Lile katazo la watoto kutokaa bweni ilikuwa ni funika kombe?

Lile katazo la watoto kutokaa bweni ilikuwa ni funika kombe?

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
762
Reaction score
1,597
Sasa Mimi huwa najaribu kujiuliza haya matamko huwa ya faida gani? Kwani Serikali inakataza Mambo halafu huoni utekelezaji wake hii inamanisha Ni kutengeneza mazingira ya rushwa au serikali Haina meno? Kama ni hivyo Haina sababu ya kukataa.
 
Aisee!! Me mwenyewe nimeshangaa Sana.

Hii likizo ya pasaka mtoto wa jilani yangu alirudi yupo STD 3 alikuwa anakaa bweni. Baada ya Pasaka amerudishwa shule.

Ndo najiuliza hivi lile tamko ilikuwa ni geresha ama vipi?
 
Mi pia nimeshangaa kaka yangu mtoto wake wa darasa la nne karudi bweni. Nikamuuliza vipi si imekatazwa? akasema siasa tu.
 
Sheria nyingi katika nchi hii ni maneno ya mtu yeyote anaeamka na kukutana na malalamiko sehemu basi anaamua kwenda kuropoka tu sehemu yake
Au mkuu wa mkoa, wa wilaya na hata waziri

Huwezi kukuta mahali sheria imepita nchi nzima tena kwa maandishi na likapita
Tunavyojua sheria inapopitishwa ni kwa maandishi tena nchi nzima

Sisi sheria zetu zinasemwa na mtu kwa utashi wake tu na hapo usitegemee ni sheria bali uozo tu
 
Waraka ulisema kwa watakao hutaji waombe vibali maalumu... Kwahio watu wametumia mwanya wa kibali maalum... Tz usenge mwingi
 
Sasa Mimi huwa najaribu kujiuliza haya matamko huwa ya faida gani? Kwani Serikali inakataza Mambo halafu huoni utekelezaji wake hii inamanisha Ni kutengeneza mazingira ya rushwa au serikali Haina meno? Kama ni hivyo Haina sababu ya kukataa.
Wamiliki wa shule wengi ni hao mawaziri, wabunge na watu wao wa karibu wenye uchumi mkubwa.

Wamiliki wa shule hizi kupotia umoja wao, wanatengeneza tamko la pamoja , kikao kinaondoka na azimio la kuendelea na bweni.

Kusimamia hili linataka roho ngumu kulisimamia.
 
Na viongozi wanaangalia, sasa sijui wanapingane ushoga bila kwanza kuzuia boarding maana kwa sehemu kubwa ndiyo chanzo
 
Back
Top Bottom