Mkuu liquid assets ziko za aina 3. Kwanza ni fixed deposits ama amana za akiba za benki. Hii unaweka hela yako bank kwa muda flani, mnakubaliana riba wamayokulipa. Hii riba yake inatofautiana kwa benki na benki na kwa kiasi ulichonacho. Wewe ukienda na 2m riba utakayipewa sio sawa na atakaeenda na 500m. Mara nyingi riba zake ni ndogo kama una kiasi kidogo cha pesa.
Liquid assets nyingine ni hisa, hati fungani za serikali ama za makampuni binafsi. Tukianza hisa, hizi wanauza soko la hisa la Dar es Salaam. Hii unanunua sehemu ya umiliki wa kampuni flani mfano crdb, kwa maana kwamba thamani ya crdb ikipanda basi na thamani ya hela yako inapanda, zikishuka na thamani ya hela yako inashuka na unaweza kufilisika kabisa. Kwa Tanzania bado soko la hisa ni changa sana mimi binafsi sishauri mtu labda kama una mabilioni ya shilingi.
Kwenye hati fungani, iwe ya serikali ama ya kampuni binafsi hii muuzaji, ama mkopaji anaweka dau la riba, kwamba nataka unikopeshe kwa 12%. Ni wewe uamue ukopeshe ama uache., take it or leave it,haina majadiliano. Ukiamua kuikopesha serikali ama shirika basi unakua unalipwa riba kwa robo mwaka ama nusu mwaka. Yaani kila baada ya miezi 3 wakakuwekea riba yako ama kila baada ya miezi 6.
Liquid assets ta tatu ni collective investment scheme (CIS) ambapo kwa Tanzania ziko 2, ya kwanza ni mifuko ya hifadhi ya jamii. Hii ni kwa watumishi na wanachama. Hii kwa wanachama ni lazima. Ya pili ni CIS ya hiyari kama UTT, hii ni kwamba unawapelekea hela yako wataalam wafanye uwekezaji kwa niaba yako, wao ndio watafte fursa za kuwekeza kisha wawekeze hela yako halafu faida inayopatikana mnagawana riba. Pia hii nadhani wanagawa riba kwa mwezi, robo mwaka na kuendelea.
So ukielewa aina ya liquid assets ndio utaelewa wapi kuna faida kubwa. Obvious CIS na hati fungani zina faida kwa Tanzania kuliko fixed deposits unless una hela nyingi sana hivyo uwe na bargaining power kubwa.