Lini Watanzania tutaamka na kusema IMETOSHA?

Lini Watanzania tutaamka na kusema IMETOSHA?

Dunia haina huruma na watu masikini raslimali tele zimejaa wekeza kwenye akili uzivune nawe uwe kama wao
 
Watz wepi hawa ambao wanafeed brain zao ngono,simba na yangu, freemason Toka asubuhi had jioni ndio wataleta changes!
You is what you think.
 
Viongozi ni kioo cha wananchi Mkuu.

Ukiona viongozi wa jamii Fulani ni wajinga, wezi, Wala rushwa au sifa zozote zile mbaya elewa jamii wanayotoka kwa sehemu kubwa ndio iko hivyo.

Jamii yenu akili haiwezi kuongozwa na kiongozi Mjinga
Jamii ya Watu waadilifu haiwezi kuongozwa na kiongozi asiye muadilifu

Tafakari
🌤️🙋‍♂️🎯✍️🤝👏🙏🎁
 
Bongo mtu akipewa cheo anatengeneza retention pattern. Hataki kwenda kinyume na waliompa cheo hata kama watakuwa wanam mislead. Hio ni aina ya cancer ambayo Watanzania wengi tunayo na yote ni sababu ya njaa. Njaa imetufumba akili kiasi cha kwamba tupo radhi hata kulamba mavi ili tu tuendelee kuwepo kwenye nafasi.

Zama za Nyerere kulikuwa na Patriotism ya hali ya juu. Endapo mtu alikuwa hafurahishwi na mwenendo wa serikali alikua na option ya kujiuzulu ili tu kulinda integrity yake. Sikuhizi hilo halipo, ni mwendo wa kusifu na kumuabudu mwenyekiti. Siasa zimekuwa sio za kujenga hoja na kuzitetea bali ni za upambe nuksi. Yote hio sababu ya ufisadi na rushwa zilizokithiri na kutengeneza mithili ya food chain kwenye chama. Siasa za makundi na vibaraka ni hasara tupu.
 
Wow! Kwani nani amekusemea wewe? Hao watu ni wapi wasiojulikana? Kwani wamekutuma au umejituma? Kama huna hoja si unyamaze tu.
Wewe ni typical CCM mnachukia sana kuona watu wakisaidiwa na wengine.
 
Ukiniuliza kama Tanzania ina kiongozi, nitajibu kuwa ina rais lakini si kiongozi. Ukiuliza kama Tanzania ina sera, nitakujibu kuwa ipo sera ya uchawa.

Ukiuliza, kiuchumi Tanzania inaongozwa na nini, nitakujibu kuwa sera yake ni ya shamba la bibi ambapo wezi huja na kugema watakavyo.

Ukiuliza kama Tanzania ni salama, nitakushauri ufanye utafiti na kuassess utekaji na kuporomoka kwa majengo.

Ukiuiza kama Tanzania ina future, nitakujibu kuwa hata past haina. Kama mwanafalsafa, nawaza tu.

Ukiuliza kama serikali inakusanya kodi na kuzitumia vizuri, nitakujibu kuwa inawakamua maskini na kuwapa matajiri wakwepa kodi na wapiga dili wanaoshirikiana na wanasiasa mafisi.

Ukiniuliza kama Tanzania ni kisiwa cha amani, nitakujibu kuwa ni kisiwa cha vurugu kinachongoja kulipuka.

Kwa wananchi wanavyoteseka huku watawala wakitanua, Tanzania inaweza kuzidiwa na hata Somalia.

Je, ni lini watanzania wataamka na kusema katu kuwa inatosha?
Wewe uliishamka?
 
We wacha tu. Leo Wasira anadai kuwa Watanzania tuna njaa. Hili ni tusi kubwa sana na dharau kwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom