Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
๐๐ข๐ง๐ข ๐๐๐ง๐ข๐ฌ๐ ๐๐๐ญ๐จ๐ฅ๐ข๐ค๐ข ๐๐ข๐ญ๐๐๐๐ง๐ฒ๐ ๐๐ข๐ฌ๐ ๐๐๐ค๐๐ญ๐ข๐๐ฎ ๐๐ฎ๐ฐ๐๐จ๐ฆ๐๐๐ ๐ง๐ ๐๐ฎ๐ฐ๐๐ค๐ฎ๐ฆ๐๐ฎ๐ค๐ ๐๐๐ญ๐ฎ ๐๐๐ฐ๐ ๐๐๐ฅ๐ข๐จ๐ญ๐๐ฌ๐ฐ๐ ๐ง๐ ๐๐ฎ๐ฎ๐๐ฐ๐?
Kanisa Katoliki limekuwa na nafasi kubwa katika historia ya dunia.
Limejenga shule, hospitali na taasisi nyingi za huduma. Hata hivyo, historia hiyohiyo inabeba dhulumua kubwa, ambapo mamilioni ya watu waliteswa, waliuzwa au waliuawa kwa jina la Kanisa au kwa baraka zake.
Swali ni hili, ni lini Kanisa litaadhimisha Misa Takatifu maalumu kwa ajili yao?
Haya nayo yanahitaji Misa takatifu kama lile la Oktoba 29:
1. Watumwa Weusi 272 waliouzwa na Ushirika wa Wajesuiti wa Maryland, Marekani, mwaka 1838 ili kuokoa Chuo Kikuu cha Georgetown.
2. Mamilioni ya Waafrika waliochukuliwa utumwani baada ya matamko ya Papa ya Dum Diversas (1452) na Romanus Pontifex (1455), yaliyoruhusu watu wasio Wakristo kufanywa watumwa wa kudumu.
3. Watu asilia wa Amerika waliouawa, kunyang'anywa ardhi na kulazimishwa kubadili dini wakati wa ukoloni uliohalalishwa na "Doctrine of Discovery."
4. Watoto wa shule za bweni nchini Kanada, ambao wengi wao walikufa mbali na familia zao na kuzikwa katika makaburi yasiyo na alama kwenye ardhi ya Kanisa Katoliki.
6. Wayahudi, Waislamu na Wakristo wa Mashariki waliouawa wakati wa Vita vya Msalaba, pamoja na Wayahudi waliofukuzwa na kuteswa barani Ulaya kwa karne nyingi.
7. Waliohukumiwa na Mahakama za Kidini (Inquisition), walioteswa na kuchomwa moto kwa tuhuma za uzushi.
8. Wanawake waliotuhumiwa kuwa wachawi, waliouawa katika kesi ambazo Kanisa lilishiriki.
9. Wanawake na watoto wa Nyumba za Magdalene na nyumba za mama na mtoto nchini Ireland. Kwa mfano, katika nyumba ya Tuam peke yake, mabaki ya watoto karibu 800 yalizikwa bila heshima.
10. Wahanga wa unyanyasaji wa kingono na mapadre kwa watoto pale Vatican, ambao maisha yao yaliharibiwa huku viongozi wakificha ukweli.