Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo Oktoba 19, 2024, ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la Mpigakura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Akiwa ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa, alijiandikisha katika shule ya msingi Nandagala, wilayani Ruangwa, pamoja na baadhi ya wanakijiji wenzake.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ruangwa, Frank Chonya, alibainisha kuwa wilaya hiyo ina vijiji 90 na vitongoji 435, ikikadiria kuandikisha wapiga kura 123,803.
Soma pia: Lindi: Mbunge wa Mchinga, Salma Kikwete ajiandikisha kwenye daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Hadi kufikia tarehe 18 Oktoba, 2024, jumla ya watu 103,468 walikuwa wameshajiandikishwa, wakiwemo wanaume 47,664 na wanawake 55,804.