Lissu akiwa mwenyekiti wa CHADEMA atahujumiwa sana na hatafanikiwa chochote, lakini pia akiwa mgombea urais wa CHADEMA atahujumiwa na atapata aibu

Lissu akiwa mwenyekiti wa CHADEMA atahujumiwa sana na hatafanikiwa chochote, lakini pia akiwa mgombea urais wa CHADEMA atahujumiwa na atapata aibu

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ukosoaji wake dhidi ya viongozi waandamizi ndani ya CHADEMA hususani kuhusu mambo ya rushwa na uchaguzi wa serikali za mitaa, ulionekana kama usaliti, hujuma, dharau na utovu wa nidhamu kwa mwenyekiti taifa wa chama hicho. Na kwahivyo sababu ya kuhujumiwa kwake msingi wake utakua ni huo

Lakini pia hata mlengwa wa ukosoaji ule ilisemekana na kuonekana wazi kua ni mwenyekiti wa Chadema Taifa. Bilashaka amemstahi tu ndiyo maana hakuwahi kujibu chochote na anajua ni wakati gani muafaka wa kujibu na kuchukua hatua.

Uamuzi wa Tundu Lisu wa kuachana na umakamu wa mwenyekiti taifa CHADEMA na kuamua kugombea uenyekiti wa Chadema Taifa akipambana na mwenyekiti wake taifa umedhihirisha tamaa na uchu wa madaraka alio nao, lakini pia umechochea vita na kukoleza uhasama baina ya wafuasi wao, na uamuzi huo unaonekana kama fujo na hujuma dhidi ya chairman wa sasa wa chadema.

Na kwa ufupi kulingana na maoni yangu,
matokeo ya uamuzi huo wa Lisu na ukosoaji wa aina ile wa lisu dhidi ya kiongozi huyu shupavu mwandamizi wa chadema kuhusu rushwa, yatakua ni pamoja na hujuma au setbacks zisizokoma katika kila atakalojaribu kulifanya Lisu ndani ya chadema, endapo atafanikiwa kuutwaa uenyekiti au ugombea urais, na kwa maana hiyo hawezi kufanikiwa katika lolote, atakutana na upinzani ambao haijawahi kukutana nao katika siasa za ndani ya chama hicho. Itakua ni fedheha sana kwake. Itakua ni zaidi ya usaliti.

Chairman wa sasa wa Chadema ni very smart politician but also very shrewd politician.
Ana uwezo wa kumpa Lisu nafasi ya kua mwenyekiti Chadema Taifa, kisha kimkakati chairman wa sasa akarejea tena kwenye nafasi hiyo kimkakati pia. Kamwe mwenyekiti huyu wasasa, hawezi kumuacha mtu aliemvuruga na kumuhujumu kwa namna mbalimbali, akaongoza kwa amani, lazima akutane na moto na joto la siasa.

Katika kuongoza taasisi, hasa hizi za kisiasa, kuheshimiana ni jambo la maana sana, na usaliti au utovu wa nidhamu ni kujichimbia kaburi la uongozi wa kisiasa mwenyewe, ndani ya taasisi iliyopo.

Unadhani Tundu Lisu anaweza kua mwenyekiti wa aina gani wa chadema endapo atafanikiwa kumshinda Freeman Mbowe mwenyekiti wa sasa wa chama hicho?🐒


Mungu Ibariki Tanzania
 
Na wewe ukiwa mwenyekiti wa chama chochote utapata nini? Mbona munahangaika sana na huyu bwana, si muache kumpa promo ya burebure, kila siku Lissu, Lissu, Lissu. Mwacheni apumue... yaani ni kama vile nyumba ndogo, ugali haupoi.
 
Yaani chawa wa ccm unatoa ushauri kwa cdm?!! 😄 🤣 😂
 
Uamuzi wa Tundu Lisu wa kuachana na umakamu wa mwenyekiti taifa CHADEMA na kuamua kugombea uenyekiti wa Chadema Taifa akipambana na mwenyekiti wake taifa umedhihirisha tamaa na uchu wa madaraka alio
Mtu aliyekaa kwenye nafasi moja kwa miaka 24, na asiyetaka kutoka yeye hana uchu wa madaraka?
 
Mtu aliyekaa kwenye nafasi moja kwa miaka 24, na asiyetaka kutoka yeye hana uchu wa madaraka?
hakuna na wala hayupo mtu wa kumtoa hata kama kibaraka anapata backup ya mabwenyenye ya magharibi hawawezi kufua dafu,

ili mpate mihemko na makasiriko zaidi 🐒
 
hakuna na wala hayupo mtu wa kumtoa hata kama kibaraka anapata backup ya mabwenyenye ya magharibi hawawezi kufua dafu,

ili mpate mihemko na makasiriko zaidi 🐒
Umetumia mihemko sana hapa.
 
Back
Top Bottom