Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Januari 11, 2023 imefunguliwa Kesi ya Uhujumu Uchumi namba ECO.NO. 1/2023 Katika Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mhe. Mariam Mchomba.
Washitakiwa ni Bw. REUBEN NDIZA MFUNE, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali na Bw. JUMA MASATU KASOGA, ambaye kwa sasa ni Mhasibu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kesi hiyo inaendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Wakili PETER CAMILIUS, ambaye aliwasomea hoja za awali za mashtaka ya kuisababishia hasara Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ya kiasi cha shs. 51,792,615/- kati ya kipindi cha Oktoba 2, 2014 na Disemba 31, 2014.
Makosa haya yanadaiwa kutendeka wakati washtakiwa walipokuwa watumishi wa Halmashauri ya Ruangwa kwa nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa mshtakiwa wa kwanza na Mweka Hazina kwa mshtakiwa wa pili.
Washtakiwa wamekana mashitaka hayo na wameachiwa baada ya kukidhi masharti ya dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi Februari 7, 2023.