Lini viwanja vitakarabitiwa angalau sehemu ya pitch

Lini viwanja vitakarabitiwa angalau sehemu ya pitch

ryan riz

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
423
Reaction score
683
Jaman ligi yetu kama mnavyoiona kila siku inazidi kukua.

Pili kwa macho ya mbali ndio inaweza kuja kuwa ligi ya tatu kwa ukubwa hasa kwa kuwavutia wachezaji wa kigeni tokana na kaliba au asili ya watanzania kuwa waungwana na wakarimu kwa wageni bila ubaguzi,hichi ambacho wachezaji wengi wa kigeni hukikosa kwa mataifa mengine ya kiafrika

Tatu azam Tv anaweza ipaisha hii ligi kuwa kivutio kwa kuanzia afrika mashariki,afrika ya kati mpaka kusini iwapo tu kukiwa na miundo mizuri ya viwanja hivyo ligi ikavutia kuangaliwa na kibiashara pia na hata serikali kujitangaza.

Au nyie ndugu zangu mnalionaje hili..?
 
Kuna Misri, Morocco, Tunisia, Afrika kusini Kwa uchache nani kakudanganya ligi yetu ya tatu
 
Sisi watanzania tumejifungia ndani ya Box na kujisifu wenyewe. Ligi yetu ni mbovu kuliko ligi nyingi za Afrika.
Hii inakuonyesha Rank ya Tanzania duniani na Afrika ni mbovu.
Ligi haizalishi wachezaji wanaoweza kushindana nje ya chi.
 
Sisi watanzania tumejifungia ndani ya Box na kujisifu wenyewe. Ligi yetu ni mbovu kuliko ligi nyingi za Afrika.
Hii inakuonyesha Rank ya Tanzania duniani na Afrika ni mbovu.
Ligi haizalishi wachezaji wanao weza kushindana nje yanchi.
Kiongozi hayo yote yanaweza kufanikiwa ikiwa tu miundo mbinu ikiwa mizuri..kiongoz kwa afrika Tanzania inayonafasi nzuri sn kuwa na ligi bora..
Afrika magharibi asilimia 90% ya wachezaji wazur hukimbilia ligi za ulaya coz wanao msingi tayari hii tokana na kutengenezewa njia na babu na baba zao..

Afrika ya kusini japo ni weusi wenzetu na wanauchumi mkubwa ila wabaguzi na roho mbaya kwa wageni.

Ukija kwa wenzetu wa kaskazi( waarabu) wao hawatoki sana nje ya mataifa yao japo wanao uwezo wa kucheza ligi za ulaya coz wamekamilika kimiundo mbinu na pia uchumi uko imara.Ila kwa wachezaji weusi kule kwa waarabu hufuata malipo mazur ila wengi wao hawafurahii maisha ya kule tokana na asili na tabia za wenyeji kwa wageni hasa weusi.

Ukija Tanzania kwa asili yetu na Tabia zetu za uungwana kwa wageni wote..ikitokea tu serikali ikaboresha miundo mbinu na vilabu vikapata udhamini mizuri,braza hii ligi itakuja kubwa sana na kimbilio la wachezaji wa kigeni wa africa.
Hii itapelekea vilabu kuimarika na pia hata wazawa kuwa kwenye ubora sahihi tokana na ushindani mkubwa.
 
Comperative Advantage ipo upande wa ligi yetu. Kama ulivo sema ligi yetu ina potentials za kuja kuwa miongoni mwa ligi 5 bora Africa. Viwanja na marefa ndizo changamoto kubwa. Sidhani kama kuna ligi Sub-Saharan Afica inayo zungumzwa zaidi na mashabiki wake kama ligi yetu.
 
Serikali inatakiwa katika sera zake za michezo itoe ruzuku Ili kuwezesha uwepo wa viwanja Bora, makocha wazawa Bora, kuwepo na vituo Bora vya michezo vya Serikali kwakua michezo ni Ajira.
Mashindano ya kutosha ya vijana wenye rika mbalimbali tutafika mbali.
Ki uhalisia Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda sera zao za michezo ni Bora kuliko zetu ndio maana Wana wachezaji wengi wanao cheza nje ikihusisha michezo mbalimbali.
 
Back
Top Bottom