Lipi jema kwa Mswahili / Mwafrika kati ya Kuchagua Kuishi maisha ya Kujitenga nao waseme Unaringa au Kujichanganya nao Wakuzoee na waanze Kukudharau?

Yaani kama kuna Siku ambayo GENTAMYCINE nitajikita Kusoma sana tu Comments zenu basi ni katika huu Uzi wa leo.
Wife alinifundisha falsafa moja siku zote huwa ananikataza kuzoeana na watu wa mtaani ( To be cheap)

Mimi huwa sizoeleki na siluhusu mazoea na Ni MTU mwenye mipaka (boundaries) Ila Ni MTU wa watu najumuika na watu

Kwa Sasa Ni hayo
 
Wewe Ni Mimi mtupu kabisa..
 
Pamoja sana Mr talented and entertainer..


Kama baridi ni kali bhas tukupatie bendera uiwakilishe Nchi vyema huko kwa kupiga show ya kuelewaka.
Mademu wa hapa Kampala Uganda nawaogopa sana Mkuu kwani ni Wazuri na wana Makalio mazuri, ila wana Moto mno.
 
Wife alinifundisha falsafa moja siku zote huwa ananikataza kuzoeana na watu wa mtaani ( To be cheap)

Mimi huwa sizoeleki na siluhusu mazoea na Ni MTU mwenye mipaka (boundaries) Ila Ni MTU wa watu najumuika na watu

Kwa Sasa Ni hayo
Mimi hili la Kuzoeana na Watu wa Mtaani limenigharimu mno Mkuu kiasi kwamba wananiona ni Mwenzao ( Cheap ) wakati kumbe Mimi hulka yangu ( na hata Marafiki na Ndugu zangu Watatu hapa JamiiForums wanaoijua hii ID yangu ) wanajua kuwa GENTAMYCINE napenda mno Kujichanganya na Watu wa Rika na Hali zote za Kimaisha na sipendi Makuu au Ukubwa au Kujulikana labda Status yangu ya Kifamilia na Kimaisha ila cha Kushangaza hao ninaowafanyia yote haya wananiona kama Mpuuzi fulani au Chizi fulani vile.

Na Mkuu najitahidi mno kutaka Kuishi Maisha ya Kuwapotezea ila nashindwa kwakuwa hiyo Kiumbwaji na Mwenyezi Mungu siyo Hulka yangu kabisa. Yaani sijui nifanyeje hakyanani. Ukisema tu uwe peke yako peke yako bado wataanza Kusema GENTAMYCINE anajiona Matawi hivi na vile. Sijui umfanyie nini / lipi Mswahili akuelewe na muende nae sawa.
 
Tatizo linapokuja huku afrika Kuna kuingiliana sana yani Kuna mipaka Fulani unajaribu kuiweka kwenye maisha yako lakini Bado watu huvunja mipaka hiyo, mwanaume mwenye akili timamu lazima Kuna 'boundaries' utajaribu kuziweka lakini hizi people zinajaribu kukatiza kwenye mistari miyekundu kitu ambacho lazima utagombana nao hivyo wanataka uwafuate wao jinsi watakavyo kitu ambacho Kwa mwanaume mwenye akili iliyopevuka hawezi kuruhusu Hilo, hivyo basi ishi kulingana na ww unavyoona inafaa ilimradi huvunji Sheria, humuumizi mtu Wala hujiumizi ww mwenyewe.
 
What a Logical comment. Asante sana Mkuu na nimekukubali. Uko vizuri Kichwani.
 
Kujitenga na watu kiaina kuna kuweka katika safe haven. Maana kuwa karibu au kuwa na circle ya marafiki wengi kuna ku expose weakness na strength zako kwa hiyo inakuwa rahisi kwao kukupigia mule mule. Kujitenga na watu kunakufanya kutotabirika kwao.
 
Mademu wa hapa Kampala Uganda nawaogopa sana Mkuu kwani ni Wazuri na wana Makalio mazuri, ila wana Moto mno.

Mambo ya dalii kimoko sio?

Wewe mzee wa Rhumba na Lingala.. Kumbuka ushauri wa Legend Remmy Ongalla... Mambo kwa soksi...

Hata ukichelewa... Kwani unataka kuwahi wapi I!?
 
Kwa sisi ngozi ya Tako nakushauri ujitenge tu japo matukio ya kijamii kama misiba usikose ,hapa matukio ya kijamii simaanishi harusi manake siku hizi nayo imekuwa chuma ulete

We jitenge fanya yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…