Lini Watanzania tutaamka na kusema IMETOSHA?

Lini Watanzania tutaamka na kusema IMETOSHA?

Wabongo huwa nashangaa tupoje maneno buku vitendo sifuri, wenzetu kenya nawaappreciate sana.
Tutaishia kulalama nyuma ya keyboard...
 
Ukiniuliza kama Tanzania ina kiongozi, nitajibu kuwa ina rais lakini si kiongozi. Ukiuliza kama Tanzania ina sera, nitakujibu kuwa ipo sera ya uchawa. Ukiuliza, kiuchumi Tanzania inaongozwa na nini, nitakujibu kuwa sera yake ni ya shamba la bibi ambapo wezi huja na kugema watakavyo. Ukiuliza kama Tanzania ni salama, nitakushauri ufanye utafiti na kuassess utakeji na kuporomoka kwa majengo. Ukiuiza kama Tanzania ina future, nitakujibu kuwa hata past haina. Kama mwanafalsafa, nawaza tu.
Ukiuliza kama serikali inakusanya kodi na kuzitumia vizuri, nitakujibu kuwa inawakamua maskini na kuwapa matajiri wakwepa kodi na wapiga dili wanaoshirikiana na wanasiasa mafisi. Ukiniuliza kama Tanzania ni kisiwa cha amani, nitakujibu kuwa ni kisiwa cha vurugu kinachongoja kulipuka. Kwa wananchi wanavyoteseka huku watawala wakitanua, Tanzania inaweza kuzidiwa na hata Somalia. Je ni lini watanzania wataamka na kusema katu kuwa inatosha?
Umeandika ujinga tupu
 
Mliletewa JPM mkaharahara hapa.

Tulieni kama "Ametosha"
Hata yeye hakufikia matarajio halisi. Alipwaya pakubwa kwenye demokrasia na uchumi wa sekta binafsi. Aliwapania kupitiliza sekta binafsi. Alisaidia nidhamu kazini japo ya woga. Ndiyo maana alipoondoka dharau na kiburi maofisini imerudi kuwa mbaya mara mbili ya wkt wa Kikwete. Aliibua miradi mikubwa iliyokuwa imekwama kama Bwawa la umeme na SGR.
 
Huoni ujinga ujinga wa watz
  • Kwamba haijawahi kutokea Watanzania wamesema sasa basi?
  • Kwamba Watanzania wanadekeza misaada?
  • Kwamba haijawahigi kutokea katika historia ya Watanzania waliosema 'hatutaki misaada' 'hatupendi rushwa' 'tunataka democracy'
Yaani unataka kutuaminisha , hajawahi kutokea mtu aliyechukizwa na Rushwa, ama hata ukandamizqji wa haki?
Ujinga gani huo wa watz. Toa maelezo kidogo
 
One man show...
Angekuwa wa maana angeingia madarakani na kuanza kuweka mifumo imara ya uongozi wa nchi. Naye alikuwa wa hovyo tu.
Ww unajizima akili tyu.
Kwa hiyo mbadala ni nani haswa Fuso?

Mifumo imara ipi, mbona hamueleweki na nn hasa mnachokitaka?

Ukiondoa jazba na biases zako ama za kukariri, unaeza ona unachokisema hakina mantiki yeyote ile. Ijs
 
Ungenifahamu humu ungejua maana yangu

Sasa si Rais mwanamke wengi walifurahia humu aliposhika uongozi huu

Nami nawasapoti kwa sanaaa

Nami nafurahia Mwanamke wenzangu anaweza sanaaaa
Sii mbaya ukanitafunia ulikuwa na maana gani kama nilikosea🙏
Enewei
hata mie nilifurahi sana, Mamaangu alinihadithia alifika Beijing na akanielezea umuhimu wa kuwasapoti wanawake pamoja na thamani za wanawake kwenye Siasa na Jamii, hivyo basi sina baya nayye
 
Ukiniuliza kama Tanzania ina kiongozi, nitajibu kuwa ina rais lakini si kiongozi. Ukiuliza kama Tanzania ina sera, nitakujibu kuwa ipo sera ya uchawa. Ukiuliza, kiuchumi Tanzania inaongozwa na nini, nitakujibu kuwa sera yake ni ya shamba la bibi ambapo wezi huja na kugema watakavyo.

Ukiuliza kama Tanzania ni salama, nitakushauri ufanye utafiti na kuassess utekaji na kuporomoka kwa majengo. Ukiuiza kama Tanzania ina future, nitakujibu kuwa hata past haina. Kama mwanafalsafa, nawaza tu.

Ukiuliza kama serikali inakusanya kodi na kuzitumia vizuri, nitakujibu kuwa inawakamua maskini na kuwapa matajiri wakwepa kodi na wapiga dili wanaoshirikiana na wanasiasa mafisi. Ukiniuliza kama Tanzania ni kisiwa cha amani, nitakujibu kuwa ni kisiwa cha vurugu kinachongoja kulipuka.

Kwa wananchi wanavyoteseka huku watawala wakitanua, Tanzania inaweza kuzidiwa na hata Somalia. Je ni lini watanzania wataamka na kusema katu kuwa inatosha?
Nyerere alikosea kugawa uongozi kwa kila mtu ni kosa, sio kila watu wana vision ya maendeleo. Unampa mtu asiyejua biashara hata ya kuuza mchicha wizara ya biashara unafikiri nini? Eti bi Kijazi waziri wa viwanda na biashara unategemea nini?
 
Nyerere alikosea kugawa uongozi kwa kila mtu ni kosa, sio kila watu wana vision ya maendeleo. Unampa mtu asiyejua biashara hata ya kuuza mchicha wizara ya biashara unafikiri nini? Eti bi Kijazi waziri wa viwanda na biashara unategemea nini?
Nyerere keshakosea na kuishia. Je sisi kwanini tunaendelea na makosa hayo hayo?
 
Nyerere alikosea kugawa uongozi kwa kila mtu ni kosa, sio kila watu wana vision ya maendeleo. Unampa mtu asiyejua biashara hata ya kuuza mchicha wizara ya biashara unafikiri nini? Eti bi Kijazi waziri wa viwanda na biashara unategemea nini?
Where is your substance?

Nyerere has been dead for so long, unataka kumbebesha maovu yanayotokea leo hii 2025? How?

Eniwei, kwa ndongabyako ulitaka amgawie nani uongozi
🙏
 
Back
Top Bottom