DOKEZO Limeshafika ghorofa ya 13 na linaendelea, lakini nguzo kama njiti za kiberiti

DOKEZO Limeshafika ghorofa ya 13 na linaendelea, lakini nguzo kama njiti za kiberiti

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Na ndio maana nimetoa angalizo, maana kuna jengo lilishawahi kuanguka kule posta na watu walikufa, na wahusika waliwekwa ndani na hatimae wakaachiwa, lakini waliopoteza maisha ndio imetoka,sasa kama naona kitu ambacho hata kwa macho tu kinatia shaka inabidi wahusika wakajiridhishe.
🥲
 
Lile liloanguka mwenye gorofa alikuwa anavunja kuta chini ili aongeze mafremu.tumeambiwa imeundwa tume.yaani Hadi kwa kesi hii nyepesi ambayo ushahidi wake upo wazi wanaunda time na kuwa lipa hela.hii ndo mwili mkubwa akili KISODA
Wazushi hawa

Ndomana nasema inatakiwa gorofa zote bomu huko kko zishuke chini tu tena ikiwezekana kwa pamoja yaani kariakoo kuwa na disaster tu naona viongozi ndy watatia akili

Ova
 
Usihofu, likianguka na kuua watu tutawakamata wote waliohusika, hadi wachangishaji nao watafikiwa
Na pia itagundulika hao ''wachangishaji'' ni ''wajanja'' wanaotumia hiyo fursa kupata fedha za kuendeshea maisha yao ya mbwembwe na kutesa.
 
Mkuu, mambo ya ujenzi hayapimwi kwa macho, embu jiongeze kidogo.
Kwani kosa lake n lipi hapo? We mwenye uelewa si ungemueleza kuliko kumshit! Hapo hujamsaidia chochote. Kama ana wasiwasi kwa ujinga wake(kama unavyohisi),we mjanja mpe nondo. Kwani aliyejua lililoleta maafa itatokea ni nani? Lingeonekana kuwa imara lisingeshuka. Hivyo mleta mada nae,wasi wasi wake una tija.
 
Haya mambo hayafanywi kienyeji enyeji tu. Lazima mtu awe na permit na authorization kutoka kwa mamlaka husika; na engineer anakuwa ame approve michoro ya hilo jengo kuwa ujenzi huo ni salama. Kama hujui kitu unauliza ufahamishwe...

Mchana mwema!
Wazee wa Permit na Authorization...viingereza vingi kumbe upuuzi mtupu.
 
Unaweza ukawa na hoja lakini Strength haipimwi kwa unene Wa beam! ingefaa ukaweka structure ikoje ili tuichambue!

Note: Jengo linaweza kuwa na column/beam nyembamba lakini zikawa ni nyingi ili kufanya load distribution kuwa safe!.

Kwahiyo ipendeze sasa kuangalia structure kwanza kabla ya kulaumu
Na huo ujirani ukoje
 
Na huo ujirani ukoje
Huo ujirani kati ya ghorofa moja na lingine ni kosa. Msingi hauko salama. Ama wa ghorofa la zamani au hata jipya. Ukubwa wa kiwanja cha kujenga ghorofa si salama. Pia ni kinyume na sheria ya mipango miji ukubwa wa kiwanja cha ghorofa unapaswa kuanzia 2000sqm mpaka 4000sqm, mpaka 8000sqm hadi 20,000sqm kwa ghorofa ndefu. Umbali unaanzia 10m mpaka 20m kwa mujibu wa sheria.


 
Back
Top Bottom