Lishe kwa mtoto - Unampikia nini mtoto wako (miezi 6-12)



Nitajaribu na hii ntaleta majibu
 


Usemavyo ni kweli kabisa
 
....Daaah!! Mwanetu ana miezi sita sasa hivi, anapenda zaidi kunyonya maziwa ya Mama ake na sio mpenzi sana wa vyakula nadhani hii thread itasaidia kujua vyakula vya kumpa mtoto wetu kipenzi.

Kesho mapema sana inabidi wife afanye ziara kwenye uzi huu.

Shukrani kwa muanzishaji wa uzi huu na wachangiaji wote.
 
......mwanangu yupo 4 yrs now,lakini alipokuwa na umri wa miezi 6 -12 menu yake kubwa ilikuwa asubuhi nilikuwa nampa avocado nusu na ndizi nusu. Nachanganya na mtindi na rice cereal vijiko 2. Anashushia na maziwa 6 ounces.

Aisee! Kameshakuwa kakubwa hivyo mara hii?

Time flies.
 

Hizo menu tunafanana vyakula unavyompa hata wa kwangu nampa ila tu sio mlaji...

Kuhusu tv wakati wa kula mie ndio naona huwa anakula zaidi mana anapenda tv ila mda mwengine ana concetrate sana
 


Ahsante sana na wewe kwa kuchangia kisses kwa mtoto wetu
 
Tatizo watu wakiwa watoto hawapati virutubisho tosha.

Wakiwa wakubwa wanadata.

Mtoto mdogo unampa uji chukuchuku.

Topic muhimu kweli. Ila basi tu.

Hahaha Kiranga una maneno!!!!
 
Last edited by a moderator:
Pretty hata watoto wa miezi 7 na kurndelea wanaweza anza kujifunza kula wenyewe ila ni kuhakikusha tu vyakula ni soft kama karot unachemsha au ku steam ili visiwakae kooni....

Hata avocado ukikata pieces ndogo ndogo anakula mwenyewe na vyengine kama ndizi n.k...

Ujanja huu apa chini

Kwa vile kushika wenyewe vyakula vinateleza mfano ndizi basi unatakiwa uvipakae unga wa cereal ili waweze kushika vizuri na kula
 
Last edited by a moderator:
Ila tv sio nzuri kwa mtoto shosti. Inamzuia kujiengage na watu na inaweza kumchelewesha kuongea.

As part of the deal, unaweza kuiwasha mara chache wakati anakula. Jaribu kubadili mazingira kama kutoka nje, balcony, chumbani, jikoni? Na hichi kiti chake kisiwe kama adhabu basi mama mkwe, lol
Hizo menu tunafanana vyakula unavyompa hata wa kwangu nampa ila tu sio mlaji...

Kuhusu tv wakati wa kula mie ndio naona huwa anakula zaidi mana anapenda tv ila mda mwengine ana concetrate sana
 
Hapo kwenye snacks shosti, badala ya cookies hebu mpe something healthy kama kipande cha chungwa, embe ama nanasi. Cookies haina virutubisho anavyohitaji. Tusisahau soda is a no ~no

Nakubaliana nawe kuhusu kutolazimishana na kuzima tv.

Wakati mwingine kuonja chakula cha mtoto ni muhimu sana. Kuna mtu nilikuta anamkaba mwanae anywe mazima, kumbe maziwa yenyewe ni maji matupu and tasteless
 
mwanangu ten months hapendi lishe (uji)anakula uji wa dona naweka maziwa au blu band hapendi sukari,anapenda machungwa sana
mtori anapenda na ugali mlaini
juice ya chungwa na maparachichi ndo vyakula vyake
 

Hio kubadilisha mazingira nafanya sana muda mwengine nampakata anakula vizuri ujue hapo ntapakwa chakula mpaka machoni lol siku hizi nae alichoshika na mie nalishwa lol
 

Hapa kwenye maziwa inatakiwa utumie formula au maziwa ya mama ila tu wakati umeshaepua
 
Last edited by a moderator:
mwanangu ten months hapendi lishe (uji)anakula uji wa dona naweka maziwa au blu band hapendi sukari,anapenda machungwa sana
mtori anapenda na ugali mlaini
juice ya chungwa na maparachichi ndo vyakula vyake


Hata wa kwangu anapenda machungwa kuna watoto wanapendea zaidi vya chumvi kuliko vya sukari ndio mana wengi hawapendi uji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…