Lini mara ya mwisho kumtamkia mzazi/mlezi wako nakupenda?

Aii katika kumbukumbu zangu sijawahi tu ... labda wale wa mboga 7 ila sisi mboga 1 siku2 aah hata huo mda hakunaga.. muda wote mchaka mchaka
Dada hadi wewe !![emoji849][emoji849]
 
Daaa Mkuu, umeongea mada nzuri sana. Nafikiri lifestyle ya malezi yetu waafrica ndio inapelekea ugumu wa kuwaambia wazazi Nakupenda. Wenzetu ulaya wamefanikiwa sana kwenye lifestyle ya malezi inayoweka urahisi wa mtoto kumwambia mzazi nakupenda.

Lakini mada yako imetufikilisha jambo kubwa la kujifunza, kuanzia ngazi ya familia hasa mzazi na mtoto, kuwe na lifestyle inayojenga urafiki kati yao. Hii italeta urahisi wa kuambiana nakupenda mama/baba/mwanangu
 
[emoji1756][emoji1756][emoji1756][emoji1756][emoji1756] tujifunze ku-apreciate nguvu zao kwetu.

Tumetoka kimaisha kwasababu walijinyima
 
[emoji1756][emoji1756][emoji1756][emoji1756][emoji1756] tujifunze ku-apreciate nguvu zao kwetu.

Tumetoka kimaisha kwasababu walijinyima
Ni kweli, lakini swala la kumwambia mzazi nakupenda ni mjadala ulioegemea lifestyle ya malezi. Mzazi mwengine hasa wa kiume ukimuambia nakupenda tena wewe ni mtoto wa kiume, anapata wasiwasi na uwanaume wako.

Kwanini ? Ni kwa sababu hakukulea katika mazingira hayo. So lifestyle ya malezi ya mzazi ndio kitengeneza urafiki kati ya mzazi na mtoto.
 
[emoji851][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jana nkamwangalia mshua nikawaza weee, nikamkaushia[emoji851][emoji851][emoji851][emoji851]
 
Nini wazazi mi mke wangu tu sijawahi mwambia kwa mdomo kwamba nampenda. Huwa sinaga ungese huo sijui valentine day sijuhi utopolo gani.

Mi huwa sinaga shobo hizo, mi ni matendo tu ndio yanaonesha hizia zangu. Mi ninaamini katika matendo kuliko maneno na taarabu.
 
[emoji1316][emoji1316][emoji1316][emoji1316][emoji1316] we jamaa ni bonge la fala hata mkeo????
 
Aya maneno tuwaachie wazungu huko
Huku kwetu ishara ya kuonesha unampenda mzazi wako ni matendo tu mema kwake
Yani ni mwambie mzee et "Nakupenda" Asee kwanza atanipiga ilo jicho atajua hapa sina kijana wa kiume[emoji23][emoji23]
 
Aya maneno tuwaachie wazungu huko
Huku kwetu ishara ya kuonesha unampenda mzazi wako ni matendo tu mema kwake
Yani ni mwambie mzee et "Nakupenda" Asee kwanza atanipiga ilo jicho atajua hapa sina kijana wa kiume[emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sio lazima utamke baba nakupenda, kuwafanyia tu matendo ya upendo ni ishara tosha kwamba unawapenda.
Ni kweli sio lazima ila maneno yana nguvu sana. Huwa naona nuru kwenye uso wa bimkubwa na changamko la sauti yake nikimwambia "nakupenda sana bi mkubwa." Jaribu one time utaona.
 
Pole mkuu. Si utamaduni tuliouzoea ila ni mzuri na unavitalize mahusiano tulonayo na wazazi wetu. Mungu amsaidie mzee apone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…