Lile Jambo kutoka kwa Rais Samia ni Leo, tega masikio yote mawili

Tuna imani na Samia, hali mradi yule shetani yupo kuzimu, tumpe ushirikiano mama.

Dosari yake kwangu ni kuingizwa mkenge kesi ya Mbowe tu, lakini muda anao wa kurekebisha na DPP kamteuwa yeye.
Kesi ya Mbowe itaamuliwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.

Huwezi kutumia makomandoo wa nchi kienyeji enyeji!
 
Chuki binafsi!
 
Wazee wa kusifia
Mlimsifia JPM mpaka ikafika muda akikosea hajui kama kakosea maana yote mnasifia, kuna wakati alipuyanga ubabe kila mahala lakini hamkumwambia ukweli kwa sababu mlishamuaminisha yuko correct kila nyanja.

Alikataa kupandisha madaraja watumishi mkashangilia eti acha ajenge nchi, kaja SSH kupandisha madaraja watumishi mnashangilia pia.

Nikumbusheni bado tupo uchumi wa kati au tumefika uchumi wa juu zaidi?
 
Bwana Yesu asifiwe wapendwa.

Kama tulivyokwishatangaziwa na Mwenezi wa CCM komredi Shaka kuwa leo Rais Samia atakuwa na jambo letu.

Tega sikio hapa hapa bwashee.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
Watu kwa sasa tuna mambo mengi ya kufanya ili kujitafutia mkate wetu wa kila siku.

Hayo mambo ya kushinda kwenye tv kisa kumtazama mwana siasa hatuna.
 
Jambo linatoka kwenye BRAIN, nadhani unanielewa. Jambo lilitoka juzi kutoka kwenye kamati ya Nobel Prize, yenye BRAIN, jambo toka kwenye brain! BRAIN iko wapi ya kutoa jambo?
Ni wachache sana watakuelewa na kwa huyo mleta uzi ndiyo kabisa umemtupa pwani ya nungwi.
 
Hakuna cha maana sana sana Chato Mkoa mpya.
Jambo kubwa Ni umoja wa kitaifa na Amani, Akitoa amri wafungwa wote wa kisiasa na mashauri tata yafutwe pia aruhusu mchako wa Katiba mpya, Hilo litakuwa Jambo kubwa na muhimu kwa umoja na ustawi wa taifa letu.
Kijambo Cha Chato kuwa mkoa Ni mwendelezo wa legacy za kijinga, na kuharibu kulipoza kundi Fulani lenye Maswali Magumu yasiyo na majibu mepesi.
 
Aisee na wewe huna kazi yaani unawacha kufanya kazi zako unawafuatilia hao ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…