Debby the FEMINIST
Member
- May 4, 2020
- 32
- 37
Afisa Kilimo kutoka kata ya Milola halmashauri ya manispaa ya Lindi ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kula fedha kiasi cha shilingi Milioni 5 za mahindi ya ruzuku kwa wananchi wa kijiji cha Milola B.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga amekiri juu ya kutiwa mbaroni kwa afisa kilimo huyo akisema mamlaka zinaendelea na hatua zaidi lakini kikubwa ni kupatikana kwa fedha hizo na wananchi wapatiwe mahindi.
Ndemanga amesema Wilaya ya Lindi ilipokea mahindi kwaajili ya chakula kutoka kwa wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula NFRA ambayo yanauzwa kwa wananchi kwa bei nafuu ya shilingi 700 kwa kilo moja ili waweze kupata chakula na kukabiliana na bei ya vyakula sokoni.
Ndemanga ameeleza kuwa wasimamizi wa zoezi hilo kwenye ngazi za vijiji walikuwa ni watendaji wa kata na Maafisa kilimo ambao baada ya kupokea fedha kutoka kwa wananchi wanapaswa kuingiza fedha hizo kwenye akaunti ya benki ya NFRA jambo ambalo halikufanywa na afisa kilimo huyo baada ya kuchukua fedha za wananchi.
Kwa upande wa Mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Lindi Juma Mnwele amesema mtumishi huyo aliwekwa ndani tangu Februari 10,2023 na hadi kufikia Februari 15 kulikuwa na taratibu za kumtoa ndani ili akatafute fedha hizo kwani alishakiri kutenda jambo hilo.