Lini tutakuwa Nchi moja, Serikali Moja? Jamhuri ya Tanzania isiwepo kabisa ile Muungano

HII sasa ni hamisha mawazo ya uchaguzi mkuu uliopita na matokeo ya ajabu,mada za kuuchokonoa muungano zaanzishwa mawazo yaelekezwe huko mbilinge za matokeo ya uchaguzi mkuu zisahaulishwe
 
tupo tunawatizama TU
WE ARE FOLLOWING THE DEVELOPMENT WITH GREAT CONCERN
THEY APPROCHING THE RED LINE

AFRO SHIRAZ PART
😂😂😂
Sasa hilo shoka ndo utalitumiaje mkuu?🙄
 
Ndo mmetumwa huko mje muanzishe mada za aina hii Mimi mtanganyika ila shiitaki muungano waachieni wenyewe wazanzibar nchi yao na kamwe haitatokea kuwa nchi moja
 
😂😂😂
Sasa hilo shoka ndo utalitumiaje mkuu?🙄
WAPELEKE MSWAADA BUNGENI WA KUFUTA SMZ SI WANA 2/3
ILI KUWE NA SEREKALI MOJA
hahahahahahahahaahhaha🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
YA TANGANYIKA
kuna baadhi ya wadanganyika wana mawazoo yakipuuzi kweli
baada kushuhulika na kuunganisha wilaya kwa barabara za lami na umeme vijijini wao wanawaza zanzibar kuwa mkoaa
 
Ulitaka kusikia kauli wa wazanzibari?. Umechelewa. Mzanzibari atakae jitambulisha kama mtanzania ni wakuja. Mwenye asili ya zanzibar huwezi kusikia ana jitambulisha kama mtanzania. Na parapanda limekwisha pigwa. Muulizeni Kabudi Palamagamba. Asiwafiche. Anajuwa kinacho endelea.
 
Bunge la February? Mkuu kama jambo limetamkwa kwenye katiba haliondolewi kizembe hivyo!

Huanza kura ya maoni nchi nzima juu ya mbadiliko ya katiba, then katiba iliyopo ibadilishwe kwanza..n.k n.k ni mchakato mrefu
 
Kwani hapo awali zenji ilikua wapi na ilikua inatambulika kama nchi au kijisehemu tu?
 
Acheni kulazimisha watu kitu wasichokitaka. Mnaona huo muungano ni wa maana sana, acheni watu waishi watakavyo na sio mtakavyo. Hilo bunge halijachaguliwa na wananchi bali vyombo vya dola, litapata wapi uhalali wa kuwapangia watu aina ya muungano?
 
Mshindwe na mlegee, Zanzibar itabaki kuwa Zanzibar. Na hamtaweza kuimeza abadan kwa uwezo wa muumba mbingu na ardhi!
 
Kama unavyoona zinatumika mbinu na hila tofauti kuitawala Zanzibar ndivyo dalili zinaonesha wazi Wazanzibar wamechoka na mwisho unakaribia.
Ilo la kuifanya Zanzibar mkoa halitowahi kutokea sababu ndilo litakalo iweka huru zaidi ya vile wewe unadhani. Vuta picha kipindi cha mihadhara ya uamsho Wazanzibar waliacha tofauti zao wakawa wamoja na usizani wamesahau. Mfano mwengine angalia utawala wa Amani Jr. siku za mwisho alipobadili katiba ya Zanzibar walisahau uccm na ucuf wakabadili katiba kuijengea mazingira ya ulinzi zanzibar na usidhani yalifanyika kwa bahati mbaya.
 
Nchi iwe na serikali moja, hata kura zikipingwa Tanganyika ni wengi tutashinda hivyo namimi napendekeza serikali moja ili kuondoa ubaguzi na kuleta mshikamano kwa vizazi vinavyokuja.
 
Nchi iwe na serikali moja, hata kura zikipingwa Tanganyika ni wengi tutashinda hivyo namimi napendekeza serikali moja ili kuondoa ubaguzi na kuleta mshikamano kwa vizazi vinavyokuja.
Ndugu kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar mabadiliko km hayo lazima waamue wenyewe. Katiba inataka kama wazanzibar wapige kura ya maoni kuamua hivyo hata kama bara wataamua kwa upande wao basi ni bure tu
 
Reactions: lum
Nchi iwe na serikali moja, hata kura zikipingwa Tanganyika ni wengi tutashinda hivyo namimi napendekeza serikali moja ili kuondoa ubaguzi na kuleta mshikamano kwa vizazi vinavyokuja.
hhahahaah yaani kweli kuna ndoto za jinamizi. Inaonyesha ndugu yangu umekula muho ukavimbiwa sasa usiku una ndoto za maajabu. Dunia imegeuka hii . Munatengwa na kila mtu sasa. Hata majirani wanaogopa kuwa rafiki wa TZ. Bado tu hamuja fahamu.
 
Yani tunahangaika kuwa na serikali tatu wewe unaongelea serikali noja as if Zanzibar na Tanganyika ni nchi moja??

The fact kwamba tunaongea wote kiswahili na tuna maingiliano ya kijamii bado haifanyi Zanzibar kuwa nchi moja na Tanganyika.

Ili huu Muungano uwe na tija, lazima iwepo SMZ, Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika then iwepo JMT. Mengineyo sasa kuhusu muundo na utendaji wa JMT ndio yanajafilika kwenye Memorandum.

Ukiongelea Serikali moja hapo ndio utafanya hata maongezi yasiwepo.
 
uko sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…