Lipigie kura Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuweza kushinda kipengele cha ‘Best Government Page of the Year 2020’


Bila shaka kura yangu mmepata,

I know how hard you're trying to make things run.
 
Siwapigii kura, tumelipia mje kutuunganishia umeme home kwetu hata simu hampigi kutujuza chochote, naanzaje kupiga kura

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uku kusini umeme unasumbua sana kwa kukatika kila mara , mtwara ,masasi,lindi na ndanda kuanzia mchana hadi sasa hivi saa 5 kasoro usiku hui hakuna umeme
 
Yaani umeme wenu unaenda kasi kama nakoboa mahindi kumbe natumia matumizi ya kawaida kabisa.
Hela ya bando la kuwapigia kura napata wapi
 
RAYAN THE DON,
Uzuri ni kwamba unatype comment kitandani kwako huku simu ikiwa imepachikwa kwenye socket inayofyonza umeme toka kwenye nguzo ya Tanesco 🤣🤣🤣
Na laiti wangejua kama nimechomeka cm kwa charge.loh wangeleta mgao eneo hili.
🤣🤣🤣🤣
 
Mnajitahidi lakini bado Kuna mapungufu hasa kitengo Cha MITA na SURVEYOR. Bila rushwa ya kuanzia Elfu 70 Hadi laki na 40 mita haufungiwi kwa wakati na Surveyor bila Elfu 30 haji kusavey.
Kwa mengine Kama Customer Care, kusajili mita n.k mnajitahidi.👏👏👏
 
Wapuuzi na wapumbavu kabisa, huo muda mnaotafuta kura hapa mngeutumia kwenda kuboresha miundombinu ya umeme mitaani tungewaona mna maana, ninashangaa mnatafuta kura hapa nguzo za umeme zimeyumba na kuhatarisha maksha ya watu barabarani mkipigiwa simu mnajibu hovyo wanaowapa taarifa, nyaya za umeme zimetepeta 2 metres from the ground mkiambiwa mnasema waliofanya kazi ni engineeres waliosomea tusiwafundishe kazi, kitengo cha customer care ni cha hovyo na response yenu ni 0 grade, kuna maeneo mengi kabisa yaliyopimwa viwanja vipya mmesimika nguzo za umeme kwenye barabara wakati mpo kwenye miji ambapo Halimashauri za wilaya na miji ndipo zilipo, mnashindwa nini kwenda kuomba ramani ili usimikaji wa nguzo ufuate michoro? Nashangaa mnatafuta kura wakati mkishauriwa mnasema siyo kazi yetu. Hopeless and poor Co of the year!!
 
Acheni kebehi, Mkipiga kura waajiriwa wote mnaweza kushinda pia. Sio lazima tupige kura sisi maana ntapiga kura kwa mazuri yapi !? Kwa huduma zipi !? Hata mkishinda itakuwa ni ushindi batili tuu maana hamna vigezo kabisa.


Mkuu umegusia jambo la muhimu hapa, hawa Tanesco wangetuambia tuwapigie kura watendaji wa hovyo wanaolisababishia shirika hasara kwa kutoa huduma chini ya viwango, kura hizo zingewasaidia kuongeza tija kama shirika. Pili wangeonekana wana akili na pia wanajitambua wangekuwa wanafanyia kazi kila malalamiko yanayotolewa na wadau, kuna sehemu nilipita nikapiga picha za nguzo na waya zilizodondoka nikawawekea hapa JF pamoja na GPS readings za eno husika, wakang'ang'ania niwape namba yangu ya simu ndipo wakarekebishe tatizo, imagine watendaji wa namna hiyo leo wanaomba kupigiwa kura!!!
 
Kuna taarifa kwa umma mmeitoa hapa hadi kichefuchefu, halafu mnakuja kutafuta kura humu....
 
Nimejenga kibanda changu manispaa kabisa mwaka wa 5 sasa umeme haujafika!!! Walileta nguzo wakazilundika zinamaliza mwaka, sasa sijui napigaje hiyo kura[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,hao ndio typical Tanzanians,aibu hawana. Yaani mtu anaomba apigiwe kura si kwa ubora wa hiyo page ambao Watanzania wanaotembelea wameuona,bali ni kwa sababu ya kutaka kushinda tu.
Yaani huu ndio mfano hai wa watumishi wengi wa mashirika,taasisi,mamlaka,makampuni na idara za umma kuwa wao wanafanya kazi ili waonekane wamefanya kazi,na si kufanya kazi kwa mujibu wa matakwa ya kazi zao kwa ustawi wa taasisi zao na Taifa kwa ujumla.
Hawa Tanesco walitakiwa wawahabarishe wananchi kuhusu huo ukurasa wao,wautembelee na ndipo huko ndani wangekutana na hiyo ya kupiga kura,na sio kuwaomba wapigiwe kura.
Uchaguzi wa Tanzania hauna tofauti na wanachokifanya hawa Tanesco.
Ila kuna watu wana moyo. Serious umekuja kuomba kura humu?
 
Boresheni huduma zenu kwenye kusambaza umeme kule kwenye mradi wa REA. Kuna sehemu mmepeleka nguzo zimerundikwa pale kwa mda mrefu lakini hamna kinachoendelea,
TANESCO You are not serious
 
Kura yangu nimeiweka Brela wakuu..

~~Kitakachokupa ushindi ni juhudi zako~~
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…