Hapo kwenye snacks shosti, badala ya cookies hebu mpe something healthy kama kipande cha chungwa, embe ama nanasi. Cookies haina virutubisho anavyohitaji. Tusisahau soda is a no ~no
Nakubaliana nawe kuhusu kutolazimishana na kuzima tv.
Wakati mwingine kuonja chakula cha mtoto ni muhimu sana. Kuna mtu nilikuta anamkaba mwanae anywe mazima, kumbe maziwa yenyewe ni maji matupu and tasteless
Hata wa kwangu anapenda machungwa kuna watoto wanapendea zaidi vya chumvi kuliko vya sukari ndio mana wengi hawapendi uji
Mi mtoto wangu asb anapata uji wa ulezi.
Mahitaji
.ulezi
. Karanga
. Mchele
Chambua karanga vizuri kutoa zilizooza kisha osha vizuri ulezi na mchele mpk mchanga wote uishe kisha anika juani hlafu badae peleka mashineni kusaga ili kupata unga wenyewe.
NOTE : mchanganyiko wa ulezi,karanga na mchele uzingatie ratio.
Baada ya kupata unga,huwa namtengenezea uji kwa kutumia maziwa kisha mchana anapata ndizi au viazi mviringo vilivyopndwa vikiwa accompanied na mboga mboga. Akimaliza kula anapata maji kisha badae akipata njaa jioni anapata maziwa.
Ila kwenye kumpa chakula sasa ni vita,ni muoga sn na muda wote anajua ni dawa hivyo kwa mara ya kwanza ni lazima kumkaba ili aonje na akishaonja tu anaanza kula bila shida.
Oooph naenjoy kupata maujanja haya ya afya ya watoto yan hapa ni full notes kwa kila kitu maana nina baby boy wa miezi 5 hapa so nasubir tu afike miezi 6 tuanze kumpata menu..
Sina mtoto lkn nimejifunza mengi,,, asanteni wachangiaji wenye mapya leteni tujifunze
Mi wangu anapenda sn tikiti maji,loh na vile sasa ana vimeno sita yaan ni shida. Lkn namshukru Mungu kwakuwa mwanangu sio msumbufu sn ktk suala zima la kula.
Kuna madokta wanasrma its ok kumpa chakula mtoto kuanzia miezi minne ila viwe vyepesi sana mfano apple and carrot puree au uji mwepesi ila maamuzi ni wewe mlezi mwenyewe
Mkuu Farkhina asante ila mbona wengi na hata ninapomsindikiza wife kriniki wanasema lazima awe na miezi 6 ndo nimpe chakula kingne cha ziada ya maziwa ya mama?
mara moja moja unamandalia na safari baridi kama analia lia sana!!
Wow maashaAllah ana umri gani? Wangu miezi 8 na nusu ila hajaanza kutoa meno
Kachelewa kidogo, wa kike au kiume?
Ndio wanatafautiana mawazo ila muhimu kufuata ushauria wao mimi binafsi nlishauriwa na dokta wake nianze kumpa uji na puree na vyakula laini alitimiza miezi 4 na ilikua vizuri tu alikua ok na hakuwa akipata tabu choo ila tu ana chagua sana vyakula
mwanangu ten months hapendi lishe (uji)anakula uji wa dona naweka maziwa au blu band hapendi sukari,anapenda machungwa sana
mtori anapenda na ugali mlaini
juice ya chungwa na maparachichi ndo vyakula vyake