- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho amekuwa na safari katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kwenda kushukuru na kusambaza ajenda yao ya No reforms No Election.
Madai
Ipo grafiki inayosambazwa mitandaoni ikiwa na Taarifa kuwa Lissu amesema kuwa hakatai kama anaumwa ila hiyo haina maana kuwa hana uwezo wa kuongoza. Garfiki hiyo inaonekana kuwa na nembo ya gazeti la Mwananchi wanayoitumia katika mitandao yao ya kijamii. Taarifa hizo zimehifadhiwa hapa na hapa
Uhalisia wa grafiki hiyo
JamiiCheck imefuatilia grafiki hiyo ka njia ya mtandao ikiwemo na kubaini kuwa grafiki hiyo imehaririwa kutoka kwenye grafiki halisi iliyochapishwa katika ukurasa wa Instagram waa gazeti la mwananchi, tarehe 15/02/2025.
Grafiki hiyo imehaririwa ujumbe, pamoja na tarehe kutoka tarehe 15/02/2025 na kuwekwa tarehe 19/02/2025. Aidha ujumbe umehaririwa kutoka,
“Lissu: Nimejiandaa kufungwa katika kudai haki mfumo wa uchaguzi” na kuwa “Lissu: Sikatai naumwa, ila haina maana sina uwezo wa kuongoza”. Tazama hapa kuona grafiki halisi.
JamiiCheck imefanya utafutaji pia kwa njia ya mtandao, kwa kutumia X advance search kwa kuchuja tarehe kati ya tarehe 18/02/2025 hadi 20/02/2025, tumebaini kuwa katika ukurasa wa (X) Mwananchi News hakukua na taarifa inayomuhusu Lissu. Hivyo grafiki hiyo haikuchapishwa na Mwananchi tarehe 19/02/2025.