EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Siku moja maza kaja kunitembelea kwangu, nikamtoa out tukala nyama akafurahi sana akaniambia Einstein mdogo wako wa mwisho siku moja aliniuliza "mama nlishawahi kukuambia NAKUPENDA?"
Akasema sikutaka kumkatisha tamaa nikamwambia umeshawahi mwanangu.
Dogo akasema "Mama NAKUPENDA"
Maza akasema machozi yalitoka mbele yake.
Wakati ananisimulia nikatafakari mimi mbona sikumbuki lini nilimtamkia neno hilo hata kwenye meseji?
Baada ya mwezi akafariki bila mimi kumtamkia NAKUPENDA MAMA hili deni linaniuma sana. Jana nimesafiri kutoka mkoani kuja Dar kumjulia hali baba ambaye yupo wodini anapigania maisha yake.
Nataka nikamwambie "BABA NAKUPENDA"before its too late.
Nauliza nyinyi hasa watoto wakiume lini umemwambia mzazi wako NAKUPENDA??
Wadada sometimes mnawezaga.
Muwe na jumapili njema watu wa Mungu.