Lililoitwa Sakata la Bandari: Pumba zimeanza kujitenga na Mchele

Lililoitwa Sakata la Bandari: Pumba zimeanza kujitenga na Mchele

It is easy to fool people than to convince them that they have been fooled.

Lord denning mimi nimekuelewa ila ni kazi kubwa kwa aliyekaririshwa kukuelewa.
Hongera sana mkuu kwa kuujua ukweli.

Siku zote mimi Lord Denning nimekuwa mtu wa kutoa facts humu JF na hii ndo heshima yangu.

Kamwe Lord Denning sio mtu wa siasa za matijaka na hovyo hovyo
 
15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao
 
Wataalamu wa siasa za nchi hii tuliposimama na Rais Samia kutetea uwekezaji wa Bandarini tulionekana sie ni machawa na tukasemwa sana.

Tuliposema kuwa hizi kelele za Bandari kuuzwa sijui nchi imeuzwa ni maneno ya chuki na uzandiki kukwamisha mipango mizuri ya Rais wetu kwenye uchumi wetu ili kuleta mapinduzi ya kiuchumi tulionekana sie tumehongwa na ni wapigaji tu.

Tulisema haya tukijua na tukiwa na ushahidi kuwa hawa watu wamekuwa wakinufaika na upigaji mkubwa ambao umekuwa unafanyika pale bandarini na wanafanya haya ili kutengeneza tension kwa muwekezaji huyu ili tu asije na waendelee kulila hili taifa letu.

Baada ya watu wenye akili kuujua ukweli na Kuanza kuelewa hoja zetu mambo yameanza kubadilika hakika

Walianza wasomi wachache, wakaja KKKT, sasa ACT Wazalendo wametuelewa na wamefanya uchambuzi murua kuunga mkono uwekezaji wa Bandarini.

Wale wengine ambao napenda kuwaita chuki fc ni kama hawasikilizwi tena. Wanaendelea kusoma waraka wao kila siku ila ni kama wamepuuzwa mazima na wananchi wanaojua kweli na wanafahamu kweli inawaweka huru.

Hayo yote tisa, kumi ni kikundi maslahi na chuki kinachotumiwa ili kumkwamisha Rais Samia. Kundi hili linaongozwa na mwanasheria Mwabukusi, mvuta bange Mdude Nyangali na aliyekimbia upadre Dkt Slaa.

Mara ya kwanza waliitisha maandamano kwa diasporas eti waandamane huko ughaibuni kwenye balozi za UAE, wakapuuzwa vibaya sana.

Jana wametoa eti siku 30 kwa serikali kuachana na Mkataba wa Bandari na walitegemea wataugwa mkono ila uzuri wamepuuzwa tena vibaya sana.


Narudia kusema humu. Ukweli una tabia ya kutembea taratibu sana ila uzuri wake ni kwamba lazima ufike tu.

Ukweli umeshafika na Watanzania wamejua kuwa hakuna Bandari iliyouzwa, IGA inahusu ushirikiano katika uwekezaji wa sehemu ndogo tlya Bandari ya Dar es Salaam ambayo ni baadhi ya Gati za Terminal 1 tu na ndo mana Mamlaka ya Bandari imeendelea kutanganza tenda kwenye maeneo mengine.

Baada ya huu ukweli sasa naona hoja ya Bandari kuuzwa sijui kugawiwa kwa waarabu imeanza kufa rasmi.

Wale TEC na wazandiki wenzao ni kama wamekuwa machizi kung'ang'ania vitu ambavyo tayari ukweli umeshaamua mustakabali wake.

Poleni sana Wazandiki. Kweli Pumba zimeanza kujitenga na Mchele.

Hongereni kwa ushindi Team Wazalendo.


Shida yenu nyie vijana ni moja Tu

Hamjibu hoja, hamjibu maswali it's like mnatetea mambo ambayo hamjui au hamna details za kutosha

Hao ambao wanapiga makelele ukiwasikiliza inaonesha wanajua wanachokisema kuliko nyie mnao tea

Me ningekuelewa kama ungekuja na majibu ya hoja zao
 
MWALIMU NYERERE ANAMALIZA KWA USHAIRI KWENYE KITABU CHAKE.

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.

Ole wake Tanzania Tusipoisaidia
Niwezalo nimelifanya kushauri na kuonya nimeonya.

tahadhali nimetoa ushauri na kuonya nimeshatoka kitini zaidi nifanye nini.

Namlilia Jaalia atumulikie njia Tanzania ailinde WAOVU wasiishinde.

Amina Tena Amina Amina Tena amina


UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
MWALIMU JK NYERERE
 
Shida yenu nyie vijana ni moja Tu

Hamjibu hoja, hamjibu maswali it's like mnatetea mambo ambayo hamjui au hamna details za kutosha

Hao ambao wanapiga makelele ukiwasikiliza inaonesha wanajua wanachokisema kuliko nyie mnao tea

Me ningekuelewa kama ungekuja na majibu ya hoja zao
Wanajua nini? Wametoa hoja gani?
 
Huu ushahidi wa upigaji ndiyo mtuonyeshe sasa ambao hatuna upande ama la mnawashtaki mahakamani kwa huo ushahidi mlio nao
 
Bada ya huu ukweli sasa naona hoja ya Bandari kuuzwa sijui kugawiwa kwa waarabu imeanza kufa rasmi.
Hujaona kuondolewa kwa muswada wa serikali kuhusu rasilimali uliotaka kurekebisha sheria ili DP World apewe bandari? Hujaona tenda ya baadhi ya gati sasa zinatangazwa hadharani? Unafikiri hayo yangefanyika? Akili itawakaa tu sawa
 
Kinachopingwa siyo Uwekezaji, kinachopingwa ni mkataba wa uwekezaji!
Kama hawapingi uwekezaji TEC wangesema bandari tuendeshe sisi wenyewe wakati wanajua mitanzania ndo tunaifirisi bandari yetu?
 
Naomba kupata CV yako,Ili tuilinganishe na viongozi wa TEC! Ahsante

Badala ya kujibu hoja, unabwabwaja, Kama chama cha mawakili Tanganyika (TLS) ,wamesena mkataba mbovu, wewe ni nani unayeukubali.
 
Hujaona kuondolewa kwa muswada wa serikali kuhusu rasilimali uliotaka kurekebisha sheria ili DP World apewe bandari? Hujaona tenda ya baadhi ya gati sasa zinatangazwa hadharani? Unafikiri hayo yangefanyika? Akili itawakaa tu sawa
Kwa akili yako uwekezaji wa bandarini unahusiana kivipi na masuala ya maliasilia?
 
Back
Top Bottom