Lini Tanzania itaruhusu matumizi ya Paypal?

Lini Tanzania itaruhusu matumizi ya Paypal?

Kwa kweli tupo nyuma sana. Kama mimi nilifanya kazi na mtu wa nje huko akaniambia anilipe kwa njia gani, ikabidi nimuambie atumie money gram hamna namna.
Dunia ni kama kijiji siku hizi, kila kitu waweza kukipata kwa simu yako kiganjani mwako kwa internet.

Cha muhimu zaidi kwenye internet ni kuitumia ijenge uchumi wako, internet imewezesha mfanyabiashara wa australia aweze kupokea pesa kwa mteja wake wa marekani kwa njia rahisi zaidi ya paypal.

Kwa Tanzania tumekuwa na uwezo wa kufanya malipo pekee kwa mfumo wa paypal bila kuruhusiwa kupokea pesa, Watu hufanya manunuzi kwenye mitandao kama alibaba, ebay, amazon, fiverr, hostgator, itunes, n.k laikini llinapokuja suala la kupokea pesa inakua haiwezekani, kitu ambacho kinafanya hata uchumi wetu udhoofike kwa kuifanya inchi iwe na imports nyingi kuliko exports.

Wenzetu hapo mpakani Kenya wameshatimiza hili zamani, kwa sasa kuna wafanya biashara hasa wale wanaotoa huduma wanaweza kufanya kazi na wateja wao wa marekani, uingereza, ufaransa, n.k na kupokea fedha kwa njia ya paypal.

Kwa hapa Tanzania hiki kitu kimepigiwa kelele sana pasipo kua na dalili yoyte ya utekelezaji, Kinachobakia watu wanatumia internet kucheki youtube, kufatilia umbea instagram, kuchati whatsapp na kutafuta wachumba facebook na badoo.

Tunakwama wapi katika kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda, Kuwepo kwa paypal Tanzania ni kuleta uchochezi wa kupanua viwanda kwasababu soko litavuka hadi mipaka.

Tutafakari, Dunia ni kama kijiji sikuhizi
 
Kwan hiz benki za hapa nchin hazilioni hili
Yaaan hata nashindwa kujua ugum uko wap
Labda watuambie ili tujue..
 
Inaruhusu kwa sasa mkuu, pay pal wameungana na CRDB Bank so unaweza kutoa pesa yako na kwenda bank kuchukua, wanacharge $2.3 kwa transaction ya mpaka $5000
 
Habari wanajamvi.
Binafsi naifahamu njia ya malipo ya online ijulikanayo kama PAYPAL inatumika katika kulipia na kupokea malipo kutoka nje ya nchi.
Sintofahamu imekuja wakati nimefanya kazi ya mtu Online na alikuwa anataka kunilipa kwa PAYPAL lkn ikashindikana.
Maswali yangu ni Je hii njia haifanyi kazi hapa nchini?je ni njia gani Naweza kutumia niipate hii ela?au kuna jinsi naweza kufanya ni enable PAYPAL?
 
Pole mkuu Kuna tatizo kwa watendaji kazi online ziko kibao shida inakuja namba ya ku kukulipa wengi watoa kazi online hutaka kukulipa kwa PayPal ukifanya kaxi.Huku kwetu unakuta hakuna na wao kule wanasema to hell with you.Serikali ibadilike kwenye hili.Hata Bidhaa zetu tungeweza ziweka online tunauza online na kulipwa kwa PayPal Kisha unazipeleka .Mtu anachagua Bidhaa online kiwe kinyago,nk ananunua kwa KU click tu pesa inaingia unampelekea mzigo wake
 
Mkuu tufanye nini ili kuaddress ili suala kwa wahusika na kuhakikisha limefika sehemu sahihi tunayoweza kupata majibu?
 
chanzo cha taarifa?
Inaruhusu kwa sasa mkuu, pay pal wameungana na CRDB Bank so unaweza kutoa pesa yako na kwenda bank kuchukua, wanacharge $2.3 kwa transaction ya mpaka $5000
 
aina gani ya account umefungua?
Inaruhusu kwa sasa mkuu, pay pal wameungana na CRDB Bank so unaweza kutoa pesa yako na kwenda bank kuchukua, wanacharge $2.3 kwa transaction ya mpaka $5000
 
Back
Top Bottom