LGE2024 Lindi: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa wajiandikisha kwenye daftari la Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

LGE2024 Lindi: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa wajiandikisha kwenye daftari la Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo Oktoba 19, 2024, ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la Mpigakura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Akiwa ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa, alijiandikisha katika shule ya msingi Nandagala, wilayani Ruangwa, pamoja na baadhi ya wanakijiji wenzake.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ruangwa, Frank Chonya, alibainisha kuwa wilaya hiyo ina vijiji 90 na vitongoji 435, ikikadiria kuandikisha wapiga kura 123,803.

kasim.jpg

Soma pia: Lindi: Mbunge wa Mchinga, Salma Kikwete ajiandikisha kwenye daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Hadi kufikia tarehe 18 Oktoba, 2024, jumla ya watu 103,468 walikuwa wameshajiandikishwa, wakiwemo wanaume 47,664 na wanawake 55,804.
 
Jakaya kikwete kajiandikisha msoga
Mke wake kajiandikisha lindi
 
  • Kicheko
Reactions: apk
Hesabu ya uongo kwa maandalizi ya kuiba kura,hawa watu hata aibu hawaoni!
 
Majaliwa amekuwa Mbunge na bado kawa Waziri kwa miaka kumi Ila bado anataka kugombea. Harafu baadae atasema msiwachague wapinzani wanauroho wa madaraka. Kauli nyingine vijana mjiajiri.
 
Majaliwa amekuwa Mbunge na bado kawa Waziri kwa miaka kumi Ila bado anataka kugombea. Harafu baadae atasema msiwachague wapinzani wanauroho wa madaraka. Kauli nyingine vijana mjiajiri.
Hivi jamaa bado atagombea ubunge? Ili iweje sasa, aje kua waziri wa maji 😀
 
Back
Top Bottom