Lipi ni chaguo (Option) sahihi kuhusu ujenzi wa nyumba ya Ghorofa moja

Aisee huu uongo wa wazi tani moja unajua bei gani? Je kila mchoro wa ghorofa unakula nondo za m15 ? Vituko hivi
Mkuu kama unaona nadanganya anza ujenzi utajua ukweli au uongo. Ila nakusihi usitumie "Fundi Maiko"
 
Mkuu kama unaona nadanganya anza ujenzi utajua ukweli au uongo. Ila nakusihi usitumie "Fundi Maiko"

Mkuu kama unaona nadanganya anza ujenzi utajua ukweli au uongo. Ila nakusihi usitumie "Fundi Maiko"
Tayari niko ktk sekta ya ujenzi muda mrefu tu, so hunidanganyi kitu! Mahesabu ya nondo ni kutokana na mchoro wako, maana kama tunanunua nondo kwa rejareja sh.21,000 mm12 ina maana kwa m15 tunapata nondo 714, tani moja ya mm12 zinakaa nondo 94, kwa hyo hapo ni tani 7.5 ghorofa ya kutumia tani 7 so mchezo ni kubwa sana, hapa tunazungumzia zile za kawaida kabisa, ambazo mpk tani 5 tani 4 unatumia, pia kumbuka michoro ni tofauti, pia ardhi inaweza fanya zitumike nondo nyingi au chache, kwa mfano anayejenga kwenye mfinyanzi tofauti na tifutifu, kuna mambo mengi mno, usikariri tu nondo M15, inaweza kuzidi au kupungua pia
 
Mkuu, hapa kila mtu anatoa uzoefu kwa namna alivyofanya ujenzi. Mimi sijasema hiyo experience yangu ndio Standard kwa kila mtu anayetaka kufanya ujenzi wa ghorofa. Nilichofanya ni kutahadharisha kuwa ujenzi wa ghorofa inabidi mhusika ajipange. Kwa hiyo, tutoe uzoefu wetu ili kuwasaidia ambao wanahitaji kufanya ujenzi.
 
Okay! Hata nyumba za chini ni kujipanga sana, maana kuna watu wanajenga nyumba za chini za gharama kubwa sana kuliko hizo ghorofa za makazi. Kitu kinachotoa uhalisia wa gharama ni ramani, kwa mtu ambaye anatamani ghorofa na bado hana pesa nyingi kivile anaweza kujenga ghorofa ndogo za mtindo wa loft type, hizi zinapunguza ukubwa wa slab, maana gharama kubwa ya ghorofa ni slab,unaweza pita Google ukaangalia hizo loft, au mfano ile ya jackline wolper ni mfano wake.
 
Na kwa jengo la kawaida la makazi la ghorofa moja nondo size gani ndo zinatakiwa kutumika kwenye slab? Nimesoma mahali kuwa inawezekana kutumia mm 12 kwa pamoja na 10 kwenye slab kwa ghorofa moja kwa maana ya kichanja cha juu na chini je hii ni sawa?

pia Countrywide, King Kong III hebu saidieni hapa
 
Mkuu kupanga ni kuchagua ,kama unataka kujenga na mpunga unao fresh ,jilipue tu.

Mimi nilipata kazi ya kujenga ghorofa la mteja wangu(Residential) ,nilimshauri atumie 25mm kwenye column ,Base 16mm ,Beam zote 16mm ,Slab 12mm juu na chini(kitanda) ,rings 8mm.

Ukijenga kama hivyo huna wasiwasi wa ghorofa kuporomoka.
 
mm 10 lazima ziwepo katika ghorofa nyingi, hizi hutumika kama rings! mm12 hutumika kwenye hicho kichanja, halafu ishu ya kichanja cha chini siyo lazima kwa kila ghorofa usikariri! Matumizi ya mm16 inategemea na ardhi na matumizi pia na mchoro ulivyo. Muulize Eng. Yoyote mm12 zinaweza kutumika bila shida kabisa kwa ghorofa za makazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…