Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daah nimecheka sana HAWAMU..😅Huyu naye, madhara ya kuogopa umande, hawamu na kula ndiyo nini!
Hapo mbona mahesabu tu mshikaji. Yaani ile unaona dude limeegemea kwenu we unaenda upande wa lenyewe. Kitambo zipigane busu we uko zako mtaroni unazicheki tu kama mechi ya simba na yanga yaniSio kwa ubaya ila nauliza dereva wa hiace kaponaje hapo ilihali ilikuwa ni head to head collission? Naona hapo mwisho wanasema amekamatwa kwa ajili ya mahojiano. HOW?
Hilo tuta halitoruhusu gari la nyuma kulipita gari la mbele over take. Hiyo hali inatakiwa tu pale penye njia nne na kuendeleaUmeelewa lakini mantiki ya point yangu ya kwenye comment hiyo uliyonukuu??
Hata kama dereva angekuwa kipofu, endapo kama barabara hiyo ingejengwa kwa kuzingatia hayo masuala niliyoeleza wala ajali hiyo isingeweza kutokea, ingezuilika.
Tuta, Ukingo au gingi kubwa kati kati ya barabara vingeweza kuzuia magari yanayopishana kuweza kukaribiana na kugongana uso kwa uso. Tuta au gingi lingekuwa kizuizi 'barrier' cha kulizuia gari la upande mmoja wa barabara kuvuka na kwenda kulivamia gari linalopita upande wa pili wa barabara hivyo kuzuia ajali kutokea.
Njia za London ni nyembamba kuliko hizi zetu na bado ni sehem salama sana kuendesha gari ,ukienda hapo Comoro ndio kabisa sio barabara ni njia na bado wako salamaUkichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba Kiini hasa cha mkasa huu ni uduni wa miundombinu ya barabara hapa Tanzania. Barabara ni nyembamba sana, 'lanes' za kupita magari hazijatenganishwa kwa matuta, kingo au magingi
Mungu awalaze mahala pema wanapostahili
Watu 13 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kufuatia ajali ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace lililokuwa likitokea Somanga kuelekea Kilwa Mkoani Lindi kugongana uso kwa uso na lori la mafuta leo April 22,2024 katika Kijiji cha Somanga.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika barabara kuu ya Lindi - Kibiti ambapo amesema chanzo cha ajali ni Dereva wa lori kuhama upande wake na kuingia upande wa Hiace na kugongana uso kwa uso.
Majeruhi sita wanapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Tingi huku miili ya waliofariki ikihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.
Kamanda Imori amesema Mashuhuda wamesema Dereva wa lori amelewa na walimuona akiwa anayumba na kumgonga Mwendesha baiskeli kabla ya ajali hyo ya gari, hivyo atafanyiwa vipimo na ikibainika alikunywa pombe kupita kiasi atachukuliwa hatua “Dereva wa lori na wa Hiace wote tumewakamata kwa mahojiano”