Lionel Messi kumpiku Karim Benzema kwenye tuzo ya Ballon d'or mwaka 2022

Lionel Messi kumpiku Karim Benzema kwenye tuzo ya Ballon d'or mwaka 2022

Hapana. Kwa mwaka huu haina mjadala BENZEMA anabeba. Messi mwenyewe majuzi kakiri kuwa mwaka huu hakuna ushindani kwenye ballon d or maana benzema hana wa kumshinda. Namkubali messi mno ila hii tuzo mwaka huu apewe tu benzema
Tatizo tuzo inatolewa baada ya kupiga kura. Messi anao ushawishi mkubwa kuliko benzema katika ulimwengu wa michezo.
 
Ww jamaa ni team messi tu hakuna lolote benzema anarekodi gani mbya ya kinidhamu?
Mkuu labda wewe hufuatilii mpira. Benzema hata timu ya taifa alikuwa haitwi kwasababu ya maswala ya nidhamu.
 
Mara baada ya mechi ya jana kwenye UEFA Cup of Champions (Finalissima) wachezaji wa Argentina walionekana kumbeba Messi na kumrusha juu katikati yao.

Kwa kawaida hili huwa anafanyiwa kocha wa timu kama ikitokea wamebeba kombe. Kitendo hiki kinatafsiriwa kwamba Messi ndiye aliyeibeba timu.

Messi alitoa assist mbili kwenye mchezo huo wa jana na amebeba Lique 1 kwa ngazi ya klabu. Benzema kabeba UCL na Laliga.

Tutarajie Messi kushinda tuzo ya msimu huu kwasababu huwa anapendwa UEFA.
Hata iweje watu inabidi wajiandae kisaikolojia tu kuwa enzi za Messi zimeishia hapo!!! Msimu mzima kwenye ligi ya ufaransa ana magoli 6 tu. AQmeshindwa kuibeba timu yake kwenye ligi ya mabingwa!! Huu ni mwaka wa BENZEMA tupende tusipende!!
 
Argentina siyo timu ya kubeba kombe la dunia!!
Haujawaona Argentina tangu walipopambana kubeba Copa America na sasa ni wazuri sana.

Italy wamefungwa jana, na hawatakuwepo wc. Timu zilizobakia inayoweza kuwasumbua labda ni england na spain. France sio wakali sana kwasasa, germany na belgium wameisha na brazil hawaeleweki.

Anabakia senegal tu kama mshindani mkubwa wa Argentina.
 
Back
Top Bottom