Lionel Messi Hana Sifa za Uongozi kama za Cristiano Ronaldo

lembu

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2009
Posts
17,951
Reaction score
23,705
Tumeshuhudia Lionel Messi kwa muda mrefu akisota na timu yake ya Taifa kuipa mafanikio tangu kombe la Dunia 2006 hadi mwaka jana 2018 tofauti na mafanikio makubwa aliyoiletea klabu yake ya Barcelona

Pamoja na kuwa na mastaa wengi, Argentina bado imeendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu kwa kuondolewa mapema kwenye mashindano muhimu kuanzia makombe yote ya Dunia Messi aliyoshiriki (ukiondoa ile ya Brazil ya mwaka 2014 ambako Argentina ilifika fainali), kwenye Copa America nk

Argentina inachokosa kikubwa ni uongozi
Kwenye uongozi kinachohitajika ni
  1. Inspiration - aweze kuwatia hamasa wenzake hata wakati wa hali ngumu ili washinde
  2. Kujengewa wachezaji positive and winning mentality
  3. Communication - aweze kuwa medium/njia laini na rahisi ya mawasiliano- kusiwepo na gap ya mawasiliano yenye kusababisha mahusiano mabaya, magomvi na kutoaminiana kwenye timu
  4. Unification au kujenga timu kila mtu ajione ni sehemu ya timu na peke yake hakuna mafanikio
  5. Kuwajengea wenzako Uzalendo - kwamba kila mchezaji ajue kuwa mafanikio ni lazima kwa ajili ya familia yake, marafiki zake, Ndugu zake, nchi yake na kila mchezaji awe tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya malengo hayo
Hizo sifa zote Messi hana
  1. Messi is not a good communicator
  2. Ukimya wake unapitiliza na mara nyingi hana muda wa kuwatia ari na hamasa wenzake
TOFAUTI NAYE
Cristiano Ronaldo hizi sifa anazo na ndizo zilizomletea kupata mafanikio kwenye timu yake ya Taifa na wenzake wanampenda sana
Makosa makubwa timu nyingi za mpira zinafanya ni kwa vile mchezaji ni mzuri uwanjani basi na wampee na unahodha wa timu wakati sifa za uongozi hana

Karibuni kama mna maoni, michango ijikite kwenye sifa za uongozi na sio uchezaji wa hao wawili
 
"Naitwa Bonifasi Mkwasa, samahanini sana kwa zile goli 7, saivi tumefafanya mamadiliko makubwa..tumebadilisha nahodha, tumemtoa Canavalo tumemuweka Samatta"
 
Pamoja na Yote Messi Bado anabaki kuwa ndiye mchezaji wa kiwango na kipaji cha kipekee kuwahi kutokea duniani
 
Mkuu kuna Utofauti Mkubwa sana wa Malezi, Elimu na Utamaduni Kati ya Ulaya (CR) na America Kusini (LM).
America kusini wachezaji wake wote Dizaini ya Wachezaji wa Manzese, TMK nk so CR usimlinganishe na hao Machoko kitabia na haiba.
 
Mkuu kuna Utofauti Mkubwa sana wa Malezi, Elimu na Utamaduni Kati ya Ulaya (CR) na America Kusini (LM).
America kusini wachezaji wake wote Dizaini ya Wachezaji wa Manzese, TMK nk so CR usimlinganishe na hao Machoko kitabia na haiba.
Messi kalelewa Ulaya na Barcelona Toka miaka 9 Kama sijakosea, Na Ronaldo pia ni mreno mwenye asili ya Brazil.
 
Kuweka ushabiki kando, binafsi nimekuelewa sana tu.Ni sawa na Kumpa ukiranja mkuu anayeshikaga ukwanza darasani bila kujali uwezo wake wa kiuongozi.Hongera sana mleta mada...!
 
Hivi Ronaldo amekiongoza nini?
-Ameibeba timu yake kuipeleka world cup vs Sweden kwenye playoff anafunga Hat trick mbele ya Ibra. Moja Kati ya mechi Kali Sana kupata kuiona.
-kwenye Euro mechi karibia zote either anafunga ama anatoa pasi ya Goli kasoro fainali. Na fainali yenyewe alivyoumia akawa kocha yeye.

Portugal Sasa hivi ni wazuri Wana young players ambao Wana potentials kubwa Sana, ila at that time Ronaldo alikuwa akicheza na watu wa kawaida Sana Kama Eder, carvalho, Silva, joao Mario, quaresma etc

Ukitaka nitakuekea clips za Euro jinsi Ronaldo alivyoibeba timu yake Hadi fainali
 
Huyu babu kashazeeka hana lolote lile atandike daluga tu..sasa hivi kiwango zero anaanza kusingizia rushwa ..the fact kwamba hawez kukubali brazil is one the the best national team in the world na wamedhihirisha hilo kwa kuchukua ubingwa wa copa America..
Messi kwishaaaa
Kwangu Messi ni bora kuliko CR7 mana hata kama hajafunga ananivutia anavyocheza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…