Lionel Messi ni zaidi ya mchezaji japo naichukia Barcelona

Lionel Messi ni zaidi ya mchezaji japo naichukia Barcelona

Messi ana mkataba wa maisha na Barca – Rais Barcelona Bartomeu September 9, 2016

Messi-badge.jpg


Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu ameviambia vyombo vya habari kwamba staa wao, Lionel Messi ana mkataba wa milele na klabu yao wakati huu wakijiandaa kufanya majadiliano ya mkabata mpya katika miezi ijayo.

Messi, 29, ana mkataba ambao utafikia ukomo June 2018. Pamoja na hayo, katika majira haya ya joto, staa huyo wa Argentina alihusishwa na mpango wa kuungana tena na kocha wake wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola, katika klabu ya Manchester City pia kurudi katika klabu yake ya utotoni, Newell’s Old Boys baada ya World Cup 2018, kitu ambacho Messi mwenyewe alisema angependa iwe hivyo.

Bartomeu amefanya mazungumzo ya kuongeza mkataba wa Messi kuwa kipaumbele hivi sasa.

“Messi ana miaka yote anayotaka kuwa nayo na Barcelona. Lionel Messi ni mchezaji bora zaidi kuwahi kuuchezea mpira wa miguu katika historia ya dunia na anaichezea timu yetu” alisema Bartomeu. “Tuna furaha sana, ni mtu muhimu sana kwa klabu, ni muhimu sana kwa mashabiki, ni muhimu sana kwa mpira wenyewe”

“Na tunaenda kuongea naye katika miezi inayokuja na yeye anajua, na anajua tayari ana mkataba wa milele. Hakuna ukomo kwake.”

“Ukomo utaamuliwa na yeye, kwa sasa ana miaka 29, ana kipaji na malengo makubwa, yupo katika umbo zuri kuendelea kung’aa kwa miaka mingi ijayo”

Bartomeu alienda mbele na kusema anategemea majadiliano yatamalizika haraka, aliongeza: “Kwa sasa, tunadhani tutalifanya hili katika miezi ijayo, na Lionel Messi ataendelea kuwepo Barcelona, kwa hakika”

Messi alirudi kuichezea timu yake ya taifa wiki iliyopita baada ya kustaafu kwa muda mfupi hiyo ikiwa ni baada ya kuumizwa na kufungwa kwa penati dhidi ya Chile katika fainali ya Copa America.

Aliisaidia timu yake katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Uruguay, japokuwa aliumia wakati mechi ikielekea kuisha hivyo hakuweza kucheza katika mechi ambayo Argentina ilitoka sare ya 2-2 na Venezuela, Jumanne. Barcelona bado hawajasema tarehe ambayo Messi atarejea.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Hamna Club ambayo Messi ana hadhi ya kwenda kucheza.

Manchester?
Chelsea?
Bayern?
Arsenal?
PSG?

Hata wewe ungekuwa Messi usingeweza kuondoka Barca na kwenda Club zingine.
hata biblia inakataza kuwafunga pamoja ng'ombe mkubwa na mdogo wakati wa kulima. hata gari, huwezi weka tairi kubwa kulia na dogo kushoto. na ndiyo maana kuna shule za vipaji maalumu. Messi kwenda huko ni sawa na mtu wa chuo kikuu kukariri la saba, ataonea wengine huku akijidumaza.
 
Kweli nimiamini messi ni dili kama vile bro wake el diogo ktk era yake
 
  • Thanks
Reactions: PNC
hata biblia inakataza kuwafunga pamoja ng'ombe mkubwa na mdogo wakati wa kulima. hata gari, huwezi weka tairi kubwa kulia na dogo kushoto. na ndiyo maana kuna shule za vipaji maalumu. Messi kwenda huko ni sawa na mtu wa chuo kikuu kukariri la saba, ataonea wengine huku akijidumaza.
Aha ha ha ha ha ha ha ha ha ha!
 
ila mbona bado wazee wa miaka hiyo ya akina DELIMA hawaji na comments zao..ina naana wote humu ni kizazi cha messi na christiano...duh..kumbe wengi wachanga humu

Barca 3- Madrid 0. Ronaldo 'The Phenomenon' katika hii mechi alikuwepo, kama vile Alivyokuwepo Mkongwe Zidane. Messi kama kawa alicheza vyema na Mashabiki wa Madrid hawakuwa na hiyana kumpongeza Ronaldinho kwa ufundi wake.

 
Back
Top Bottom