lembu
JF-Expert Member
- Dec 31, 2009
- 17,951
- 23,705
Pamoja na kuwa na mastaa wengi, Argentina bado imeendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu kwa kuondolewa mapema kwenye mashindano muhimu kuanzia makombe yote ya Dunia Messi aliyoshiriki (ukiondoa ile ya Brazil ya mwaka 2014 ambako Argentina ilifika fainali), kwenye Copa America nk
Argentina inachokosa kikubwa ni uongozi
Kwenye uongozi kinachohitajika ni
- Inspiration - aweze kuwatia hamasa wenzake hata wakati wa hali ngumu ili washinde
- Kujengewa wachezaji positive and winning mentality
- Communication - aweze kuwa medium/njia laini na rahisi ya mawasiliano- kusiwepo na gap ya mawasiliano yenye kusababisha mahusiano mabaya, magomvi na kutoaminiana kwenye timu
- Unification au kujenga timu kila mtu ajione ni sehemu ya timu na peke yake hakuna mafanikio
- Kuwajengea wenzako Uzalendo - kwamba kila mchezaji ajue kuwa mafanikio ni lazima kwa ajili ya familia yake, marafiki zake, Ndugu zake, nchi yake na kila mchezaji awe tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya malengo hayo
- Messi is not a good communicator
- Ukimya wake unapitiliza na mara nyingi hana muda wa kuwatia ari na hamasa wenzake
Cristiano Ronaldo hizi sifa anazo na ndizo zilizomletea kupata mafanikio kwenye timu yake ya Taifa na wenzake wanampenda sana
Makosa makubwa timu nyingi za mpira zinafanya ni kwa vile mchezaji ni mzuri uwanjani basi na wampee na unahodha wa timu wakati sifa za uongozi hana
Karibuni kama mna maoni, michango ijikite kwenye sifa za uongozi na sio uchezaji wa hao wawili