The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Vyama vya upinzani tunapokua tunalilia demokrasia hapa Tanzania huwa tuna maana gani iwapo kwenye vyama vyetu tu hatuna demokrasia.
Leo viongozi wa vyama vya siasa Tanzania wana combined leadership period of more than 50 years. Kama nilivyoeleza kwenye kichwa cha mada hapo juu, Lipumba alipewa uwenyekiti wa CUF mwaka 1995, Mbowe alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA mwaka 2004, Zitto alijiteua kuwa kiongozi mkuu na mshauri mkuu (Supreme Leader and Chief Advisor) wa ATC Wazalendo mwaka 2014. Jumla ni miaka 50 na ushee. Sijataka kuunganisha miaka ya Rungwe, Mbatia, Mrema na wengine.
Viongozi hao wao kuwa viongozi wa maisha kwenye vyama vyao ni sawa ila CCM ilichaguliwa na wanachi kuendelea kutawala nchi hii inakua nongwa. Unajiuliza, sasa kama maana demokrasia ni kuchaguana na kuchaguliwa, ndio maana hao viongozi wanachaguliwa na wanachama wao, (Zitto Hachaguliwi wala hapigiwi kura) kuendelea kua viongozi, kwa nini watanzania wakiichagua CCM kuendelea kuwatumikia inakua nongwa?
Huwa najiuliza hivi hawa jamaa kweli wana nia njema na demokrasia ya nchi hii? Mfano Zitto amejipa cheo kisichokua na uchaguzi, yeye ndie mkuu wa chama na mshauri mkuu wa chama, hachaguliwi wala hapigiwi kura, uchaguzi ukiitwa wanachaguliwa wengine ila sio yeye Supreme Leader lakini at the same time CCM wakichaguliwa(angalau basi uchaguzi unakuwepo) inakua nongwa.
Binafsi naamini kuyumba kwa demokrasia nchi hii kunachangiwa sana na viongozi wa vyama vyetu hivi vya siasa kua na tamaa ya uongozi na kutokua ama kuruhusu demokrasia kwenye vyama vyao huku wakitaka demokrasia ya kweli nchini.
Vyama vya siasa, onyesheni demokrasia kwa vitendo ndani ya vyama vyenu. Acheni kuendesha vyama vya siasa ki gangstar ama mafia style kwamba boss mpya atapatikana baada ya kifo cha boss aliekuwepo.