Lile rundo la marais katika nchi moja limeenda wapi?

Lile rundo la marais katika nchi moja limeenda wapi?

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
542
Reaction score
735
Wana bodi,

Miaka miwili kama sio mitatu iliyopita tulizoea kusikia watu wakijiita.. Rais wa kawe, rais wa mbagala, manzese, kiwalani, salasala, mara rais wa wasafi, rais wa kimara temboni, nakadharika.

Hiyo ilipekea hata mimi kidogo nitake kurudi kwetu nikajiite rais wa kalenga na maeneo yake kama vile kiponzelo, tosamaganga, ipamba, mangalali, nzihi, magubike, kidamali na nyamihuu.

Ila kwa kipindi hiki kumekuwa na ukimya uliotawala juu ya hawa ma rais wengi waliotamalaki kipindi kilichopita, sasa sababu ya ukimya wao ni nn?

Kwa sasa naona rais mwingine ukiacha rais wa nchi ni rais wa TFF pekee anayesikika akitajwa kwa cheo hicho cha urais....

Jamani, naombeni kujua walikoenda hawa marais wetu hata kama ni ziara za nje ya nchi mbona ni mda mrefu sana?
=======================
Nimeagiza lita mbili za ULANZI hapa huku nikisubiri majibu kutoka kwenu wanajukwaa....
=========================

kALEnga kidamali
 
Wako jela...wengine waliikataa hiyo title ya Raisi e.g. kitale Raisi wa mateja
 
Agiza mbavu za mbwa ushushie huo ulanzi niko ipogolo hapa nakuja kulipa!(Rais wa wala mbwa).
 
Marais wale wote walikumbwa na UWAFAM(UKATA WA FEDHA MFUKONI)wakafa wote.Tumebakia na mbabe wa vita tu rais ya daresalama
 
Back
Top Bottom