KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,181
- 17,187
Bila shaka wakati huu Bashiru anatafuta kila njia ya kuhakikisha kwamba Lissu hatasimama kumkabili Magufuli.Atoe manifesto ili Bashiru akopi
Hebu CHADEMA watazame hatua zilizosalia mbele, ambazo hawa watu wanapanga kuzitumia kumzuia au kumchelewesha maksudi Lissu kuwa mgombea wa chama chao.
Hebu angalia- CHADEMA wakishamteua mgombea wao (Lissu), nani tena aliye na uwezo wa kmwekea mizengwe asiwe mgombea?
Mapingamizi yakiwekwa, ni nani anashughulikia kutoa uamzi wa hayo mapingamizi.
Anao uwezo wa kumchelewesha maksudi mgombea, kwa kupoteza muda, kwa mfano.
Mambo haya inapashwa CHADEMA wasimame kidete kabisa kuyakabili. Bila shaka CCM watafurahi sana kuwapoteza lengo CHADEMA, hata kutamani wajitoe kwenye uchaguzi!
Huu ni wakati muhimu sana kwa CHADEMA kusimama imara. Chaguo lao ni lazima walisimamie kidete, isiwe tu geleshagelesha ya hapa na pale.