Linganisha Delegation ya Botswana na ya Tanzania kwenye kuapishwa Rais Mteule wa Zambia

Mimi naona ni vizuri CCM wamekwenda kwa wingi kushuhudia mpinzani HH amechukua nchi kwa sababu tunajua karma is a .........it will happen in Tz one day
 
Wao CCM ndio waliokuna vichwa mpaka wakabuni na kufanikisha TOZO wacha wazifaidi, mchumia juani hulia kivulini. Sisi uchumi tulikwisha paa tuko matawi ya juu hauwezi ukatufananisha na wafuga ng'ombe, CCM MBELE KWA MBELE wacha wajue hii nchi ina wenyewe na wenyewe ni CCM.
 
Ni mwandishi wa Barua wetu mswahili tu kaipenda kujaza majina bila sababu. Halafu anaziba comments kwenye page, huyu Haniu mshezi kweli
We una akili au matope? Kosa la mwandishi nini kuripoti alicholetewa? Shame on you!
 
Wakuu inasikitisha Sana!

Imagine Rais Samia anaondoka na jopo lote Lile, cha kushangaza wote ni makada wa chama pendwa bila kuwa hata na chembe ya mchanganyiko wa kiongozi mmoja toka chama pinzani chochote kile!

Hii Ni aibu kubwa sana, na inatoa picha kwa mataifa ya nje kuwa Tanzania hawapendani, hawana mshikamano, wamejawa unafiki wakitangaza Kuna amani kumbe mioyoni mwao Hamna amani. Ni roho za korosho!

Viongozi wa Taifa hili, mjirekebishe, jifunzeni kwa mataifa mengine ambao wameambatana na viongozi wa Vyama pinzani, mathalani Botswana!

Kwani wamepungukiwa Nini? Wamekufa?

# Acheni ubinafsi

 
Lakini kwa kweli sasa tunaanza kuishiwa hoja.Ujumbe wa uwakikishi kila nchi inaamua kivyake na siyo swala la kuzua mjadala.Ndiyo maana tunasema huenda mpaka ikifika 2024 CHADEMA itabakiwa na makapi matupu maana yake hata mambo wanayoongea kwa sasa ukiwasikiliza unajiuiza hawa wako hai au wameshaondoka katika dunia hii siku nyingi.
 
Ni aibu sana Chama hatari na cha kipumbavu kama CCM kwenda kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais kwenye Taifa la kidemokrasia, CCM wanatakiwa kwenda Afghanistan au Mynmar kwa watu wanaofanana nao tabia
 
Unapeleka Makada?
Wenzetu Botswana kuna na KIONGOZI WA UPINZANI kwene msafara.
Lakini kwa Tanzania Kiongozi Upinzani yuko korokoroni na ana KESI YA UHAINI ya kutengexwa ili kummaliza Mbowe!!!!Hii nji ina LAANA YA CCM kwa kweeri!
 
Hapo Naona and Senior Government Officials

Sasa hao ni wangapi wanaweza wakawa wawili, au wanaweza wakawa 200.
Umenikumbusha AFCON 2019 Cairo, wakati Senegal wakiwabeba wachezaji wao Nguli wa soka kina Diof, Camara, Diop na wengine kuisindikiza timu yao ili kuipa hamasa na ushauri wa kisoka timu yao, TFF na kamati ya ushindi wakamchukua Pierre Liquid mtu asiyejua lolote kuhusu soka! Hiyo ndio delegation ya Rais na wazee wa Ndiyoo! #MbowesioGaidi
 
Tuna utawala wa hovyo kabisa kuwahi kutokea
 
Hivi huyu bibi uchaguzi ukiwa ni wa haki kabisa yaani tume huru ya uchaguzi hata mume wake kweli atampigia kura?
 
MKUU TULIPOFIKIA NI PABAYA SANA. Tanzania ya leo umimi, ubinafsi, ukanda na uvyama umetamalaki. Haikutegemewa kwa Tanzania kunaweza kuwa na magaidi, wasiojulikana n.k. Tuna muda wa kujirekebisha, TUJIREKEBISHE
 
Duh kumbe?
Ndiyo hivyo. Hata askari wa majeshi yetu ni government officials but they are not civil servants, they are millitary servants. Hata wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani ni government officials.
 
Ndiyo hivyo. Hata askari wa majeshi yetu ni government officials but they are not civil servants, they are millitary servants. Hata wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani ni government officials.
Hahahaa hahahahahaa hahahahahaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…