Lissu alaani unyanyasaji wa wafanyabiashara nchini

Lissu alaani unyanyasaji wa wafanyabiashara nchini

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Katika ziara yake ya Mbeya, mheshimiwa Tundu Lissu amekemea vikali unyanyaswaji wa wafanyabiashara nchini kupitia TRA. Amesema TRA inapelekea biashara nyingi kufa na hivyo haisaidii biashara kukua

Wakati huohuo Tundu Lissu amelaani mtindo wa vitambulisho vya wamachinga vinavyouzwa shilingi 20000 na akasema hivyo vitambulisho havipo kwa mujibu wa sheria.

Huku akishangiliwa sana, Lissu amesema hayo mambo mwisho wake ni tarehe 28 October mwaka huu pale ambapo Magufuli atang'olewa madarakani.

Kwa taarifa zaidi unaweza kumsikiliza hapa chini:

Mlisema ooooh Lissu haongei masuala ya wananchi

Sasa mnaona mdogomdogo anaanza kuongeza volume taratiiiiib kuelekea tarehe ya kuanza kampeni, mambo ni fire fire!

Lissu atawanyoosha CCM kwa sababu ni jasiri, halembi, haogopi, anapiga nyundo pale msumari ulipowekwa!
 
Ila kusema kweli wafanyabiashara wamefanyiwa kitu mbaya kabisa hasahasa wa Dsm! unakuta RC anaweza kumwita mfanyabishara na kutishia kumpa kesi kama hatatoa kiasi flani cha fedha! haya yametokea ktk mikoa kama Dsm, Arusha, manyara nk na wilaya kama ile ya DC sabaya!
 
YEYE AENDELEE KUTALII NA SISI TUNAMSUBIRI ADHABU YAKE OCTOBER 28
 
YEYE AENDELEE KUTALII NA SISI TUNAMSUBIRI ADHABU YAKE OCTOBER 28
Huoni aibu??? Kuna hatihati CCM hamfikishi hata 30% ya kura mwaka huu!! Maana mmeharibu kote, si kwa wafanyabiashara si kwa wakulima si kwa wafanyakazi si kwenye ajira kwa vijana!!! Lazima mzimie mwaka huu
 
Watamchangia ili awaondole hiyo kodi, ndio maana ya nchi kushikiliwa na "mabeberu"
 
Huoni aibu??? Kuna hatihati CCM hamfikishi hata 30% ya kura mwaka huu!! Maana mmeharibu kote, si kwa wafanyabiashara si kwa wakulima si kwa wafanyakazi si kwenye ajira kwa vijana!!! Lazima mzimie mwaka huu
NADHANI UMETOKA KUVUTA BANGI KULE BA-VICHAA!
SINA MUDA NA WAVUTA BANGI ZA MCHANA
 
Kuhusu 20,000/ ya wamachinga, hii haina kosa kabisaa! Shida inaanzia pale mtu unakitambulisha, bado kuna Luba la halmashauri linataka kitu tena,

Hilo Luba ndilo limevuruga huo utaratibu mzuri wa kila aliye Mtanzania kuijenga nchi yake Kwa angalao Kodi kiduchu, na sidhani hata yeye mh Lisu akibahatika kuingia Ikulu eti autoe huo utaratibu badala ya kuuboresha, hapo tena atatengeneza upinzani wa nguvu kutoka Kwa wafanya biashara nchi nzima hasa wenye mafremu
 
NADHANI UMETOKA KUVUTA BANGI KULE BA-VICHAA!
SINA MUDA NA WAVUTA BANGI ZA MCHANA
Tukutane October. Ccm hampati hata 30% ya kura kwenye uchaguzi huu. Furahini vya mwisho mwisho. Majibu yenu mtayapata October 2020 hapo!!
 
Ndugu, unaunga mkono unyanyasaji wa wafanyabiashara kupitia ubambikizwaji wa kodi?
Weka mahesabu yako vizuri kuepuka ukadiriaji ambao wewe unaona ni uonevu, tumia efd.

Zaidi ya hapo ni propaganda za kisiasa zenye nia ovu za kuleta taharuki, na chuki kati ya wafanya biashara na serikali yao.
 
Kuhusu 20,000/ ya wamachinga, hii haina kosa kabisaa! Shida inaanzia pale mtu unakitambulisha, bado kuna Luba la halmashauri linataka kitu tena,

Hilo Luba ndilo limevuruga huo utaratibu mzuri wa kila aliye Mtanzania kuijenga nchi yake Kwa angalao Kodi kiduchu, na sidhani hata yeye mh Lisu akibahatika kuingia Ikulu eti autoe huo utaratibu badala ya kuuboresha, hapo tena atatengeneza upinzani wa nguvu kutoka Kwa wafanya biashara nchi nzima hasa wenye mafremu
Kwani before huo utaratibu wa 20000 kuanzishwa wafanyabiashara wa mafremu walikuwa wanalalamika kuhusu machinga ?
 
Back
Top Bottom