kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Tangu nchi ipate Uhuru Haakuna Ilani ya Uchanguzi ya chama cha siasa isiyokuwa na agenda kusabambasa maji, zahanati, pembejeo, masoko, ajira kwa wananchi, lakini baada ya uchaguzi kumalizika na mshindi kutangazwa hakuna ahadi iliyotekelezwa.
Uchaguzi ukija wanarudia yaleyale tena mpaka miaka 60 sana wananchi wamegawanyika kati ya wenye maji na wasio na maji, wenye umeme na wasiokuwa na umeme, wanaopata huduma ya za afya karibu na wanaofuata huduma za afya mbali sana, wenye barabara za lami na wasiokuwa na barabara hata za vumbi, wenye shule na wasiokuwa na shule karibu.
Mbaya zaidi yale maeneo ambayo wanasiasa hawakupeleka maji, umeme, hospitali, shule, vituo vya polisi, barabara nzuri, masoko, pembejeo, nk ndiko ambako wanasiasa wanapita bila kupingwa na wanashinda uchaguzi kwa kishindo kiliko kule ambako angalau kuna nafuu wa upatikanaji na huduma hizo. Hili ni laana au ni nini?
Kwanini Wananchi hawahoji ahadi za wanasiasa kwao? Au wananchi wanahoji lakini wanasiasa hawategemei kura zao ili kuchaguliwa tena na tena?