JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kwenye shauri hilo la jinai, Namba 19525, Mwaka 2024, Askofu Kadutu au Askofu Mwana Mapinduzi anadaiwa kutamka maneno ya uchochezi katika mkutano wa siasa, uliofanyika siku ya Jumatatu, Mwaka huu, Kijiji cha Ibaga wilaya Mkalama Mkoani Singida, hali iliyoelezwa na Wakili wa Serikali Almachius Bagenda.
Wakili huyo wa Serikali amesema ni kosa linaloweza kujenga chuki kwa Wananchi dhidi ya askari na Serikali yao, kutokana na uchochezi huo.
Kutokana na hali hiyo, Wakili Tundu Lissu, amemwomba Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida, Allu Nzowa, kupitia shauri dogo alilofungua mahakamani hapo, kutupilia mbali kesi hiyo, hoja iliyoibua malumbano ya kisheria, kutoka kwa wakili wa Serikali, Bagenda.
Hakimu Nzowa, ameahirisha hadi Desemba 2, 2024, atakapotoa uamuzi, juu ya pingamizi lililowekwa na upande wa utetezi, kupinga kuendelea kusikilizwa kwa shauri hili, linalomkabili Askofu Kadutu.