Lipi la kujivunia miaka minne ya JK Ikulu?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363




DESEMBA 21, mwaka 2009, Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Awamu ya Nne Tanzania anatimiza miaka minne ya kukaa madarakani, tangu alipoapishwa kuwa Rais Desemba 21, 2005.

Kazi ya urais si nyepesi kama wengi wanavyodhani, kama muasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alivyohoji, wapinzani wanakimbilia Ikulu kuna nini?

Kazi ya kuongoza watu ni nzito aliyotwishwa na Watanzania tangu kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Tanzania Desemba 14, 2005.

Mtihani wa kwanza mkubwa alipoingia Ikulu ya Magogoni, ilikuwa kushinda shinikizo kubwa la wanasiasa waliotaka kulipwa fadhila kwa kupewa vyeo eti kwa sababu kaingia Ikulu.

Katika kundi la mamba hata kenge wamo, wapo waliotaka kupewa fadhila hizo kwa sababu za kibiashara na shughuli nyingine ili kuzifanya zipite kiulaini.

Rais akafanya uteuzi wa Baraza la Mawaziri 60, wananchi wengi wakahoji juu ya ukubwa wa baraza hilo ingawa Rais Kikwete mwenyewe alisema amefanya hivyo ili kusukuma mambo ya maendeleo kwa kasi kubwa aliyoitazamia.

Kuunda Baraza la Mawaziri, Mawaziri kamili 30 na Naibu Mawaziri zaidi ya 30 kutokana na miongoni mwa wizara kuwa na manaibu wawili, si jambo la kawaida.

Hilo lilikuwa baraza kubwa kwa serikali na walipa kodi wake. Hata hivyo pamoja na nia nzuri ya Rais kuwateua wasaidizi wake, kilichotokea ni baadhi ya mawaziri kutotimiza wajibu wao ipasavyo hatua iliyomfanya Rais Kikwete kupanga upya safu ya Baraza lake na kupunguza ukubwa wake.

Kuhusu rushwa, Rais Kikwete amejitahidi sana kuijengea uwezo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Si siri kwamba chombo hicho hivi sasa kina nyenzo za kufanya kazi vizuri kuliko ilivyokuwa enzi za utawala wa serikali zilizopita.

Lakini kukipa nyenzo chombo hicho pekee yake hakutoshi, wananchi wanaona bado tuhuma za vigogo kujihusisha na rushwa bado zinakaliwa.

Katika hotuba zake nyingi hasa anapozungumza na Watanzania, Rais Kikwete hutamka maneno mazito dhidi ya namna atakavyopambana na rushwa, lakini baadhi ya watendaji katika vyombo husika hajawashawishi Watanzania wakaridhika na kasi yake ya uchukuaji wa hatua kwa vigogo wanaotajwa kuhusika na vitendo vya rushwa.

Penye ufisadi, hakuna haki. Pasipo na haki, hakuna amani. Na pasipo na amani, hakuna maendeleo, hivyo kwa kushughulikia polepole masuala ya mafisadi ni sawa na kuendelea kufuga ufisadi serikalini ambao ni maadui wakubwa wa taifa hili.

Kwa mfano, baadhi ya mawaziri mpaka sasa, bado wanaandamwa na tuhuma nzito za ufisadi, na wengine wametajwa kwa majina hadharani, lakini vyombo vinavyohusika ikiwemo Takukuru vimekuwa na kasi ndogo ya kuchukua hatua.

Mbali ya ufisadi kufunika anga la siasa nchini, upande mwingine mambo mengine yakiwamo ya kilimo, yanakwenda vizuri.

Rais Kikwete ameingia na kasi ya ‘Kilimo Kwanza.’ Ukweli katika ngazi ya rais, kilimo kwanza kimekwenda vizuri, kilichobaki ni utekelezaji katika halmashauri na wilaya.

Kuimarika kwa mikakati ya kilimo, kumemfanya Rais Kikwete sasa aanze kuelekeza nguvu kwenye sekta ya mifugo.

Sekta hiyo ambayo iliipa uzito wa aina yake kwa kuiundia Wizara (Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) imekuza kwa kiasi kikubwa ufugaji na uvuvi.

Katika kuhimiza sekta ya mifugo, ambayo yeye mwenyewe ni mdau kama mfugaji kule Bagamoyo, amepita kukagua mashamba mbalimbali ya mifugo mkoani Iringa na kuona mafanikio na changamoto zilizopo.

Kilimo Kwanza, kimeanza pamoja na kampeni za kuhakikisha halmashauri zinakuwa na matrekta ya kukodisha wakulima wadogo ili waachane na jembe la mkono, lakini pia ameimarisha mfumo wa upatikanaji pembejeo kwa kuanza kutumia vocha na stakabadhi ghalani ili kutowanyosha wakulima jasho lao.

Jitihada zinafanyika hata kama kasi katika baadhi ya maeneo ni ndogo. Kuhusu elimu, Rais Kikwete amezoa sifa tele, kuanzia kwenye shule za awali hadi ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma (Udom) ambacho kitakuwa kikubwa zaidi Afrika Mashariki.

Watanzania wanakubaliana na kasi hiyo, wanajua matunda yake si ya mwaka kesho au keshokutwa, ya karne.

Mbegu anayoipanda itachelewa kutoa matunda katika elimu, lakini ipo siku itatoa matunda yatakayokuwa kumbukumbu ya karne.

Katika sekta hiyo kilio cha wananchi kimebaki kwenye miundombinu ya kuboresha elimu hiyo, hasa uhaba wa walimu, nyumba za walimu, vifaa vya maabara na zana nyingine muhimu katika kutoa elimu bora wala si bora elimu.

Kampeni ya Rais imeelekezwa katika kujenga zahanati katika kila kijiji kilicho umbali wa kilometa tano kutoka ilipo nyingine, lakini pia kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya, wilaya inakuwa na hospitali na mkoa unakuwa na hospitali ya rufaa.

Hospitali za kanda za rufaa za kanda na taifa zifanya kazi hiyo si kutibu mafua. Upande mwingine ambao umeonekana katika kipindi cha miaka minne ni kuhusu vyama vya akiba na mikopo.

Kikwete ameimarisha Saccos, kwanza alianza kwa kasi ya kuingiza mabilioni, yaliyojulikana, ‘Mabilioni ya Kikwete.’

Pamoja na nia nzuri ya kuwajaza mapesa Watanzania, bado kuliingia urasimu wa ajabu kuanzia kwenye benki hadi kwa wale waliopewa dhamana ya kuchagua wakopaji mikopo hiyo.

Walijipendelea, wakajikopesha na kujinufaisha, hivyo walio wengi wakabaki na kiu ya mapesa na umaskini ukazidi kuwakaba.

Wakati anaingia madarakani miaka minne iliyopota, ilikadiriwa kwamba ndani ya kipindi cha miaka mitano, kutakuwa na maambukizi mapya ya Ukimwi kwa zaidi ya watu 1,000,000 na vifo 500,000, lakini kwa kazi ambayo serikali yake imefanya katika kipindi cha miaka minne tu takwimu hizo zitashuka.

Lakini mafanikio makubwa ambayo Rais Kikwete ameyapata katika kipindi cha miaka minne ni namna alivyoiendesha kampeni dhidi ya Ukimwi.

Ukimwi ni tatizo kubwa katika nchi yetu na Rais ameonesha kutambua hilo. Hatua ya Rais Kikwete kuanzisha kampeni ya kitaifa ya kupima Ukimwi kwa hiari na yeye na mkewe Salma kuwa watu wa kwanza kupima Ukimwi hadharani, ilikuwa ni changamoto chanya.

Hata hivyo hali ya kipato cha wananchi bado ipo chini, umasikini unatesa mamilioni ya Watanzania. Zaidi ya asilimia 54 ya Watanzania ni masikini, na kati yao asilimia 18.7 ni masikini wa kutupwa ambao hawana hakika hata ya mlo mmoja kwa siku.

Hali hiyo inabaki kuwa changamoto katika kipindi kinachobaki. Mkakati wa serikali wa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo vya maji, ilioutangaza Aprili mosi, mwaka 2006, kwa hakika, umeleta matunda mazuri.

Ardhioevu ya Ihefu, Mbarali na unakoanzia mto mkuu wa Ruaha kwenye mpango wa milima Livingstone, na mahali pengine nchini, imejirudia hali yake ya zamani kwa kasi, maji yameongezeka na uoto wa asili umetanda kila mahali.

Rais Kikwete anapenda michezo, hatasahauliwa katika kuimarisha, kudumisha na kuendeleza michezo, licha ya kumtafuta kocha wa kuinoa timu ya Taifa (Taifa Stars) Marcio Maximo, lakini pia amekuwa akimlipia kocha kwa muda wote. Wakati mwingine amekuwa akikemea vitendo vinavyoharibu sura ya nchi katika michezo. Mikakati hiyo

ya maendeleo inayosimamiwa na Rais Kikwete imeleta matokeo mazuri baada ya Taasisi ya Utafiti wa Demokrasia Tanzania (REDET) kuonesha kwamba, licha ya kasoro za hapa na pale zinazoiandama serikali ya awamu ya nne,

lakini bado Watanzania wana imani na Rais Kikwete ingawa hawana imani na serikali yake. Sekta na idara zilizotajwa hapo juu ni chache kati ya nyingi ambazo amezifanya vizuri katika utendaji wake hata kama kumekuwa na dosari ndogo ndogo, serikali ya awamu ya nne inayo ya kujivunia.

Hayo ni miongoni mwa mambo mengi ya kujivunia ya Rais Kikwete, ambaye leo ametimiza miaka minne akiwa Ikulu.

Ni ukweli kwamba machoni mwa Watanzania Rais Kikwete anaaminika, taasisi za kimataifa zinamuheshimu, kazi kwao watendaji wake ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya taifa la Tanzania.

http://www.habarileo.co.tz/makala/?n=4931
 
La kujivunia ni kwamba amewajuza watanzania kwamba 70% yao ni fuata-upepo!...Lakini pia amewafundisha watanzania kwamba maisha bora hayawezekani, na kuwa chama chake kinataka matajiri tu, maana masikini wakichekewa wataishia kukichangia kuku...Nawsilisha.
 
"lakini bado Watanzania wana imani na Rais Kikwete ingawa hawana imani na serikali yake".

Really????????????????
 
mimi binafsi cha maana saana ninachoona huyu bwana kafanya ni:

1 ile hotuba ya kwanza bungen (ilikuwa nzuri)
2 kumlazimisha mahita astaafu mapema
3 kumwachisha kazi balozi mahalu na kusema ni mwizi
4............
5..........

mapungufu yake huyu bwana

1 amekuwa na fadhila sana
2 anakurupuka katika maamuzi
3 ni rahisi sana kudanganyika huyu bwana na kufaata ushauri wa mtu ambao ni uongo
4 amekuwa na safari nyingi sana
5 mpaka sasa amesimama huu ya mabega ya mkapa
6 usalama wa taifa unafanya kazi yake sana lakini mkulu hafanyii kazi majalida na riport anazopewa,
7 maendeleo mengi ni ya kinadhalia sana
8. anapenda kuwa na marafiki matajiri wakati yeye ni masikini
9. kuna hatari huyu bwana akaikwaza nchi hii kuliko hata mwenzake aliyepita.
10...........
11...........
12---------


huyu mimi bwana eti hanifani jamani sijui nyie wenzangu!
 
Mzizimkavu this whole story ya mafanikio ya jk is bulshit....umetumwa nini. Huyu bwana hatufai ni bora tukae bila prezdaa na tuongozwe na council of religious leaders maana tukienda makanisani na misikitini huko angalau tunapewa matumaini ya mbingu mpya na nchi mpya. Kuliko hyo jk wako mwongo..............!
Mtumie salamu
 

fikiria asingekuta pesa hazina mkapa kazitunza nchi ingekuwaje.
Huyu bwana is empty headed!!!!!!!!!
 
Maisha yamezidi kuwa magumu, wananchi wanyonge wanazidi kuonewa na wenye mali haki hakuna (upebari mambo leo), hakuna matumaini yoyote kila mtu mnyonge ananung'unika, kipato cha kaya kimepungua hali ni mbayaa sana, , pato la taifa haligawanyiki kiusawa, wizi umezidi serikalini na katika idara zake kiasi kwamba pesa za bajeti zinamalizikia huko huko juu bila kuwafikia walengwa, halmashauri zetu rushwa lukuki, elimu inazidi kudidimia hasa ya msingi na secondary, majengo ya shule za kata ni mengi kudanganya watu, hakuna ustawi wa jamii.
 


Kweli tunamatatizo makubwa ya uelewa wa uongozi na uchambuzi wa mambo! Huwezi kupima mafanikio ya Rais ama uongozi wowote ule bila kuwa na mlinganisho (benchmark). Ndio maana kuna ilani ya chama (manifesto).

Mafanikio ama kushindwa kwa utawala wa kikwete kunapaswa kupimwa against certain benchmarks ambazo yeye mwenyewe na chama chake cha CCM walijiwekea wakati wanaomba ridhaa ya kuongoza taifa hili AMA katika kipindi hicho hicho cha miaka minne tumpime kwa kumlinganisha na mtangulizi wake (i.e utendaji wa Kikwete 2006-2009 against utendaji wa Mkapa 2000 to 2004).

Hapo angalau tunaweza kupata ulinganishi mzuri, lakini sio hivi ambavyo mashabiki na wapenzi wa kikwete wanavyoorodhesha mafanikio yake. Ukisoma habari hiyo hapo juu, unakufanya uamini kuwa nchi inaendeshwa bila dira, kwa sababu mwandishi anadokoa dokoa 'mafanikio ya Kikwete' kama vile alitarajia Rais asingefanya chochote katika hii miaka minne, kwa hivyo ameshangazwa kwa hayo yaliyofanywa!

Ukipima, objectively, what president kikwete has so far achieved against what he promised to achieved under his famous slogan of Maisha bora kwa kila Mtanzania both quantitatively and qualitatively, he will not even score 20% (no matter lenient the analyst is).

Ndo maana sishangai kusikia wapambe wake wakimridhisha kwa kumwambia Watanzania wana imani na Rais Kikwete ingawa hawana imani na serikali yake, which is RIDICULOUS to me!! How can it be possible wakati yeye ndo mkuu wa hiyo serikali????
 
Lakujivunia:

Ametoa uhuru mkubwa wa watu kutoa maoni yao juu ya serikali, bunge, mahakama na hata vyama vyao vya siasa, michezo n.k. Hakuna kuzibana midomo hapa. Hongera sana Rais Kikwete kwa uvumilivu huu.

Mapungufu:

1. Anapenda sana kusafiri nje wakati kuna watu chini yake ambao wanaweza kufanya hivyo kwa gharama ndogo.

2. Anaogopa au hana jeuri ya kuwafokea wateule wake wanaofanya kazi vibaya kwenye chama na serikalini.

3. Inamchukua muda mrefu kusoma alama za nyakati kuhusu mstakabali wa amani na maendeleo ya Tanzania. Tafadhali Mheshimiwa Rais Kikwete acha mzaa katika mambo haya.
 
Na hao wenye haki ya kukimbilia Ikulu, wanatafuta nini na kwa nini wao tu ? Na huyu naye alikimbilia Ikulu kutafuta nini na kama alidhani Uraisi ni rahisi, mbona kashindwa kutulia hapo - leo huku, kesho kule na je, kesho kutwa ?

Kuhusu rushwa, Rais Kikwete amejitahidi sana kuijengea uwezo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Si siri kwamba chombo hicho hivi sasa kina nyenzo za kufanya kazi vizuri kuliko ilivyokuwa enzi za utawala wa serikali zilizopita.
Ndio, ameijengea Takukuru uwezo mkubwa na imefanya kazi nzuri sana ya kuwakingia kifua watoa rushwa na kuwasafisha wala rushwa. Takukuru ya sasa si kichekesho tu bali ni kielelezo tosha ya mapungufu ya awamu hii.

Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi, kauli hii ya REDET ni fedheha kubwa kwa Raisi kwani inamtuhumu kwamba hana uwezo wa kuyaona mapungufu ya watendaji anaowateua yeye. Kwamba Raisi mwenyewe hashtukii hii kejeli explains a lot kwamba may be it is true, and that's sad, really sad !

Ni ukweli kwamba machoni mwa Watanzania Rais Kikwete anaaminika, taasisi za kimataifa zinamuheshimu, kazi kwao watendaji wake ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya taifa la Tanzania.
Ni kweli anaaminika kwa asilimia 70% ya Watanzania aliowaita wafuata upepo na taasisi za kimataifa zinamheshimu kwani ni wabia wake wakubwa katika kugawana rasilimali za taifa kama peremende. Hizo changamoto anatakiwa akae chini akazikabili na si kuzunguka dunia kukwepa majukumu na maamuzi mazito likiwemo la kwawajibisha hao watendaji - the buck stops with the President, full stop.
 
Mafanikio yako kibao bro!!!

Kopo lake la umatonya limekusanya pesa nyingi sana kutoka kwa wahisani kupitia safari zake za kikazi nje ya nchi.

Vilevile kupitia safari zake za kikazi nje ameweza kutanganza utalii wa TZ mpaka watalii wanakuja kwetu haka kama hakuna umeme.

Amekuwa rais wa kwanza kutoka Africa kukutana na Rais Obama na alikuwa rais wa mwisho kutoka Africa kukutana na Rais mstaafu GW Bush.


Ame........
 
Ndo maana sishangai kusikia wapambe wake wakimridhisha kwa kumwambia Watanzania wana imani na Rais Kikwete ingawa hawana imani na serikali yake, which is RIDICULOUS to me!! How can it be possible wakati yeye ndo mkuu wa hiyo serikali????

Hilo nalo neno mkuu. Hawa ndo wanaoitwa Wapambe Nuksi.
 
La kujivunia ni kwamba yeye ni mtu anayependa kupigwa sana picha
 
La kujivunia kama lipo ni kwa mafisadi ambao wamegundua Kikwete anawaogopa kama ukoma.
 
Wakuu wana bodi,

Ni muda mrefu sijapost thread hapa,ila leo wakati tukiendelea kuisubiria Sikukua ya kuzaliwa kwa bwana Yesu Kristo nimeona ni vyema kuanza na thread hii.

Binafsi nampongeza mhe. Rais kwa kuweza kuliongoza taifa letu kwa miaka Minne,tumepitia mambo mengi ,msikusuko mingi na mambo kadha wa kadha.

Ila leo yakiwa yamepita masaa 48 ningependa tukumbushane ni yapi mazuri aliyofanya na yapi tunaona ni wa kati muafaka kumshauri mhe. Rais ayafanyie kazi kw akipindi cha mwaka mmoja ujao.

naomba tujadili..


Btw the Line,I smell something fishy on ATCL.Stay tuned!
 
MAZURI:-
- - - - -
1. Amehimarisha Uhusiano wa Tanzania na Nchi mbalimbali Duniani kutokana na ZIARA nyingi alizofanya nchi za Nje..

2. Amejenga majengo mengi yanayokusidiwa kuwa SHULE pindi Walimu watakapopatikana na Vifaa vya kufundishia.

3.
 
amesafiri sana kwa hili anatakiwa kupongezwa!Safari sizokuwa na matunda kwa asilimia kubwa ya watanzania,pia apongenzwe kwa MAISHA HOLA KWA ASILIMIA KUBWA YA WATANZANIA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…