Lindi: Maofisa wa Magereza wanaotuhumiwa kwa mauaji wafikishwa Mahakamani mara ya nne

Lindi: Maofisa wa Magereza wanaotuhumiwa kwa mauaji wafikishwa Mahakamani mara ya nne

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Maafisa watatu wa magereza wanaotuhumiwa kwa mauaji ya mfungwa Mkoani Lindi, Abdallah Ngalumbale, wameendelea kusota rumande baada ya shauri la kesi yao kusikilizwa kwa njia ya mtandao, leo Agosti 3, 2022.

Watuhumiwa hao wamefikishwa Mahakamani kwa mara ya 4 ambapo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Lindi, Consolata Singano aliahirishwa shauri hilo hadi Agosti 15, 2022 kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika .

Watuhumiwa ni ACP Girbert Sindani ambaye ni Mkuu wa Gereza la Liwale, Sajenti Yusuph Selemani na Coplo Fadhil Mafwad.



Video: Azam TV

Pia soma:

Kesi ya Mauaji ya Mkuu wa Gereza la Liwale na wenzake yasikilizwa Mahakamani, yaahirishwa leo Julai 6, 2022

Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Liwale kortini kwa mauaji
 
Wajiandae tu kuvaa jezi za bluu maskini Uyui,Isanga&Maweni kambi zinawasubiri maisha bana
 
Wasimamizi wa wafungwa nao wawa wafungwa
Sio wafungwa hao ni mahabusu mpaka pale kesi yao itakapo amuliwa.

Lakini dah mtu kama ACP( Assistant Commissioner of Prison) naye kajumuishwa.

Sagent na huyo kopolo hakuna tatizo.

Ila hao ujera jera ni asili yao hata wakifungwa watakuwa wamerudi nyumbani.
 
Back
Top Bottom