka, na mimba za utotoni,” alisema Gyumi.

Alisema pia kipindi hiki cha corona, wanawake wengi wasio katika sekta rasmi wakiwemo mama ntilie, wafanyabiashara sokoni, wanawake wanaofanya kwenye hoteli na sekta nyingine za utalii, wameathirika zaidi kutokana na mlipuko wa janga hilo.

Mkuu wa Idara ya Ushirikiano kutoka Ubalozi wa Finland, Riikka Roatikainen alisema ukatili wa majumbani, umeongezeka katika kipindi hiki cha mlipuko wa Covid 19. Kwamba uwazi unahitajika kwa kutoa takwimu sahihi na utoaji wa habari sahihi na kuwapa nguvu wanawake katika ngazi za maamuzi.

“Kwa kipindi hiki cha janga la Covid- 19, upatikanaji wa taarifa sahihi ni haki kwa kila mwananchi. Hivyo ni muhimu mbinu zinazotumika ziangalie mahitaji ya taarifa kwa makundi mbalimbali ya kijamii na vyombo na muda sahihi wa kupeleka taarifa kwa makundi hayo hasa vijijini,” alisema.

Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Lihundi alisema ugonjwa wa Covid-19 umeleta changamoto kubwa kwa wanawake na kuitaka serikali iweke kipaumbele na nguvu zaidi katika huduma za jamii, ikiwemo sekta ya elimu, maji na afya.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Ajira Duniani (ILO) mwaka 2006, zaidi ya asilimia 80 ya wanawake wapo katika ajira zisizo rasmi, kama vile sokoni kwenye mikusanyiko mikubwa, jambo linalowaweka katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Alisema pia kwa miaka mingi kundi hilo limekuwa lipo chini kielimu. Taarifa ya UNESCO ya 2019, inaonesha kuwa kiwango cha elimu kwa watu wazima ni asilimia 77.89, ambapo wanaume ni asilimia 83 na wanawake ni asilimia 73.09

“Takwimu hizi ni ushahidi wa wazi kuwa wanawake wameachwa nyuma katika masuala mbalimbali. Tofauti hiyo ya wanawake kuwa nyuma utaiona pia katika nyanja ya ufikiwaji wa taaarifa sahihi kwa wakati mfano magazeti, redio, televisheni na mitandao ya kijamii,” alisema.
Alisema hali hiyo kwa kiasi kikubwa inatokana na mifumo ya jamii ya kutokuwa na mgawanyo sawa wa majukumu.

Wanawake kwa kiasi kikubwa wameelemewa na majukumu ya kulea familia na kazi za kutoa huduma, ambazo zinasababisha kukosa muda wa majukumu ya kiuchumi, kisiasa, na hata kupata taarifa sahihi na kwa wakati.

Alisema janga hili la virusi vya corona, limeibua changamoto mpya katika familia na jamii, hususani kwa watoto wa kike na wa kiume, ambao shule zimefungwa na wapo majumbani Liundi alisema takwimu zinaonesha kuwa takribani asilimia 60 ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, hutokea majumbani na wanaofanya vitendo hivyo ni ndugu wa karibu au majirani.

“Kwa ujumla, ukatili wa kijinsia huongezeka sana wakati wa majanga kama haya, si tu kwa watoto bali pia kwa wanawake,”alisema.

Liundi alisema wanawake wengi wapo katika sekta isiyo rasmi, wakijishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile mama lishe, biashara sokoni, shughuli za viwandani na wafanyakazi wa majumbani.

Kazi hizo zinahusisha kutoka mazingira ya nyumbani na kukutana na watu mara nyingi katika mazingira yenye misongamano. Hali hii inawaweka katika mazingira hatarishi ya kupata virusi hivi vya corona.
Hakuna shida kwani watoto watakaozaliwa wote watasoma.
 
Rafiki yangu ni mwalimu mkoani huko, niliongea naye akasema wazazi wanalalamika mabinti hawashikiki mtaani ni bora tu shule zifunguliwe.
 
Soon we gonna celebrate baby boom! Serikali ianze kujiandaa kimkakati maana miaka michache ijayo huduma za kijamii zilizopo hazitatosha - madarasa, hospitals, hadi matundu ya vyoo! Watunga sera walione hilo na walifanyie kazi mapema maana patakuwa hapatoshi.
 
Back
Top Bottom