dr shayo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2014
- 555
- 980
Kwa kweli tupo nyuma sana. Kama mimi nilifanya kazi na mtu wa nje huko akaniambia anilipe kwa njia gani, ikabidi nimuambie atumie money gram hamna namna.
Dunia ni kama kijiji siku hizi, kila kitu waweza kukipata kwa simu yako kiganjani mwako kwa internet.
Cha muhimu zaidi kwenye internet ni kuitumia ijenge uchumi wako, internet imewezesha mfanyabiashara wa australia aweze kupokea pesa kwa mteja wake wa marekani kwa njia rahisi zaidi ya paypal.
Kwa Tanzania tumekuwa na uwezo wa kufanya malipo pekee kwa mfumo wa paypal bila kuruhusiwa kupokea pesa, Watu hufanya manunuzi kwenye mitandao kama alibaba, ebay, amazon, fiverr, hostgator, itunes, n.k laikini llinapokuja suala la kupokea pesa inakua haiwezekani, kitu ambacho kinafanya hata uchumi wetu udhoofike kwa kuifanya inchi iwe na imports nyingi kuliko exports.
Wenzetu hapo mpakani Kenya wameshatimiza hili zamani, kwa sasa kuna wafanya biashara hasa wale wanaotoa huduma wanaweza kufanya kazi na wateja wao wa marekani, uingereza, ufaransa, n.k na kupokea fedha kwa njia ya paypal.
Kwa hapa Tanzania hiki kitu kimepigiwa kelele sana pasipo kua na dalili yoyte ya utekelezaji, Kinachobakia watu wanatumia internet kucheki youtube, kufatilia umbea instagram, kuchati whatsapp na kutafuta wachumba facebook na badoo.
Tunakwama wapi katika kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda, Kuwepo kwa paypal Tanzania ni kuleta uchochezi wa kupanua viwanda kwasababu soko litavuka hadi mipaka.
Tutafakari, Dunia ni kama kijiji sikuhizi