PISTO LERO
JF-Expert Member
- Mar 8, 2011
- 2,819
- 1,455
Chama cha Wananchi (CUF), kimeitaka Serikali kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015, kwa kuwa inahitaji muda wa kuijadili na si suala la kukurupuka.
Akifungua semina ya Baraza la Katiba ya CUF, Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema kunahitajika utaratibu mbadala wa kuingia kwenye uchaguzi mkuu katika hali ya amani na utulivu.
Alisema ili uchaguzi huo uwe huru na wa haki mchakato wa Katiba Mpya inayotokana na muafaka wa kitaifa uweze kukamilishwa baada ya uchaguzi mkuu.
"Ili kupata Katiba ambayo ni muafaka wa kitaifa katika mambo ya utawala, uchumi na siasa inahitaji muda hasa katika taifa lenye Muungano wa nchi mbili ambao kwa muda mrefu umekabiliwa na kero nyingi, huwezi kupata mwafaka wa kitaifa fastafasta," alisema Profesa Lipumba.
Aliipongeza Tume ya Jaji Warioba, kwa kufanya kazi kwa ujasiri mkubwa hasa ikizingatiwa pendekezo kuu la mfumo wa serikali tatu unakinzana na msimamo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)