KERO Lini Serikali itaondoa changamoto ya kivuko Ferry?

KERO Lini Serikali itaondoa changamoto ya kivuko Ferry?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hapo Magogoni palitakiwa kujengwa daraja refu ambalo lingeruhusu meli kubwa kupita chini.

Daraja hili lilihitajika zaidi ya daraja la Tanzanite au lile la Nyerere.

Ila, nchi yetu ina tabia ya kuwa na vipaumbele vibaya.
Mradi wa watu ule hawako tayari kuupoteza.
 
Habari za mchana.

Je, serikali imejipanga vipi na ina mpango upi wa muda mrefu kwa wakazi wa Kigamboni ambao wakuwa wakipata hadha ya kuhangaika na usafiri wa kivuko Ferry takribani mwezi mmoja sasa, kivuko kinachofanya kazi ni kimoja tu MV kazi.

Ambacho kuvuka upande mmoja kwenda mwingine kinatumia takribani lisaa limoja na zaidi.

Hali ambayo inapelekea kuchelewesha shughuli za kila siku za uzalishaji mali kwa wakazi wa Kigamboni wanaofanya shughuli zao mjini.

Nikiwa kama mwananchi wa kawaida ninaomba serikali itupe jibu imejiandaaje na ina mpango gani na shughuli za uvukaji Kigamboni A.

Ahsante.
Serikali haiombwi na raia bali serikali inaamrishwa. Endeleeni kuomba basi muone itachukuwa muda gani? Waache kustarehe na kununua magari ya anasa, watumie hizo fedha kununulia raia kivuko?
 
Mbona bei rahisi sana? Sikuwahi kufikiri kitu kama hicho
Umeona mkuu haya ulizia sasa kama unaweza kuweka hapo uone mziki wake
Ila kinawezekana ingawa wabongo utakavyo zungushwa ofisi hadi ofisi
 
Ukiamua kutumia daraja badala ya pantoni unaongeza 5 au 6km mpakq Posta. Umbali huo na muda unaookoa hapo feri ni afadhali mara 1000!
Nilishaachana na kupita feri, hapo ni jambo la muda tu pantoni itazama na watu.
Yeah, lakini unaongelea ulimwengu ambao feri hakuna daraja.

Feri kungekuwa na daraja, usingeongeza hizo km 5 au 6, ambazo ukizizidisha kwa idadi ya maelfu ya watu zinakuwa nyingi sana.

Tanzania inapoteza muda, uzalishaji, nishati kwa kiasi kikubwa sana kwa watu wanaoenda mjini kuongeza km 5 au 6 kupitia kwenye daraja.

Kwa sababu daraja limejengwa sehemu ya kuzunguka.
 
Kabla ya daraja hapo feri unaweza kukaa 2-4hrs uvuke. Baada ya daraja feri tulikuwa tunavuka less than 45mins peak hours(pantoni tatu zinafanya kazi effectively).
Then pantoni zimeanza kufa moja moja and nobody cares matokeo yake ndio haya.
Hio delay ya feri ni sababu ya pantoni lufa huku uongozi unakenua meno tu.
Pantoni tatu zikirudi kazini hata mimi darajani sipiti. Daraja lilikuwa second option lakini sasa hivi ndio 'only' option.
Kuokoa 2-3 hrs kwa kuendesha extra 5km will do anytime.
 
Serikali haiombwi na raia bali serikali inaamrishwa. Endeleeni kuomba basi muone itachukuwa muda gani? Waache kustarehe na kununua magari ya anasa, watumie hizo fedha kununulia raia kivuko?
Tanzania hii uiamrishe serikali? Utaambiwa wewe ni mkimbizi muda si mrefu
 
Kabla ya daraja hapo feri unaweza kukaa 2-4hrs uvuke. Baada ya daraja feri tulikuwa tunavuka less than 45mins peak hours(pantoni tatu zinafanya kazi effectively).
Then pantoni zimeanza kufa moja moja and nobody cares matokeo yake ndio haya.
Hio delay ya feri ni sababu ya pantoni lufa huku uongozi unakenua meno tu.
Pantoni tatu zikirudi kazini hata mimi darajani sipiti. Daraja lilikuwa second option lakini sasa hivi ndio 'only' option.
Kuokoa 2-3 hrs kwa kuendesha extra 5km will do anytime.
Sikulaumu kwa kutumia daraja la sasa.

Nakuambia daraja la ferry lingesolve tatizo habari zote za pantoni kupanda kushuka zisingekuwapo.
 
Kwani kwenye madaraka wapo kufanya nini kama siyo kutekeleza wanayotakiwa kufanya na wananchi?
Nchi ilinayokubali kuitwa daraja la tatu ni nchi ya daraja la tatu tu!
Taifa likitaka kuitwa taifa tukufu ni lazima litumie fursa ya kukataa aina yoyote ya sera ambayo ni kinyume na utu wa binadamu! Ikiwa hutaikataa serikali mbovu, malalamiko yataendelea kuwepo na kuwepo.
 
Sikulaumu kwa kutumia daraja la sasa.

Nakuambia daraja la ferry lingesolve tatizo habari zote za pantoni kupanda kushuka zisingekuwapo.
Hata hili huku limesaidia sana. Kuna trucks zilikuwa zinazunguka Kongowe over 50km round sasa hivi wanasafiri 5km wako bandarini au kwemye yard zao kigamboni. Sodhani kama daraja la feri lingepitisha hizi trucks. Maana hizo trucks zingejaa hapo city centre sijui ingekuwaje?Halafu daraja la ferry lingeanzia na lingeshukia wapi?Maanake inabidi liwe juu kiasi cha kupitisha meli chini au la kufunga na kufungua kuruhusu meli. Daraja lilipo sasa hivi linasaidia watu wa kawaida na biashara maana liko karibu na bandarini kabisa. Anyway wakazi wa kigamboni wanajua kero ambazo daraja limetatua.
 
Sisemi kwamba daraja la sasa halitatui kero yoyote, na pengine tunalihitaji pia, lakini pia, hapo ferry panahitaji daraja.

Kuhusu pa kuanzia, kama wameweza kujenga Tanzanite Bridge kutoka huku Aga Khan mpaka huko Oysterbay Beach, basi kuna jinsi ya kulipandisha daraja juu liruhusu meli zipite chini, kuanzia hata Mikadi Beach huku kuliunganisha kwenda kukutana na Barack Obama Drive hapo.

Kuna technical difficulties za mkondo wa meli ulio deep hapo, lakini sifikiri kama ni sehemu ndefu sana na with the right budget wangeweza kujenga.

Tatizo ni nia, labda na bajeti tu. Na hiyo bajeti kukiwa na nia inapatikana tu, tatizo kibwa ni nia tu.
 
Hii seemu kama hakuna Mbunge kabisa yaaan au sijui kajikatia tamaa. Wakazi wa Kigamboni ndio watumiaji wakubwa Kwa stendi ile iliyokua pale ferry ingawa ni jimbo jingine lkn imeondolewa shida wanaopata ni wakazi wa Kigamboni maana wakivuka wanajikuta wanatembea mpk Ohio kule.
Kati ya wavunge wanaofanya vizuri zaidi hapa mjini. Wa kigamboni ni mmoja wao. Changamoto iko kwa serikali.

Mfumo wa uendeshaji wa vivuko hauko efficient. Tamesa wameshindwa kabisa kama walivyoshindwa DART kwenye mwendo kasi au tanesco kwenye umeme.

Serikali haiwezi kufanya biashara, huo ndo ukweli. Msimamo wa mmbunge wa kigamboni akiwa bungeni na akiwa mtaani ni kwamba vivuko vipewe sector binafsi iviendeshe kwa ufanisj.

Serikali imegoma kabisa kupokea hii hoja
 
Back
Top Bottom