Lissu acha kushambulia watu, nadi sera zako watu wakuelewe

Lissu acha kushambulia watu, nadi sera zako watu wakuelewe

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
17,079
Reaction score
12,312
Nimemsikiliza Lissu akimshambulia Deo Mwanyika, nimesikitika sana, nimejiuliza huyu mtu anayeitwa Lissu anamatatizo gani? Sote tunajua Deo alipata shida kwa kudhaniwa anauhusiano na Lissu. Sasa bado tu anamwandama, hivi hamna namna Lissu akafanya kampeni bila kutuhumu mtu? Siasa gani za hovyo anazofanya?

Lissu huyuhuyu aliyokuwa bungeni aliwashambulia kwa maneno makali Prof Tibaijuka Anko Rugemarila na Askofu Kilaini bado tu anaendeleza haya mambo? Akiwa Rais atakuwa mtu wa namna gani?
 
Sisi watu ndo tunawapenda watu wanaowashambulia na kuwaponda wale wanaotudhalilisha na kutunyanyasa!

Amefanya homework yake. Anaongea kile watu wanataka kusikia.

Hizo ilani zenu ni changa la macho. Mnazitangaza mkishapata mnafanya yasiyokuwemo.

Msiyemtaka karudi. Ngoja awanyooshe mnyooke.

NB: Safari hii hakuna kumuachia MUNGU. Mambo yetu tunamalizana kivyetu vyetu.
 
Umemsikiliza hadi mwisho maana amenadi sera barabara sasa ulitaka asiseme kuwa Mwanyika hana sifa ya kuwa mbunge kwa mujibu wa sheria za Tanzania wakati ni kweli na kwanini amepitishwa kinyume na sheria ya uchaguzi.
 
Chadema chama cha wambeya wa kusema watu, bila umbeya chadema haipo
 
Adui anajifanya anakushauri mbinu za kivita eti ili ushinde?hakuna mbinu hyoo katka mapambano..Lissu amechora mbinu za kpambana juu ya uhuru haki na maendeleo ya watu. Na jinsi ya kufikia hapo ameweka kwenye ubongo wake. TWENDE LISSU KAMA SI LEO BASI NI Lini?? !!Tanzania ni yetu sote si kikundi cha watu :
 
Tangu alivyoanza kampeni zake ni hayo tu ndo ya muhimu uliyoyasikia kwake! Tujitahidi kuacha chuki binafsi tuikombowe nchi yetu! Tukumbuke katika siasa lolote linaweza kutamkwa kutemeana na jinsi gani mhusika analijengea hoja inayoshikika!
 
Moja ya wajibu muhimu kwa serikali yoyote mpya ni kusahihisha na kukomesha madudu ya serikali iliyopita. Vyama vya upinzani kueleza madudu ya serikali iliyopo kwa ahadi ya kwenda kuyashughulikia nayo ni Sera isiyoepukika.

Mfano Mwalimu Nyerere mwaka 1995 katika hotuba yake ya mustkabali wa taifa na uongozi wetu alitamka na alikosoa madudu yaliyofanywa na utawala was Ally Hassan Mwinyi na kutoa rai kuwa raisi ajaye akayashughulikie.
 
Yuda iskariote hawezi kuwa raisi haitotokea kamwe na yeye binafsi anajua,na ndio maana anazidi kudata na sonoma ina zidi kumtafuna
 
Back
Top Bottom