Sijui utajitofautishaje na mpinga Kristo , sijui utajitofautishaje na mdharau Mungu ,sijui utajitofautishaje na muasi shetani.
Katika ufahamu na mafundisho mbalimbali ya maisha na elimu ya dini tumekuzwa kwa kulitukuza,kuliheshimu ,kuliheshimu na kuliabudu jina la Nyumba wetu yaani MUNGU.
Sasa kwako nimerudia Mara mbilimbili kusoma Uzi wako nikijaribu kutafuta unafananisha nn au una maana gani? Nimeshangazwa na uandishi wako wa neno Mungu lenye kuanza na herufi kubwa kumfananisha na Messi.
Hakika huku ni kutukosea heshima na dharau iliyojaa kiburi kisa soka kumlinganisha binadamu na Muumba wetu.
Binafsi ningekuomba ujitafakari na utumie mifano mwingine mingi na bora kumsifu Messi na kumponda Cr7 na jamii ya wapenda soka ingekuelewa