Lissu aendelea kummbana shahidi mahakamani -16.10.2025

CHRC

Senior Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
174
Reaction score
229
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Leo Oktoba 16, 2025

Jana tuliishia part 105 so leo tunaendelea na-;

Part 106

Muda huu ni saa tatu asubuhi.

Tumefika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es salaam.

Hali ya Mahakama ni nzuri.

Tunawashuhudia Waandishi wakichukua picha mgando na mnato kwa watu mbalimbali waliopo hapa Mahakamani.

Askari Magereza wale wa Kikosi Maalum yaani KM wako hapa ndani ya Chumba cha Mahakama wanazunguka zunguka kama wanakagua lindo vile.

Wasaidizi wawili wa Majaji tunawaona wako hapo mbele, Mwanamke mmoja na Mwanaume Mmoja kwa wasiofahamu hawa wanaoitwa Wasaidizi wa Majaji kitaaluma ni Mahakimu Wakazi.

Cheo chao ni sawa na Mahakimu waliopo Kisutu pale hawa hufanya kazi ya kuwasaidia majukumu ya kufanya research mbalimbali za masuala ya kisheria.

Wameingia hapa Majaji watatu kama kawaida ambao ni Jaji Dunstan Ndunguru, James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde. Wakiwa kwenye magauni yao nasikia yanaitwa majoho mekundu.

Limesomwa shauri hapa na karani na amesimama Renatus Mkude Wakili Mkuu wa Serikali na ametambulisha wenzake muda huu, anasema upande wa Jamhuri wako tayari.

Mhe. Lissu ameulizwa yuko tayari na anaomba akumbushwe shahidi aliishia wapi kujibu maswali yake.

Amekumbushwa anasema anaomba aanze sasa.

Mhe. Lissu: Shahidi umeamka salama?

Kaaya: Nimeamka salama Mheshimiwa Lissu.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ulieleza kwamba fomu No. 145 kwamba haikusomwa wakati wa committal Kisutu?

Kaaya: Sikuwepo Kisutu.

Mhe. Lissu: Je umeileta hapa Mahakamani?

Kaaya: Sijaileta pia.

Mhe. Lissu: Sasa turudi tulipoishia jana. Maelezo yako Polisi ulitoa maneno mengi ikiwemo "Baadhi ya maneno mengine aliyotamka Rais alitoa maelekezo kuwa hakikisheni wapinzani hawaendi kokote....."

Naomba majaji shahidi apewe Exhibit D1 ili twende pamoja.

Sasa shahidi baada ya kelele nyingi za wapinzani kuenguliwa akiwemo Nchimbi alisema mambo kuhusu uchaguzi.

Je unafahamu Mchengerwa Waziri wa Tamisemi alisema wakikata rufaa wagombea walioenguliwa watarudishwa?

Kaaya: Sikumbuki.

Mhe. Lissu: je unafahamu Mchengerwa aliongeza muda wa rufaa ili watu wakate rufaa?

Kaaya: Sikumbuki.

Mhe. Lissu: Unafahamu wagombea angalau wa Chadema kwa maelefu walikata rufaa ndani ya huo muda wa rufaa ambao uliongezwa na Mchengerwa?

Kaaya: Sikumbuki.

Mhe. Lissu: Rufaa za Uchaguzi wa serikali za mitaa zinasikilizwa na Kamati za Wilaya?

Kaaya: Sina kumbukumbu.

Mhe. Lissu: Je unafahamu wenyeviti wa kamati za rufaa za Wilaya ni Makatibu tawala wa Wilaya ambao ni wateule wa Rais?

Kaaya: Sina Uhakika.

Mhe. Lissu: wote waliokata rufaa waliorudishwa hawafiki hata 10?

Kaaya: Hilo silifahamu.

Mhe. Lissu: Ila maneno yangu unasema ya uongo kuhusu uchaguzi wakati wewe kila kitu hujui?

Kaaya: Kimya.

Mhe. Lissu: Sasa watu wanaosimamia uchaguzi wote wa serikali za mitaa ni watu wa Rais kama nilivyokuonyesha mimi nakosea wapi?

Kaaya: Rais akishachaguliwa anafanya kazi kwa niaba ya Serikali na sio Chama chake.

Mhe. Lissu: Kwahiyo akikosea na mimi nikimpinga nikisema anafanya mambo ya hovyo kuengua watu wa Chadema nakosea wapi? Hapo anakuwa ameacha kuwa mwana CCM?

Kaaya: Haachi kuwa Mwanaccm.

Mhe. Lissu: Sasa wewe fundi wa Viyoyozi hebu tuambie kazi za Mwenyekiti wa CCM anazifanya nani kipindi akiwa Rais?

Kaaya: Anaendelea kuzifanya mwenyewe.

Mhe. Lissu: unafahamu zaidi ya asilimia 98 ya wenyeviti wa mitaa waliochaguliwa ni wa CCM?

Kaaya: Sifahamu.

Mhe. Lissu: Je unafahamu kwamba mwaka 2014 kwenye Uchaguzi wa Vijiji na mitaa ambao wagombea wa upinzani hawakuenguliwa walipata asilimia 33 ya viti vyote vya serikali za mitaa?

Kaaya: Sina Takwimu hizo.

Mhe. Lissu: Je unafahamu mwaka 2014 asilimia zaidi ya 20 walienda kwa upinzani ulienda kwa upinzani?

Kaaya: Hilo nilisikia.

Mhe. Lissu: Uchaguzi wa 2019 ambao wagombea walienguliwa wa upinzani CCM ilipata wenyeviti wa mitaa 100%?

Kaaya: Sikumbuki.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 107

Mhe. Lissu: Uchaguzi wa 2019 Serikali za mitaa CCM ilipata asilimia 98 ya wenyeviti wa Vijiji?

Kaaya: Sina Kumbukumbu

Mhe. Lissu: Je unafahamu uchaguzi mkuu wa 2020 ndio ulikuwa na wagombea wengi wa ubunge kuenguliwa kuliko chaguzi yoyote toka uchaguzi uanze?

Kaaya: Ukikosa sifa unaenguliwa tu.

Mhe. Lissu: Wewe ni fundi viyoyozi mambo ya sifa unayajulia wapi? Haya jibu swali langu.

Kaaya: Sikuwahi kufanya huo utafiti.

Mhe.Lissu: Kwamba wagombea 63 kati ya 244 walienguliwa wa ubunge?

Kaaya: Sijawahi kuwa mwanaCHADEMA.

Mhe. Lissu : Hata magazeti husomi ndugu yangu?

Kaaya: Sifahamu mimi.

Mhe. Lissu: wagombea wa udiwani 1150 kati ya 3900 walienguliwa mwaka 2020 unafahamu?

Kaaya: Sina takwimu mimi. Sijui.

Mhe. Lissu: Wagombea wa CCM 872 wa udiwani walipita bila kupingwa kutokana na kuenguliwa kwa wapinzani kwa mujibu wa taarifa rasmi ya tume?

Kaaya: Sijawahi kuisoma hiyo taarifa.

Kaaya: Waheshimiwa Majaji mimi nilisikia wagombea walipita bila kupingwa lakini idadi ya 28 sikumbuki.

Mhe. Lissu: Mimi nasoma ndio maana najua walikuwa 28 wewe unatengeneza Viyoyozi.

Kaaya: Mimi ni askari Polisi sio fundi viyoyozi.

Mhe. Lissu: Kwahiyo hukusema hapa kuwa umesomea Air Condition? wewe ndio ulituambia haya mambo ya viyoyozi au nani alituletea?

Kaaya: Nilisema basi yaishe.

Mhe. Lissu: Kwahiyo toka 1995 hakuna mgombea hata mmoja wa CCM amewahi kuenguliwa kwa kukosa sifa?

Kaaya: Unaweza kuwa sahihi.

Mhe. Lissu: Waangalizi wa AU wa uchaguzi umewahi kuwasikia? AU election expert mission walitoa ripoti inayolalamikia kuenguliwa kwa wapinzani?

Kaaya: Nimewasikia lakini ripoti sikuisikia.

Mhe. Lissu: Je jumuiya ya Ulaya walituma EU election observation mission walituma waangalizi pia na kulalamikia kuenguliwa kwa wapinzani?

Kaaya: Silijui kiukweli.

Mhe. Lissu: Ongeza sauti basi unamnong'oneza nani?

Kaaya: Sijui

Mhe. Lissu: Je waangalizi kutoka jumuiya ya madola ambao ni Commonwealth observer group walitoa ripoti kulalamikia vitendo vya kuengua wapinzani?

Kaaya: Kweli.

Mhe. Lissu: Watizamaji wa Umoja wa Afrika walipendekeza kuwa serikali iondoe vikwazo vya kiuchaguzi kabla ya uchaguzi wa 2025?

Kaaya: Sina uhakika kabisa.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu mashirika ya kiraia walituma waangalizi Tanzania?

Kaaya: Walitumwa kwenda wapi?

Mhe. Lissu: Kuja Tanzania.

Kaaya: Basi msemaji wa Serikali anazo hizo taarifa.

Mhe. Lissu: Msemaji wa Serikali ni shahidi namba ngapi?

Kaaya: Sijui

Mhe. Lissu: Shahidi hapa ni wewe jibu swali langu.

Kaaya: Sijui.

Mhe. Lissu: Sasa unajua watizamaji wa ndani pia wa Uchaguzi huu wapo nao wamekuwa wakitizama uchaguzi miaka yote wanaitwa Tanzania Election Monitoring Committee ikijumuisha viongozi wa dini na chuo kikuu cha Dar es salaam (TEMCO)?

Kaaya: Ni sahihi.

Mhe. Lissu: Je umewahi kusoma ripoti ya hao TEMCO hata moja?

Kaaya: Sijawahi kuziona hata kwa sura wala kuzisikia.

Mhe.Lissu: so huwezi kufahamu mashirika haya kuwa nayo yamelalamikiwa mfumo wa uchaguzi na kuondolewa kwa wapinzani?

Kaaya: Sifahamu na sio majukumu yangu.

Mhe. Lissu: Sasa mimi kulalamikia uchaguzi unasema nasema uongo kwanini wakati huna unalojua?

Kaaya: Kusema Rais ndio niliona kuna shida.

Mhe.Lissu: Uchaguzi wa mwaka huu mgombea Urais wa ACT Wazalendo ameenguliwa na Tume ya Uchaguzi?

Kaaya: Hajakidhi vigezo.

Mhe. Lissu: Kaenguliwa na tume au hajaenguliwa?

Kaaya: Kaenguliwa na tume kweli.

Mhe. Lissu: Je Mwenyekiti wa Tume na Majaji waliokataa kesi jana wote si wateuliwa wa Rais?

Kaaya: Ni kweli.

Mhe. Lissu: sasa ulitegemea Mpina apate haki kutoka wapi kama wote aliokuwa anategemea wampe haki ni wateule wa Rais?

Kaaya: Ingekuwa ngumu sana kiukweli.

Part 108 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.

Part 107 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 108.

Mhe. Lissu: Jana ulisema hujasoma hati ya mashitaka vipi leo umeisoma?

Kaaya: Nimeisoma.

Mhe. Lissu: anamsomea hati ya mashitaka yote.

Sasa nataka useme kuhusu tuhuma nilidhihirisha nia kwa kitendo cha kusema na kuchapisha.

Swali langu.

Hayo maneno yapo kwenye video clip?

Kaaya: Ni sahihi.

Mhe. Lissu: Tukitaka kujua maana ya Kuchapisha tuangalie Sheria ya mitandaoni yaani Cyber Crime Act?

Kaaya: Tunaweza kupata kupitia sheria ya makosa ya mtandaoni na sheria zingine.

Mhe. Lissu: Zingine ni zipi mimi najua moja.

Kaaya: kama zipo

Mhe. Lissu: mimi sizijui wewe niambie ni zipi?

Kaaya: Nikizijua nitakwambia.

Mhe. Lissu: Sasa mimi sihangaiki na huo umbea wewe soma Section 3 ya hiyo Sheria ili usitupotezee muda. Je kwenye hiyo Sect 3 kuna maana ya neno uttering yaani kusema?

Kaaya: kuna neno hapa offering in other way

Mhe. Lissu: We afande unasikia kweli? Nimesema neno uttering sio offering

Kaaya: Uttering halipo hapa.

Mhe. Lissu: Tafuta neno lingine ambalo ni publishing

Kaaya: Lipo means distributing, transmitting, disseminating, circulating, delivering, exhibiting, exchanging, barter, printing, copying, selling,…

Mhe. Lissu: Waeleze majaji sasa hiyo video iliyoko kwenye mtandao wa Jambo Tv nani ameiweka huko?

Kaaya: wewe ndio uliiweka.

Mhe. Lissu: je mimi nilikuwa na password yaani nywila.

Kaaya: Sina Uhakika.

Mhe. Lissu: Nani aliyeisambaza?

Kaaya: Wewe kupitia Jambo TV.

Mhe. Lissu: Nani aliyedisseminate?

Kaaya: Wewe.

Mhe. Lissu: Nani aliyecirculate?

Kaaya: wewe kupitia Jambo TV.

Mhe. Lissu: Nani aliyeonyesha?

Kaaya: Jambo TV ndio alionyesha.

Mhe.. Lissu: Nani aliyefanya Exchange. Kutoa Jambo kwenda Clouds kwenda The Chanzo kwenda vyombo vingine?

Kaaya: Sifahamu.

Mhe. Lissu: Nani aliyefanya printing and bartering?

Kaaya: Sifahamu.

Mhe. Lissu: Copying je?

Kaaya: sijui.

Mhe.Lissu: je kuna malipo hawa watu wa youtube huwalipa hao wanaorusha haya video?

Kaaya: Nasikia ila sijui.

Mhe. Lissu: sasa nani aliyepata pesa za viewers wa hizo videos?

Kaaya: sijui.

Mhe. Lissu: Sasa niliwezaje kuingia kwenye hizo system za Jambo Tv na kusambaza?

Kaaya: Hilo sifahamu kabisa.

Mhe.Lissu: Kama hufahamu kama nilikuwa na uwezo au sina unawezaje kusema niliingia na kufanya. Tuseme ukweli wa Mungu. Hebu tueleze.

Kaaya: Lengo lake kuita waandishi ilikuwa ni ili wasambaze.

Mhe. Lissu: Unakumbuka nilikuuliza idadi ya watu waliotazama na kusema wamecomment?

Kaaya: Nakumbuka.

Mhe. Lissu: Je umepata wasaa wa kutizama tena?

Kaaya: Sijatizama.

Mhe. Lissu: Je bado ni msimamo wako kuwa hiyo video ina comments 300 tu?

Kaaya: niko sahihi.

Mhe. Lissu: Je sasa umetoa kielelezo chochote kuthibitisha idadi hiyo ya comments 300. Sina maswali zaidi na shahidi huyu.

Kaaya: Sijatoa kabisa.

Mh. Lissu sina swali lingine.

Anasimama Katuga kwa ajili ya Re Examination kwa shahidi.

Majaji wanaandika kidogo.

Katuga: Nikupe Pole kwa maswali mengi ya siku nyingi.

Sasa relax umesharelax tayari?

Kaaya: sawa

Katuga: Uliulizwa kuhusu ajira yako na ulianza lini haswaa.

Kaaya: Ukiteuliwa kuanza mafunzo ya Polisi ndio ajira yako inakuwa imeanza hapohapo. Ukishahitimu ndio unaweza kuanza kutekeleza majukumu yako.

Katuga: Sasa ifafanuliwe Mahakama.

Kaaya: Nilipoteuliwa ndio nilianza kuwa askari na nilipotamka mwaka 2006 ndio mwaka niliohitimu mafunzo na kuanza kazi rasmi.

Katuga: Yale maelezo yako ya Polisi uliulizwa mambo mengi sana kuhusu hili limo na hili halimo.

Kaaya: Nilikuwa naelezea substance ya ushahidi wangu lakini ushahidi niliouwasilisha nilikuwa naelezea zaidi kuhusu maelezo niliyokwisha aandika.

Nilichokifanya ni kuelezea kwa upana kile nilichokuwa nimekiandika kwenye maelezo yangu.

Part 109 itaendelea kwenye post inayofuata.

Part 109

Katuga: Uliulizwa kuhusu suala la Notebook kama hiyo notebook umeileta. Je kwanini hujaileta.

Lissu anasimama napinga hilo swali la sikufika huko hakutoa sababu za kwanini hakuileta.

Katuga: Mhe. Jaji alimzuia shahidi asiendelee kutoa maelezo kwanini hakuleta.

Jaji: Hayo mambo ni mapya hatuwezi kukuruhusu. Uliza swali lingine.

Katuga: uliulizwa nani aliyechapisha ulisema ni wewe siku nyingine ukasema sifahamu na leo pia umesema ni yeye kupitia Jambo Tv. Sasa sisi tunataka ufafanuzi

Kaaya: Kupitia Jambo TV alichapisha maudhui yaliyopo kwenye hati ya mashitaka kitendo cha yeye kuwaalika wanahabari na kutoa maudhui yale ni tayari alikuwa ameridhia kutoa maudhui yale mtandoani.

Katuga kila baada ya swali moja anafanya vikao na mawakili wenzake sita hapa Mahakamani. Hii Re Examination yao imekuwa ngumu sana aiseee. Wanahangaika halafu ni kama shahidi anawajibu namna ambavyo walikuwa hawatarajii. Hawayafurahii majibu ya shahidi wao kabisa.

Katuga: Waheshimiwa Majaji naomba tuishie hapa kwenye maswali ya ufafanuzi kwa shahidi wetu. 😂

Hadi majaji wamecheka hapa kimya kimya. Hii re examination ilikuwa ngumu sana. Mhe. Lissu kamshona shahidi hadi upande wa Jamhuri wameshindwa kujua Shahidi atoe ufafanuzi wa jambo gani.😀

Jaji shahidi unaruhusiwa kuondoka. Tunakushukuru kwa ushahidi wako.

Insp. John Kaaya amejaribu kutoka kwa speed kidogo amejikwaa hapa kwenye kiti ametaka kumdondokea Askofu Mwamakula maana amekaa nae karibu na kizimba pale. 😂

Watu wamecheka inaonekana huyu Polisi alikuwa amechoka sana hii kazi kwakweli. ametoka kama haamini kweli amemaliza huu msala.

Amesima Renatus Mkude anasema tunae Shahidi wa tatu ambae ni SAMWEL ELIBARIKI KAAYA.

Jaji sasa huyu shahidi nae aje tuendelee.

Ananingia hapa Askari Mfupi wa kimo, ana kipara na ndevu nyinginyingi kidogo ambazo hazina afya zile ndevu kipilipili.

Jaji unaitwa nani?

Naitwa Samwel Elibariki Kaaya.

Mkaguzi wa Jeshi la Polisi.

Anaangalia kwa chini chini kwa kumuangalia tu muonekano wake inaonekana ana roho ngumu sana.

Anasema ana miaka 39.

Dini yangu ni Mkristo.

Anapelekewa Biblia aweze kuapa.

Anaishika mkono wa Kulia na amenyanyua juu.

Naapa ushahidi nitakaoutoa ni wakweli ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.

Renatus Mkude anasimama naomba aongozwe na Thawabu Issa Wakili wa Serikali.

Huyu Thawabu Issa Wakili wa Serikali ndo yule alijifanya kurusha ngumi juzi kati anajikuta Rashid Matumla.

Amesimama ana kipara kama cha ushahidi.

Thawabu: Uongee kwa Sauti shahidi.

Jaji: Na wewe Wakili ongeza sauti sasa.

Thawabu: Kitengo gani upo?

Samwel Kaaya: Kitengo cha picha Kamisheni ya Uchunguzi sayansi jinai.

Sasa I tabidi huyu Shahidi nimuite Samweli maana na yeye ni Kaaya kama aliyetoka.😂

Thawabu: Kinajihusisha na nini kitendo hicho.

Samwel: Kitengo hicho kinajihusisha upigaji picha wa matukio mbalimbali lakini pia kurekodi matukio mbalimbali ya uhalifu. Kurekodi picha mjongeo za watuhumiwa wa uhalifu.

Thawabu: Upo kama nani kitengoni hapo?

Samwel: Niko kama mtaalamu wa picha baada ya kuteuliwa na DPP na kutangazwa na gazette la serikali GN. No. 745/2022.

Thawabu: Majukumu yako ni nini?

Samwel: Kupiga picha, kurekodi matukio ya uhalifu, kufanya uchunguzi wa picha mbalimbali kwa maana ya picha mjongeo na mnato.

Elimu yangu imegawanyika katika makundi mawili.

Elimu ya Kipolisi mwaka 2013/2014 nilihudhuria mafunzo ya awali ya Polisi. Recruit Course chuo cha Polisi Moshi CCP. Na mwaka 2014 nilimaliza na kutunukiwa Certificate of Competence.

Huko CCP Moshi nilijifunza criminal Laws, Evidence Law, Criminal Procedure, Bionnet, Parade Training, Parade la kutuliza ghasia, Self defense kwa maana ya Judo na Karate na Medani za Kivita.

Thawabu: Ulitunukiwa nini?

Samwel: Cheti cha Umahiri.

Thawabu: Kingine nini?

Samwel: Nilipata cheo cha awali cha Police Constable.

Part 110 itaendelea kwenye post inayofuata.

Part 110

Thawabu: Baada ya kuwa Police Constable nini kilifuata?

Samwel: Nilipangiwa kitengo cha picha yani sayansi jinai.

Mwaka 2014 nilianza mafunzo yanayohusu upigaji wa picha zote yaani video na picha mnato. Nilijifunza pia SOP for Photography laboratory.

Mafunzo hayo yalichukua miezi 6 hayo ya SOP.

Mafunzo mengine mwaka 2021 hadi 2022 nilihudhuria mafunzo ya mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi kwa maanaa ya ACP niliyachukulia Moshi huko.

Yalikuwa ya miezi minne nilijifunza leadership, criminal procedure na sheria ya ushahidi Evidence Law, Criminal Law na Parade, First Aid, Medani za Kivita, Arresting, Drill Parade. Nilipata cheo cha mkaguzi msaidiz wa Polisi.

Kundi la pili linahusu elimu ya ujuzi yaani professional qualification mwaka 2010 nilihudhuria mafunzo ya stashahada ya teknolojia ya habari na mawasiliano yaani diploma in Information technology.

Pia nilihudhuria Mafunzo taasisi ya Uhasibu arusha. Anajisemea hapa alijifunza multimedia, web designing, graphical designing , OOP Object oriented programing language, sema anaongea haraka kama chiriku majaji wanashindwa kumpata vizuri mda mwingine.

Anaendelea hapa alijifunza Computer mathematics, business mathematics, communication skills, database management baada ya hapo nilitunukiwa diploma in Information technology.

Anasema pia alihudhuria mafunzo 2015 ya forensic video examination and data dot technology and itching technology katika chuo cha HAMASCRA College , Gauteng Province , South Africa.

Akajifunza video analysis, email analysis, facial recognition, motor vehicle chassis number examination mafunzo yalichukua muda wa miezi 6 na akapata certificate of competence.

Anaulizwa tena kama anaujuzi mwengine?

Anasema 2016 hadi 2019 alihudhuria mafunzo ya shahada ya kwanza ya elimu ya mawasiliano alisoma IFM.

Anaanza kulist masomo alisoma data base management, computer network,object oriented programming language, supply chain management, artifical intelligence technology, development studies😂😂wanatuchosha tuu hawa.

Alipomaliza alipata Bachelor of Science in Information technology 2019.

Mwaka 2024 alihudhuria mafunzo ya CCTV Forensic Gandinaghar, gujarat state India. Sema shahid nae kutamka alikosoma hawezi anataka atuandikie hapa na hakuna ubao.

Anasema alisoma National Forensic Science University alisoma kwa miezi 3 CCTV surveillance au monitoring, NVR technology network video recorder vs digital video recorder baada ya kuhitimu alipewa certificate of attendance.

Anasema Shughuli hizi kazifanya kwa miaka 12 (utaalamu wa picha)

Anaulizwa maabara ya uchunguzi wa picha inafanyaje kazi?

Anasema wanafanya kwa kuzingatia SOP Standard Operating Procedure za maabara.

Anakuwa na mtaalam mchunguzi wa maabara anaitwa Photographic Expert majukumu ya huyu mtaalamu ni kupokea barua mbalimbal kutoka kwa requesting authorities na kuhakiki vielelezo mbalimbali vinavyotoka sehemu mbalimbal, kuhakiki kama vielelezo vimekidhi matakwa ya kiuchunguzi.

Baada ya kuridhika vile vielezo vimekidhi matakwa hayo vinasajiliwa kwenye laboratory register book yaani PF113 akimaliza kusajili anatoa namba ya usajili kwa ajili ya ufuatiliaji.

Akishatoa hio namba anafungua jalada la uchunguzi wa kimaabara kwa kurejea zile namba alizoziandika

Baada ya kusajili namba hio mchunguzi atapeleka jalada kwa mkuu wa kitengo kwa ajli ya assignment

Mkuu wa kitengo akishapelekewa ataasign mchunguzi ni kwa ajili ya kumantain chain of custody baada ya mkuu wa kitengo kumuassign mchunguzi ataondoka na jalada na vielelezo hivyo.

Mchunguzi akiondoka na vielezo hivyo vinaenda kufanyiwa kazi anasema hapa ofisi yao inafanya kazi mtindo wa FIFO First in First Out yaani kilichoanza kuja ndiko kitafanyiwa kazi.

Kanuni ya FIFO ikizingatiwa mchunguzi ataanza kuja na ataendelea na uchunguzi wake uchunguzi unafanyika katika njia kuu 3.

Wakipokea kielelezo cha picha mjongeo au video utaratibu unakuwa hivi.

Part 111 itaendelea kwenye post inayofuata,

Part 111

Wakipokea kielelezo cha picha mjongeo au video utaratibu unakuwa hivi-;

1. Programu endeshi "operating system"
2. Programu Chunguzi "Forensic Software"
3. Programu Linzi "Security Software"

Hizo ndio njia zinazotumika kufanya uhakiki wa video au picha wakizipokea.

Thawabu anamuuliza kinachofanyika ni nini haswaaa.

Tunachokifanya Computer ni hardware kitu kinachoshikika unakikagua. Kama inaweza kuwa inainteract yaani kuoana na programu endeshi inaweza kuanza kufanya kazi.

Jaji: Shahidi nendeni taratibu msiwe na haraka. Hatuwaelewi kabisa ni kama mnaambiana huko.

Sawa Jaji tunaanza vizuri. Anasema Thawabu Issa.

Hardware ni kitu chochote kinachoshikika. Unachokagua ni utimamu wa Computer kama unafanya kazi. Unakagua programu endeshi ambayo ipo kwenye computer.

Je mfano wa programu endeshi ni nini? Wakili anamuuliza.

Mfano ni kama Window OS ndio programu endeshi.

Thawabu: Endelea sasa

Samweli Elibariki Kaaya: Anaendelea hapa. Unaangalia program endeshi kama iko updated na unaangalia programu chunguzi kama iko poa na Forensic Investigation programu nayo unaiangalia kama iko poa.

Kwenye programu Chunguzi unachokagua ni je program iko updated na inaweza kufanya uchunguzi? Programu linzi yenyewe mfano wake ni CasperSky hizi ndio Security Software. Huko tunakagua programu hiyo ni current au ya zamani isije ikala file.

Thawabu: Tuendeleee Shahidi.

Samwel: Baada ya hapo tunaanza uchunguzi wa awali ambao ni preliminary investigation.

Uchunguzi wa awali tunatizama physical examination na kuangalia content au maudhui yaliyoko kwenye picha mjongeo hio yaliyoko labda kwenye kibebeo chochote mfano flash, solid state drive, au hard disk external hard disk.

Ukimaliza kutazama kielelezo chako utafungua kifaa kwenye komputa ulionayo hio komputa ndio zile komputa zao za kazi.

Ukishafungua utatazama maudhui na picha mjongeo hio picha mjongeo ni video Utanote kwa penseli ulichoandika kupitia police notebook.

Tunanukuu kwenye notebook ili kupata taarifa, uchunguzi na kutunza kumbukumbu.

Baada ya kutazama mchunguzi atafanya confirmatory test au uchunguzi wa kisayansi hapa hii ni stage ya pili baada ya uchunguzi wa awali.

Tunaangalia rangi ya picha na mwanga wa picha yaani RGB anasema hii ni primary colour anaangalia kama ni halisi.

Pia anaangalia movement ya lips na matamshi kama viko sambamba.

Tunaangalia pia necessary au unnecessary movement of things akimaanisha anaangalia vitu vinavyopita kwa kuongoza au vyenyewe automatically mfano kupita kwa mtu kupeleka Mike kwenye podium, kupita kwa nzi.

Anatazama pia mwendelezo wa matukio

Kama kuna kukatika kwa picha au jamshot

Anaangalia mstari mshazari au line of perspective

Hivi vitu vinasaidia kujua maudhui ni halisi au sio halisi kwenye uchunguzi wa awali.

Mstari mshazari unanisaidia kung’amua uhalisia wa picha kwa kuonyesha ukaribu ulioko baina ya object na length ya camera.

Jamshot inasaidia kungamua kujua kama video imekatwa kipande au haijakatwa...

Necessary au unnecessary movement of things inasaidia kujua vitu vinavyopita bila kutarajia.

Unapoona viumbe wanapita hata watu inakuwa sio movement ya kupanga inasaidia kuonyesha originality ya video.

Ukiangalia lips utaona zinatofautiana kama video haitakuwa rahisi.

Huo ndio Uchunguzi wa awali unavyofanyika, nimeeleza hapo awali.

Hatua inayofuata ni Uchunguzi wa Kisayansi ambao ni SCIENTIFIC EXAMINATION.

Huko kinajiri nini?

Anajibu huko tunaenda ku confirm tulivyoviona uchunguzi wa Awali kama ni sahihi ndo maana tunaita confirmatory test.

Huko tunafanya Data Analysis ambapo Meta Data Analysis tunaifanya kupitia program chunguzi ambayo ni Amped Authenticate.

Part 112 itaendelea kwenye post inayofuata,

Part 112

Anaendelea Wakili wa Serikali Thawabu Issa

Hii Meta Data ni nini hasa?

Meta Data ni Data about Data. Yaani picha mjongeo ni Data ndani ya Picha mjongeo kuna Data nyingine ambazo ni taarifa. Hzio taarifa zinaweza kuwa tarehe, jina na kadhalika. Taarifa hizo mjongeo zilizopo kwenye picha mjongeo ndio tunaita Meta Data.

Anasimama Renatus Mkude Wakili Mkuu wa Serikali huyu Baba ni mstaarabu kwakweli. Yeye muonekano wake hana nouma. Anaongea kistaarabu sana. Hana arrogance yoyote. Kwa kumuona tu haoneshi kuwa kisirani kama mawakili wengine wa Serikali.

Anasema kwa sasa ni saa saba naomba tupate break watu wakapate Chakula.

Majaji wanaandika kidogo.

Wanamuuliza Mshitakiwa. Anasema sina pingamizi.

Wanaandika kidogo. Wanasema sasa twendeni break tukutane baada ya lisaa limoja kutoka sasa. Tumeishia hapo kwa sasa. Tukirudi Shahidi ataendeelea kutoa ushahidi wake kwa maana ya EXAMINATION IN CHIEF ITAENDELEA.

Kumbuka jina la Shahidi ni SAMWEL ELIBARIKI KAAYA alkiongozwa na Wakili wa Serikali Thawabu Issa.

Tukutane baadae kidogo.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 113

Thawabu Issa anasema Uliishia kwenye kutazama Meta Data.

Sasa endelea.

Samwel: Nilisema tunafanya Meta Data Analysis. Kuna kitu kinaitwa JSON tunatumia kuidentify taarifa za kidigitali. Pia inaweza ku identify taarifa mbalimbali kama vile aspect ratio kwa maana ya ukubwa wa video na picha yenyewe.

Kingine tunafanya uchunguzi wa Chron analysis. Hii maana yake ni namna ya kufanya utambuzi ili kung'amua kama kuna viashiria vya deep fake.

Hii deep fake ni uwezekano wa teknolojia ya Artificial Inteligence au teknolojia yeyote inayoweza kufanya Manipulation.

Kitu kilichofanyiwa Chron maana yake mifumo mingi inayoendeshwa kwa AI hivyo basi upo uwezekano wa kuweka sura ya mtu au sauti ya mtu kwenye mwili wa mtu mwingine.

Hii AI ni alogarithm ambayo ina learn behaviour ya kitu na kuiga kufanya kitu hicho. Hivyo ni muhimu kufanya Chron analysis ili kuthibitisha.

Yote hayo yapo kwenye programu chunguzi yaani Amped Authenticate. Unaenda kwenye button ya Chron Analysis. Hapo itakuonesha sehemu za trace. Yaani ni sehemu zilizofanyiwa Chron.

Ukishajiridhisha unaenda kwenye hatua inayofuata. Unafanya kitu kinaitwa error level data analysis. Hapo utabaini whether picha mjongeo ni compressed au decompressed. Yaani je video imefinywa au iko halisi? Hapo ndio utajua.

Tunaenda kwenye button iliyoandikwa error hapo ndio tunaangalia vitu viwili. Ambavyo ni V CODEC na A CODEC.

Unaposema VCODEC maanaa yake ni video compression and decompression.

A CODEC audio compression and decompression.

Hatua nyingine tunafanya (PRNU) Cencor patern analysis Hii ni Photo Response Non Uniformity ambayo unaitumia ku identify kwamba picha mjongeo hiyo kama ina alama ya kipekee ambayo ndio hiyo video printing.

Digital signature inaacha camera inatambulisha camera yenyewe.

Baada ya hapo naenda kwenye hatua inayofuata noise analysis ambayo natazama usafi wa picha mjongeo tutakayoichunguza yaani VIDEO CLEANLINESS.

Hapo kwenye noise ni kama chengachenga zikisambaa zinadistort au kuharibu uhalisia wa video

Maelezo yote haya anaelezea ufundi wakuangalia video

Anasema video ikirekodiwa usiku inakuwa na chenga chenga wakat mwingine kama ile rekodi haikuwa nzuri zile chengachenga zinaweza sababisha picha isionekane vizuri.

Nimepata dharura nalazimika kutoka mazingira ya hapa so sitaweza kuendelea kuwapa updates za kesi kwa siku ya leo naomba radhi kwa usumbufu wote uliojitokeza.

Credit: page ya hilda Newton fb
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Hivi walikua wanasema mashahidi ni wa siri mbona majina yao yanawekwa wazi au mimi ndo sielewi kinachoendelea

..mashahidi wa siri toka Jambo Tv, Chaumma, na kwingineko, watakuja baadae.

..sasa hivi ni mashahidi toka vyombo vya dola. Na mahakama iliamua kwamba mashahidi toka vyombo vya dola hawatakuwa wa siri.

..mashahidi ambao ni raia ndio iliamuliwa na mahakama kuu kuwa watakuwa wa siri.
 
Nimekupata vyema!
Shukran kwa ufafanuzi.
 
Kaaya: Mimi ni askari Polisi sio fundi viyoyozi.

Mhe. Lissu: Kwahiyo hukusema hapa kuwa umesomea Air Condition? wewe ndio ulituambia haya mambo ya viyoyozi au nani alituletea?

Kaaya: Nilisema basi yaishe.

😂😂😂😂😂😂😂😂😂
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Comrade, uwe unatuletea mapema hii taarifa ya kumhusu Rais wetu. Nimeutafuta huu uzi kutwa nzima, sikuupata. Thanks for that.
Ngoja niupitie sasa taratibu, hatua kwa hatua.
Sawa mkuu
Si unajua napost baada ya mahakama kuisha
 
Leo Oktoba 17, 2025

Jana tuliishia part 113 so leo tunaendelea na -;

Part 114

Imepigwa high courttttttt watu wote wamesimama.

Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao.

Karani anasoma namba ya kesi.

Anasimama Wakili Mkuu wa Serikali anatambulisha jopo lake.

Renatus Mkude anamwambia Jaji anaomba Thawabu Issa aendelee alipoishia jana.

Shahidi ulisema kwamba baada ya kufanya analysis ya picha nini huwa kinafuata?

Baada ya kumaliza kufanya hio analysis kinachofanyika ni kuscreenshot ambako ni kupiga picha kutumia interface ya kioo taarifa za kidigitali kupitia metadata.

Baada ya kuscreenshot nitazichapisha kwa maana ya kuziprint kwa ajili ya kuambatanisha na taarifa ntakayoiandaa kwa ajili ya Uchunguzi.

Baada ya kufikia hio hatua naandaa tarifa ya uchunguzi kwa kurejea uchunguzi niliofanya kwa kuangalia police notebook na taarifa nilizoandika.

Taarifa hio huwa inaenda sambamba na covering letter na covering letter kwa ajili ya kuwajibu requesting authority walioomba niwajibu baada ya kufanya uchunguzi huo.

Baada ya kuandaa tarifa hiyo taarifa ya uchunguzi inakuwa na majina ya mchunguzi, logo ya jeshi la polisi, mchunguzi akishamaliza kuandaa tarifa hiyo ataisign, kugonga muhuri wa commission ya uchunguzi wa sayansi jinai (forensic).

Baada ya kugonga muhuri itasainiwa na mnadhimu wa sayansi jinai kwa niaba ya kamishna wa uchunguzi jinai.

Kama mnadhim hayuko basi afisa kwenye rank ya assistant commissioner ataisign.

Mchunguzi atapaki vielelezo kwenye bahasha, atasign bahasha iliyobeba vielelezo na kugonga muhuri.

Barua na covering letter tunaweka kwenye bahasha na kuandika maeneo zinakoenda, kusign na kuweka muhuri.

Baada ya hapo ofisi itawasilana na requesting authority kupata majibu ya kielelezo cha uchunguzi husika.

Iambie mahakama tarehe 8 Mwezi wa 04, 2025 ulikuwa wapi?

Samwel: Kama afisa mchunguzi wa zamu katika kitengo cha picha nilipokea barua mbili zenye kumbukumbu Na DA. 223/476/01DB/168 nyingine ikiwa DA.223/476/01DB/169 na ikiwa imeambatana na flash disk moja aina ya XIOXIA yenye ukubwa wa GB 8 Na flash disc ikiwa na alama ya DM na Ilikuwa iko attached Na. PF145 (exhibit label)

kielelezo kingine kilikuwa Secured Digital SD Adapter ilikuwa imepewa alama ya X Sticker na adaptor hio ilikuwa ina rangi nyeusi ndani ya SD Adaptor kulikuwa na memory card aina ya aldeepo.

Kielelezo hiko kilikuwa kwenye kibahasha kidogo kilichokuwa attached na PF-145 exhibit level

Waheshimiwa majaji barua hizo na vielelezo hivyo vililetwa na Assistant inspector Michael Gyumi.

Vikitokea ofisi ya mkuu wa upelelezi kanda maalum ya Dar es salaam.

Baada ya kupokea vielelezo hivyo na kusign dispatch book Waheshimiwa majaji nilihakiki vielelezo nilivyoletewa kama vinakidhi matakwa ya uchunguzi.

Nilihakiki vifaa vilivyoletwa kama ndivyo vilivoandikwa kwenye barua ya requesting authority.

Katika kuhakiki nilibaini vinakidhi matakwa ya uchunguzi wa kisayansi.

Katika maabara yetu tunapokea vifaa vibebeshi ni kama vile flash disk, memory card baada ya kujiridhisha na uhakiki wa vielelezo nilivyoletewa nilisajili vielelezo hivyo laboratory book register PF 113.

Nilisajili kwa barua yenye kumbukumbu namba DA. 223/476/01B/168 nilisajili kwa namba FB/PH/LAB/106/2025 na barua yenye kumbukumbu namba DA.223/476/01D/169.

Nilimuandikia hizo namba Insp. Michael Gyumi kwa ajili ya ufuatiliaji.

Zile nambari zinatokana na sequence and series jinsi tupokeavyo vielelezo.

Kikipokelewa cha kwanza January kitaandikwa namba moja.

Tunakwenda hivyo hivyo hadi mwisho.

Nilifungua majalada mawili ya uchunguzi wa kimaabara jalada hilo lilirejea namba nilizosajili kwenye PF 113.

Na baada ya usajili huo nikapeleka kwa Mkuu wa kitengo kwa ajli ya assignment kwa hayo majalada niliyoyafungua kwa ajili ya uchunguzi.

Part 115 itaendelea kwenye post inayofuata

Part 115

Anaendelea Shahidi namba 3 wa Jamhuri Samuel Elibariki Kaaya

Baada ya hilo kutokea nilienda maabara kwa ajili ya kuandaa vifaa vya uchunguzi.

Barua zote mbili tukianza na ile ya FB/PH/LAB/106/2025 Ilikuwa inahusu jalada la kuchunguza uchapishaji wa taarifa za uongo na lile lenye namba /PH/LAB/107/2025 ikiwa na kosa la uhaini.

Thawabu ; umesema baada ya kuwa assigned ulienda maabara, ieleze mahakama nini ulifanya nini?

Nilifika maabara na kufanya maandalizi ya vifaa vyangu vya uchunguzi.

Maandalizi niliyoyafanya ni kuandaa vifaa chunguzi kwa maana ya computer maalumu kwaajili ya uchunguzi.

Baada ya kumaliza kuandaa computer, printer kwaajili ya uchunguzi.

Tukumbuke kwamba nilikuwa na barua mbili ambazo nilikuwa assigned kuzifanyia kazi hivyo niliamua kusoma barua hizo ili kufaham matakwa ya requesting authority wanataka nini.

Mhe Jaji Barua moja ilikuwa inahusu kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni na nyingine ilikuwa inahusu uhaini.

Barua ya uhaini ilikuwa na kumbukumbu namba DA.223/476/01B/169.

Barua hiyo pamoja na muhtasari ilinihitaji kufanya mambo yafuatayo; ilihitaji chanzo cha picha mjongeo inayopatikana kwenye flash disk aina ya XIOXIA, kuchunguza uthibitisho wa uhalisia wa maudhui ya picha mjongeo iliyopo kwenye flash disk, nichunguze chanzo cha picha mjongeo iliyopo kwenye memory card.

Pia nichunguze uhalisia wa maudhui ya picha mjongeo iliyopo kwenye memory card aina ya Aldeepo, kufanya ulinganisho wa maudhui ya picha mjongeo iliyoko kwenye flash disk aina ya XIOXIA kama yanafanana na maudhui ya picha mjongeo iliyokuwepo kwenye memory card aina ya Aldeepo.

Kiuhalisia huyu shahidi anazungumza jambo hilo hilo moja na Wakili wa Serikali anarudia kuuliza swali hilo hilo mara tatu tatu mpaka mtu unaona uvivu kuandika.

Mfano hiyo habari ya video ilisema nini au Mh. Lissu alisema nini kwenye mazungumzo yake na watia nia kwa namna kesi inavyoenda hata sio tatizo na amekuwa hapingi kuwa maneno yale sio yakwake. Swali lake na hoja yake ni kwamba je hayo aliyosema ni kosa kisheria? Ni Uhaini?

Sasa hawa mashahidi watupotezea muda wa siku kadhaa kutuambia namna walivyochunguza video wakati hiyo video mtuhumiwa hana pingamizi nayo. Nafahamu zipo hatua za kisheria zinapaswa kufuatwa ili exhibits zipokelewe Mahakamani lakini kwa shahidi huyu nimewauliza hata Mawakili wanasema kwa kiasi kikubwa wanapoteza tu muda. Mengine hata sio matakwa ya kisheria.

Acha tuendelee nae na tunasubiri muda wa yeye kuanza kuulizwa maswali ya Dodoso na Mshitakiwa ndio tutaelewana zaidi.

Samuel Kaaya: Pia niliambiwa nichunguze maudhui yafuatayo kama yanapatikana kwenye flash disk hiyo, maudhui hayo ni haya;

"wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli kabisa maana tutazuia uchaguzi, hivyo tutahamasisha uasi, hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko, tunaenda kukinukisha sana sana, uchaguzi huu tutauvuruga maana tunaenda kukinukisha vibaya sana."

Nilifanya uhakiki wa vifaa vya uchunguzi kwa maana ya computer maalumu kwaajili ya kufanyia uchunguzi huo, printer maalum aina ya Epson, nilikagua program endeshi kwa maana ya operating system window eleven, programu chunguzi kwa maana ya forensic software and security software amped five na ampend authenticate.

Waheshimiwa majaji naomba nieleze maana ya amped five na amped authenticate.

Ampend authenticate inafanya basic and advance image analysis, pia inafanya basic and advance video analysis pia inafanya utambuzi wa sura kwa maana ya facial recognition Waheshimiwa majaji nilitazama pia programu linzi kwa maana ya security software.

Hii programu linzi ni Kaspersky antivirus ambayo kazi yake ni kulinda programu endeshi pamoja na programu zote zilizopo kwenye computer hiyo na pia inalinda vielelezo unavyovipokea visiliwe na virus au malware.

Part 116 itaendelea kwenye post inayofuata.

Part 116

Anaendele Shahidi Samuel Elibariki Kaaya

Tunafanya huu uhakiki kwasababu programu endeshi ndiyo inayoendesha hardware computer, kwa maana nyingine kama programu linzi isipokuwa compatible / isipoendana na hardware kwa maana ya compute hiyo, it cannot execute any task.

Sambamba na hilo programu chunguzi lazima iwe compatible na programu endeshi ili iweze kufanya majukum yake mahususi.

Waheshimiwa majaji hali ya programu kwa siku hiyo ya tarehe 08/04 ilikuwa timilifu kwa maana programu zilikuwa updated/zilikuwa salama kwaajili ya kufanya majukumu yake mahususi.

Waheshimiwa majaji baada ya kufanya uhakiki wa vifaa nilifanya uchunguzi wangu wa awali kwa maana ya preliminary examination.

Nilifungua computer yangu maalum kwa maana ya kuiwasha, nilichukua flash disk aina ya XIOXIA kwaajili ya kuifanyia uchunguzi.

Baada ya kufungua computer yangu niliiweka kwenye universal serial bus (USB).

Baada ya kuiweka kwenye USB niliifungua ili kutazama kilichopo ndani ya flash.

Baada ya kuifungua nilikuta ina nywila yaani passwords hivyo niliwasiliana na mamlaka iliyoleta vielelezo kwa ajili ya kupata nywila.

Baada ya kupata nywila niliendelea na uchunguzi wangu wa awali na nilikutana na video mjongeo moja ilikuwa na heading Tundu Lissu uso kwa uso na watia nia majimboni, no reforms no election njia panda.

Na hiyo Video ilikuwa na urefu wa masaa matatu na dakika 38 na ilikuwa katika mfumo wa MP4 file format.

MP4 inatokana na neno MPEG part 14 (kirefu cha MPEG ni Movable Picture Expert Group).

Huyu Bwana Samweli Elibariki Kaaya nae miongoni mwa kitu anatufurahisha hapa Mahakamani ni kujifanya anapenda vingereza fulani kutaja misamiati yake ya kitaalamu.

Sasa anakosea sana kutamka hayo maneno Mh. Lissu kuna muda anauliza mara mbili mbili kuwa umetamka nini?

Akirudia anawaambia tamkeni vizuri jamani kingereza cha wapi hicho, Nafikiri kama Taifa hili swala la kizungu ni ugonjwa mkubwa, inafaa utafutiwe dawa halafu huu ugonjwa kwa mapolisi unaweza kuwa ni mkubwa sana kuliko makundi mengine yote. 😂😂😂

Thawabu Issa: Kingine nini uliona:

Shahidi: Waheshimiwa majaji pia niliona maudhui yafuatayo:

Wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi ni kweli maana tutazuia uchaguzi hivyo tutahamasisha uasi na hiyo ndio namna pekee ya kuapata mabadiliko, tunakwenda kukinukisha sana sana tunaenda kuuvuruga uchaguzi huu, tunaenda kukinukisha vibaya sana.

Waheshimiwa majaji maudhui haya yanapatikana kwenye lisaa la pili na dakika 58.

Pia nilibaini mwendelezo wa matukio kwa maana ya continuity, pia nilibaini jup shoot kwa maana ya kuwa hakukuwa na kukatika kwa picha.

Nilibaini pia necessary or unnecessary movements, kulikuwa na movement za watu mbalimbali au mtu mmoja mmoja kutoka sehemu moja Kwenda sehemu nyingine.

Nilibaini pia uwepo wa rangi halisi na mwanga halisi wa picha mjongeo.

Naomba nifafanue kuhusu rangi na mwanga halisi.

Waheshimiwa majaji unaporekodi picha au picha mjongeo kuna kitu kinaitwa white balance.

White balance kazi yake ni kuseti mwanga na rangi asili ya vitu vinavyorekodiwa.

Hii white balance ina component chache kwa ajili ya kufanya hayo.

Mfano kama unarekodi wakati wa mvua utaiseti camera yako kwenye cloud setting, kama ni kwenye kivuli utaseti camera yako kwenye shadow, kama ni majira ya kawaida ya jua utaseti kamera yako kwenye day.

White balance ilituonyesha kwamba video hii ina mwanga halisi.

Waheshimiwa majaji pia nilitazama mstari mshazari na ninaomba nizungumzie hapa ili pakae sawa.

Katika mizania ya informatics object near the length of the camera is much greator than the object far from the length of the camera.

Mfano mzuri ni mtu anapojipiga selfie, sehemu ya Kichwa itakuwa ni kubwa kuliko sehemu ya miguu ambayo iko mbali na camera.

Kwa maana hiyo waheshimiwa majaji focal length is the basic attribute in this fact.

Part 117 itaendelea kwenye post inayofuata

Part 117

Thawabu: Shahidi uliona nini ulipotazama video uliyokuwa unachunguza kuhusiana na mstari mshazari?

Waheshimiwa majaji nilibaini uwepo wa mstari mshazari kwa maana kuwa picha mjongeo ile ilikuwa ni halisi.

Mwisho wa Ushahidi wa shahidi kuhusu uchunguzi wa awali, sasa anaingia uchunguzi wa kisayansi kuhusu picha mjongeo.

Shahidi anaulizwa baada ya kumaliza uchunguzi wa awali kumalizika ulifanya nini? Waheshimiwa majaji nilifanya uchunguzi wa kisayansi maana uchunguzi wa awali hauwezi kuthibitisha kila kitu.

Hii ni kwasababu huwezi kuthibitsha uchunguzi wa kisayansi kwa kutazama tu lazima uingie kwa ndani.

Katika kufanya uchunguzi wa kisayansi nilifungu application yangu ya amped authenticate nilienda sehemu imeandikwa file na kuna menu ndani inaitwa open, niliielekeza sehemu inayosomeka flash disk XIOXIA.

Niliifungua na baada ya kuiona niliihakiki then baada ya kufungua flash hiyo nili double click picha mjongeo hiyo iliyopo kwenye flash kwaajili ya kuivuta (to export) kwenye amped authenticate interface.

Amped authenticate interface ni pale ambapo the examiner anaweza kuiona video na kuifanyia uchunguzi.

Thawabu : ulifungua nini tuendelee.

Samweli: baada ya kufungua nili click baada ya kufungua nili double click picha mjongeo iliyopo kwenye flash kwa ajili ya kuivuta kwenye Amted Authenticate interface (kuivuta ni export)

Thawabu : Tuendelee

Samweli: Amted authenticate interface ni sehemu ambayo examiner anaweza kuiona video yake na kuifanyia uchunguzi.

Samweli: baada ya kufungua export video yangu nilianza uchunguzi wa kisayansi.

Thawabu: ambapo ulifanya nini?

Samweli: Nilienda moja kwa moja kwenye media info ambayo nini JSOM.

Lengo la kwenda hapo ni kutafuta info za picha mjongeo kwa maana ya meta data.

Baada ha kwenda kwenye JSOM Kutafuta data za kidigitali za picha mjongeo nili screenshot pia nilikuwa na police notebook kwa ajili ya kurekodi kila hatua ninayofanya

Thawabu: Ulichobaini hapo ni nini?

Baada ya kupata taarifa za kidigitali nilibaini picha mjongeo ninayochunguza ni picha iliyopakuliwa kwa maana ya downloaded

Picha iliyopakuliwa kwenye mtandao wa kijamii unaotokana na website au web inayotambulika kwa URL

Thawabu : URL ni ya mtandao gani?

Samweli: youtube

Thawabu: kitu gani kingine uliona?

Samweli: Niliona URL upload ilikuwa ni at jambo Tv.

Pia nilibaini viewers walioona walikuwa takribani 52,406 lakini pia niliona wafuasi kwa maana ya subscribers ambao ilikuwa jumla ya watu 1,010,000.

Pia niliona walio-like kwa maana ya kupenda hayo maudhui walikuwa 578, vingine nitavionyesha nitakapokuwa nawasilisha taarifa yangu ya uchunguzi.

Shahidi anamaliza kueleza kuhusu uchunguzi wa kisayansi sasa anaeleza hatua inayofuata ya clone analysis.

Shahidi anaulizwa baada ya kumaliza uchunguzi wa kisayansi alifanya nini?

Baada ya kumaliza uchunguzi wa kisayansi nilifanya clone analysis.

Waheshimiwa majaji hapa tunaangalia kama kuna pandikizi labda la sura ama sauti. Clone analysis may determine if there is a deep fake.

Waheshimiwa majaji kupitia hiyo menu ya clone analysis inayopatikana kwenye amped authenticate, hii inasaidia to identify sehemu ambazo zimepandikizwa na mtu akiwa anongea itakuwa inaonyesha mark mtu akiwa anaongea ila kwenye video itakuonyesha trace ya maungio kama mtu amevalishwa sura ya mtu mwingine. Mimi nilibaini kuwa picha mjongeo niliyoletewa haikuwa na pandikizi lolote.

Shahidi anamaliza kueleza kuhusu uchunguzi wa clone analysis sasa anaeleza hatua inayofuata ya noise analysis.

Thawabu: tupo kwenye hatua ya noise analysis hebu tuendelee.

Samweli: Kwa mantiki hiyo tunapofanya mambo ya noice analysis ni namna gani kinaweza ku affect hichi kitu kinaitwa pixel

Thawabu Issa: ulibaini kitu gani kwenye noise analysis na pixel?

Samweli: Picha hiyo mjongeo ilirekodiwa day time.

Part 118 itaendelea kwenye post inayofuata.

Part 118

Thawabu baada ya kubani picha ilirekodiwa mchana ni nini kingine ulibaini?

Samweli: Nilikuwa na note kwenye note book yangu nikaenda hatua inayofata.

Thawabu: Hatua gani hiyo ndugu shahidi?

Samweli: Baada ya hapo nilitoa flash yangu.

Thawabu: umeitoa wapi

Kuna muda wanaulizana vitu hadi mtu unasema hivi wana akili hawa.🤦🏾‍♀️

Samweli: Nilitoa kwenye USB port kwenye kompyuta yangu ya uchunguzi.

Samweli: Nilitoa memory card inayotakiwa kufanyiwa uchunguzi pia.

Waheshimiwa Majaji nilifungua software na kompyuta ilikuwa on nika export kama nilivyosema mwanzo.

Waheshimiwa naomba niwarudishe nyuma kidogo nisije nikawa naruka nilifanya uchunguzi wa Awali wa Memory card pia.

Thawabu: Ulifanya nini kwenye uchunguzi huo wa awali?

Samweli: Nilifungua memory card ili kujua kilichopo ndani baada ya kufungua nilibaini mambo yafuatayo:

Kuwepo kwa vipande 25 vya picha mjongeo.

Thawabu: Kingine ulichobaini ni nini?

Samweli: Vipande hivyo vilikuwa kwenye folder lililoandikwa stream.

Na pia Vipande hivyo vilikuwa named kuanzia namba 6 hadi 30.

Kipande namba 28 kilikuwa na maneno yafuatayo, wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi, kweli maana tutazuia uchaguzi tutahamasisha uasi hiyo ndio njia pekee ya kupata mabadiliko tunaenda kukinukisha sana sana uchaguzi huu tutauvuruga tunaenda kukinukisha vibaya sana.

Maudhui hayo yalipatikana dakika ya 8 na sekunde 27.

Waheshimiwa majaji pia niliona mwendelezo wa matukio kwa maana ya continuity, niliona necessary and unnecessary movement of the things, niliona mstari mshazari, pia niliona uwepo wa rangi halisi na mwanga halisi due to the presence of white balance.

Ni hayo tu waheshimiwa majaji nilibaini na niliandika kwenye notebook yangu.

Mwisho wa ushahidi wa shahidi kuhusu uchunguzi wa awali kuhusu picha mjongeo zilizo kwenye memory card.

Thawabu Issa: Shahidi anaulizwa baada ya kumaliza uchunguzi wa awali ulifanya nini?

Waheshimiwa majaji nilipita njia zilezile nilizosema awali nilifungua ampend authenticate nilifungua menu ya file na niliclick palipoandikwa open nak u export video moja baada ya nyingine.

Waheshimiwa majaji hapa nilikuwa na video clip 25 hivyo nilichukua video moja baada ya nyingine mpaka nilipomaliza uchunguzi wangu.

Nilianza na uchunguzi unaoitwa error level analysis na hapa tunaangalia compression or decompression ya video unayoifanyia analysis.

Hapa nilitazama v codec na a codec ili kutazama kama video iliongezwa sauti au video yenyewe. Nilibaini katika uchunguzi wangu kuwa video ilikuwa ni halisi.

Waheshimiwa majaji baada ya hapo nilifanya sensory pattern analysis kwa maana ya PRNU (kirefu chake ni Photo Response Non-Uniformity).

Katika uchunguzi wangu nilibaini kamera iliyotumika ni sony hxr-nx100 kupata picha mjongeo hizo.

Baada ya kubaini hivyo niliendelea na hatua inayofuata lakini naomba kueleza mheshimiwa jaji kwamba meta data inaweza kubainisha kifaa ulichotumia.

Waheshimiwa majaji pia nilifanya clone analysis na nilibaini kuwa hapakuwa na pandikizi lolote la picha mjongeo hiyo wala sauti.

Baada hapo nilifanya noise analysis na nilibaini picha mjongeo niliyokuwa naichunguza haikuwa na noise zilizosambaa.

Uchunguzi mwingine niliofanya ni illumination analysis hapa tunaangalia kiasi cha mwanga uliotumika wakati picha inarekodiwa kwa maana ya light balance, iso, iris or aperture na mwisho ni shut up speed.

Hii ilinisaidia kutambua kuwa pich hiyo ilirekodiwa na camera hivyo ni halisi.

Shahidi anamaliza maelezo kuhusu uchunguzi alioufanya na sasa anaeleza nini alifanya baada ya kumaliza uchunguzi.

Part 119 itaendelea kwenye post inayofuata.

Part 119

Shahidi sasa anaulizwa baada ya kuchunguza vielelezo hivyo viwili kwa maana ya flash disk na memory card alifanya nini? Anayemuuliza ni Wakili wa Serikali Thawabu Issa.

Shahidi anajibu kuwa waheshimiwa majaji nilianza kuandaa taarifa ya uchunguzi huo.

Taarifa ambayo ilijibu kile ambacho matakwa ya requesting authority ilitaka kufanyiwa.

Requesting authory walitaka kujua chanzo cha picha mjongeo iliyopo kwenye flash disk, lakini pia chanzo cha picha mjongeo iliyopo kwenye memory card, kingine kupata uthibitisho wa uhalisia wa maudhui yaliyokuwepo kwenye picha mjongeo iliyopo kwenye flash disk na uthibitisho wa uhalisia wa maudhui yaliyokuwepo kwenye picha mjongeo iliyopo kwenye memory card, ulinganisho wa uhalisia wa picha mjongeo iliyopo kwenye flash disk na iliyopo kwenye memory card, pia kutambua kama kuna uwepo wa maudhui yafuatayo;

Wanasema msimamo huu unaashiria uasi ni kweli kwasabbau tunakwenda kuzuia uchaguzi hivo tutahamasisha uasi hiyo ndio njia pekee ya kupata mabadiliko tutakinukisha sana sana uchaguzi huu tutauvuruga tutakinukisha vibaya sana.

Kulingana na maombi kutoka kwa requesting authority niliandaa ripoti nikijibu hayo niliyoombwa kuyachunguza majibu niliyoandaa ni kama yafuatayo.

Mh. Lissu anasimama na kupinga shahidi kuanza kuzungumzia ripoti kabla ya ripoti kuwa tendered mahakamani ikiwa hivyo ni sawa na kuingiza Ushahidi kwa mlango wa nyuma.

Wakili wa Serikali Thawabu Issa ameomba kuondoa hilo swali.

Baada ya kukamilisha kuandaa report uliandaa nini? Waheshimiwa majaji niliandaa covering letter kwaajili ya kuwajulisha requesting authority kuhusu majibu ya uchunguzi huo.

Baada ya kuandaa barua hiyo ilisainiwa na mnadhimu wa maabara ya uchunguzi kwaniaba ya kamishna wa uchunguzi wa sayansi ya jinai.

Barua pamoja na ripoti ya uchunguzi ziligongwa muhuri wa kamisheni.

Baada ya hapo nilisaini taarifa yangu ya uchunguzi na tulipaki vielelezo na taarifa ya uchunguzi.

Vielelezo niliweka katika bahasha na taarifa niliweka katika bahasha. Baada ya hapo nilisaini bahasha zile na kuandika majina yangu katika bahasha sambamba na hilo niliandika maelezo ya uchunguzi nilioufanya.

Bahasha niliiwekea lakiri / reference nyekundu.

Kwenye bahasha ya taarifa niliweka covering letter, ripoti na taarifa ya uchunguzi.

Baada ya kukamilisha hayo niliwasiliana na requesting authority hapa namaanisha ofisi ya Mkuu wa upelelezi kanda maalum ya Dar es Salaam.

Thawabu Issa: Sasa nini tena kiliendelea?

Shahidi anajibu hapa.

Siku hiyo ya tarehe 08/04/2025 Assistant Inspector Michael Gyumi alivifuata vielelezo hivyo;

Nilimkabidhi vielelezo akasaini kwenye dispatch book akasaini na akaondoka na vielelezo.

Nilimkabidhi taarifa ya uchunguzi ikiwa sambamba na meta data, vielelezo pamoja na maelezo yangu.

Ieleze Mahakama unawezaje kuitambua flash disk? Ilikuwa ni aina ya XIOXIA, ukubwa wa GB 8, alama ya stika ya kijani imeandikwa DM, ilikuwa attached na exhibit label PF 145.

Ndani yake kulikuwa na video yenye title Tundu Lissu uso kwa uso na watia nia, no reforms, no election njia panda.

Waheshimiwa majaji kuhusu memory card naweza kuitambua ilikuwa kwenye sd adaptor iliyopewa alama x, ilikuwa aina ya aldeepo na ilikuwa na ukubwa wa GB 32, ilikuwa na rangi nyekundu na nyeusi, ilikuwa na jumla ya vipande vya video 25

Wakili mkuu wa serikali Renatus Mkude amesimama kuomba health break.

Mhe. Lissu anasimama na kusema waheshimiwa majaji sitaki kuwafundisha mawakili kumi na Jamhuri namna ya kuendesha kesi yao.

Lakini kwa hapa walipofikia wanaweza ku tender vielelezo vyao ili tukienda break wawe wameshamaliza zoezi la Kutenda vielelezo labda kama wana maelezo mengine lakini kwa hapa tulipofikia nafikiri wange tender vielelezo, hapa watu wanaongea kwa hisia naona Mawakili wa Serikali wanakubaliana na hoja ya Lissu.

Part 120 itaendelea kwenye post inayofuata.

Credit!hilda Newton fb
 
Hii kesi ni ya kijinga! Na inapotezea tu watu muda wao. How come, mashahidi wote wanarudia kuongelea mambo yale yale! Tunakinukisha sana! Tutahakikisha uchaguzi haufanyiki, nk. Na wakati mtuhumiwa alishajibia tayari!!!
 
Huyu Lissu sio wakumkimbilia akiwa mahakamani anakuvua nguo peupeee ukiwa haujajipanga.
 
Back
Top Bottom