Lionel Messi kumpiku Karim Benzema kwenye tuzo ya Ballon d'or mwaka 2022

Hapana. Kwa mwaka huu haina mjadala BENZEMA anabeba. Messi mwenyewe majuzi kakiri kuwa mwaka huu hakuna ushindani kwenye ballon d or maana benzema hana wa kumshinda. Namkubali messi mno ila hii tuzo mwaka huu apewe tu benzema
Tatizo tuzo inatolewa baada ya kupiga kura. Messi anao ushawishi mkubwa kuliko benzema katika ulimwengu wa michezo.
 
Ww jamaa ni team messi tu hakuna lolote benzema anarekodi gani mbya ya kinidhamu?
Mkuu labda wewe hufuatilii mpira. Benzema hata timu ya taifa alikuwa haitwi kwasababu ya maswala ya nidhamu.
 
Hata iweje watu inabidi wajiandae kisaikolojia tu kuwa enzi za Messi zimeishia hapo!!! Msimu mzima kwenye ligi ya ufaransa ana magoli 6 tu. AQmeshindwa kuibeba timu yake kwenye ligi ya mabingwa!! Huu ni mwaka wa BENZEMA tupende tusipende!!
 
Argentina siyo timu ya kubeba kombe la dunia!!
Haujawaona Argentina tangu walipopambana kubeba Copa America na sasa ni wazuri sana.

Italy wamefungwa jana, na hawatakuwepo wc. Timu zilizobakia inayoweza kuwasumbua labda ni england na spain. France sio wakali sana kwasasa, germany na belgium wameisha na brazil hawaeleweki.

Anabakia senegal tu kama mshindani mkubwa wa Argentina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…